Salaam Wana JF.
Nimesoma na kuona andiko la Bwana Tundu AM Lissu kutoka Ubelgiji akijenga hoja juu ya maendeleo ya vitu na watu ndani ya eneo la Chato anapotoka rais wa sasa Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Sijaona mantiki ya Lissu kupotosha umma wa Watanzania dhidi ya maendeleo ya sasa kwa Chato. Aidha, kabla ya kujenga hoja zangu dhidi ya hoja za Lissu, nitumie jukwaa hili kukanusha upotoshaji wa kumfananisha Rais Magufuli na Madikteta wa Kiafrika akina Mobutu Sese Seko, Felix Houphouet-Boigny, Hastings Kamuzu Banda na wengineo, Kwa hoja hii Lissu umepotosha umma na awatake radhi Watanzania na Rais Mwenyewe, kamwe uwezi kuzifananisha sifa za Mobutu na JPM labda kama hujui uovu na ukatili wa Mobutu Sese Seko.
Aidha Bwana Lissu unaporejea Kitabu cha Peter Kenyon "Dictatorland, The Men Who Stole Africa" Anachokiongelea Mwandishi Peter kwa viongozi wa Kiafrika walionajisi nchi zao hakina uhalisia na kinachofanywa na Rais Magufuli kwa sasa ndani ya eneo la Chato, Mantiki ya Peter Kenyon ni kuwamulika viongozi waliotawala Afrika na kujitajilisha wao wenyewe kimaendeleo dhidi ya Umma yaani wenye nchi, Rais Magufuli anatajilisha Umma kimaendeleo badala yake binafsi ndipo hoja iliposimama hapa.
Bwana Lissu kama unavyojua ni ngumu sana kuzuia watu kusema lakini linapokuja suala la upotoshaji ni sharti tujenge hoja kuepusha kikombe hiki kutamalaki, Bwana Lissu kinachofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli katika Mkoa wa Geita wilayani Chato ni Jambo la kawaida kwa mantiki kuwa kusudio la Maendeleo hayo ni kwa manufaa ya Watanzania wote bila kujali eneo unalotoka, Umerejea awamu zilizopita ukiwataja viongozi wa awamu hizo nne kuwa hawakufanya kinachofanywa kwa sasa, Bwana Lissu nikujulishe kuwa kila nyakati na mambo yake.
Wakati wa Mwl. Nyerere alifanya kulingana na uhitaji na mipango ya wakati ule lakini pia alinyoshewa kidole na wakosoaji wake wa masuala ya maendeleo, Hivyo hivyo kwa Mwinyi, Mkapa na Kikwete kwahiyo lawama za namna hii hazikuanza leo na kamwe huwezi kuzimaliza lakini zinapopotosha zinajibiwa kimantiki, hata hivyo kila utawala utofautiana kiutawala, tunachokiona sasa sio kile tutakachokiona awamu ijayo ya sita.
Tunge jenga hoja za kumushambulia Rais Magufuli endapo tu kama angekuwa anafanya maendeleo ya namna hii nje ya Tanzania, hata mimi ningeunga mkono hoja kwa kitendo hicho lakini kinachofanywa ni ndani ya ardhi ya Tanzania, Aidha ninge hoji na kukosoa endapo tu Rais Magufuli angekuwa anafanya kwa maslahi yake binafsi na familia yake, lakini kinachofanywa ni kwa maslahi ya umma, Je nongwa inatoka wapi? Au ni husuda tu wa kisiasa kwa sababu ya itikadi za vyama vyetu?
Bwanba Lissu unadriki kulinganisha Mobutu Sese Seko ,Felix Houphouet-Boigny na Rais Magufuli, Je unajua viongozi hawa walitumia kodi za walala hoi kufanya starehe na anasa nyingine za kufuru hata zilizokuwa kinyume na amri kumi za Mungu kwa kujenga majumba ya kifahari kwa familia zao na kuwekeza mapesa mengi kwenye makampuni yaliyo je ya mataifa yao, Kinachofanywa Chato ni uwekezaji wa anasa au kwa mustakabari wa maendeleo ya watu kwa kizazi cha leo na hapo badae? Je baada ya rais muda wake yote yaliyofanyika ndani ya geita yatakuwa mali ya serikali au familia ya Magufuli?
Je, hoja ya kupinga maendeleo ya Chato inatoka wapi na ina mantiki ipi? Hata hivyo bwana Lissu unapo ongelea kisa cha Rais wa zamani wa Afrika Kusini bwana Zuma aligeuza kijiji chake cha Nkandla kuwa kama ambavyo Magufuli anaigeuza Chato Si kweli, Tuhuma za Zuma ni kujenga Jumba la Kifahari na baadhi ya mambo mengine ya anasa kwa kutumia kodi ya Wana Afrika Kusini badala ya kutumia pesa yake binafsi, na ndo maana mahakama iliamuru arudishe hela na akarudisha, Je ufanano wa Zuma na Magufuli upo wapi hapa bwana Lissu?
Nihitimishe andiko hili kwa kusema kinachoendelea mitandaoni kuhoji na kushambulia kile kinachofanyika Mkoani Geita wilayani chato kama kitu kisichokubalika kwa umma ni upotoshaji ambao sharti Watanzania tuupuuze na tuungane kwa pamoja kuendelea kuijenga nchi yetu katika dhana ya maendeleo na watu wake, Maendeleo hayana ukanda ilimradi tu kinachofanyika kiwe ndani ya ardhi ya Tanzania.
Deogratias Mutungi
Kuna dalili zote kuwa hujamwelewa Tundu Lissu...
In fact , unajibu hoja za TL kwa hasira za "tofauti za kiitikadi za kisiasa" tu na si kwa sbb ya hicho unachosema "upotoshaji"...
Unasema Magufuli asilinganishwe na kina Mobutu Seseseko, Dr. Hastings Kamzu Banda, Felix H. Bouigny na wengineo...
Na unasema kuwa lengo la kitabu la Peter Kenyon, "Dictatorland: Men Who Stole Africa" hakizungumzii viongozi wa aina ya Magufuli ambao lengo lake ni kuwaletea maendeleo watu nadhani kwa wewe kufikiri hawa wanaotajwa kwenye kitabu hicho hawakuwa na lengo hili: kuwaletea wananchi wao maendeleo..
Unaendelea kutetea hoja yako kwa kusema, kuwa, kitabu hicho kinazungumzia viongozi walioiba na kujitajirisha kupitia rasrimali za nchi zao na John Pombe Magufuli hawezi kuingia kwenye kundi la viongozi hao kwa vigezo na sababu anazozitaja Tundu Lissu na kinachofanyika Chato kijijini kwa Rais Magufuli...
Kwanza pole sana kwa sababu unadhani viongozi madikteta wezi huufanya wizi wao kama wezi au vibaka wa kawaida wanaovamia na kuvunja benki na kisha kukwapua mabegi ya pesa...
Laiti ungejitendea haki kwa kusoma kwa umakini uchambuzi wa Tundu Lissu na kisha uka - acknowledge tu na ukatulia, ungekuwa na busara sana....
Lakini Bahati mbaya kivuli cha itikadi za kisiasa zimekufunika na unaonekana u - kipofu wa fikra na kwa hiyo huwezi kuona chochote kizuri toka kwa watu wengine mnaotofautiana nao kiitikadi hususani mtu kama Tundu Lissu...
Nikuulize swali hili moja: Hivi wewe unadhani Rais Magufuli ni mtu mzuri na mtakatifu sana eti eeh...?
Pole sana. Sijui utajibu nini. Lakini najua ni vilevile tu. Nami nakuambia, UNAJIDANGANYA wewe na nafsi yako. Ninachoweza kukushauri, endelea kumwombea kama kiongozi wako ili arudi njia kuu, atoke kwenye upotofu, ukaidi na aache roho ya tamaa na uuaji...!
Ukifanya hivi, utakuwa unamsaidia sana...
Rais Magufuli hana tofauti na hao kina Felix F. B, Dr Hastings Kamzu Banda, Mobotu na wengine wanaosemwa na Peter Kenyon ktk kitabu chake...
Kwa kuwa Magufuli humuoni kusafiri nje ya nje unadhani siyo mwizi, ni mtu mwema sana na anawajali wananchi wake...
Deogratius Mutungi, dictator huwa haibi kwa njia hiyo unayodhani wewe...
Viongozi madikteta huiba kwa kutumia mifumo dhaifu ya kiutawala ya kiserikali na kinchi ambapo ktk uchambuzi wake Tundu Lissu amefafanua na kueleza kwa uzuri na urahisi sana kwa mtu yeyote mwenye akili na ufahamu mzuri kuelewa...
Dalili zote za dikteta mwizi ni haya anayoyafanya Rais Magufuli kwa kutupa kwenye dustbin vipaumbele vya kitaifa na kufanya maamuzi yake binafsi na kuyasimama kama vipaumbele vya taifa...
Viingozi wezi na madikteta hawajali sheria wala katiba. Kauli zao na maamuzi yao binafsi ndiyo sheria. Huyu ndiye Magufuli. Kwanini huoni hili...??
Viongozi madikteta mfano wa Magufuli, huendesha vikundi vya maauji, utekaji, na torture ya wapinzani wao kwa siri kubwa. Huyu ndiye Magufuli. Kwanini huoni na kuamini...??
Viongozi madikteta wa aina ya Magufuli wana hasira, hujipenda wenyewe, hawapendi watu wengine, ni wabinafsi na ma - ant-democracy. Huyu ndiye Magufuli. Kwanini huoni hili wewe...??
Hawa kina Mobutu, Houpgheiny - Bouigny, Kamzubanda na wengine ndivyo exactly walivyofanya...
Ngoja siku watu waje kuja na orodha ya mali na account za benki za kwake, rafiki zake, na ndugu zake zenye mafedha huko ndiyo utakuja kushangaa na kuishia kujijutia kwa kusema..
".....ala kumbe nilikuwa natetea shetani badala ya malaika bila kujua..!!
Pole sana. By then it could already been too late...!!