Bwana Tundu Lissu, Hoja ya Chato na Maendeleo ya sasa inajibika Kimantiki

Bwana Tundu Lissu, Hoja ya Chato na Maendeleo ya sasa inajibika Kimantiki

Ulio karibu kwa umbali wa Mwanza na Chato kwa kiwango cha huo wa Chato?
Unahangaika bure kamanda mkuu. Kwa usalama hata kama ndege kubwa imeshindwa kutua Mwanza, basi chato ni karibu.

Pia kama ilani ya Ccm ilitamka kuwa kila mkoa uwe na uwanja wa ndege sioni kama ni tatizo.
 
Hata uwanja wa ndege Mobutu aliujenga nchini kwake, lakini kijijini kwao. Na Lissu amesema kabisa, kilichofanyika huko hakikuwa kwenye mpango kazi wowote wa dira ya Taifa, bali mambo hayo yamefanyika kwakuwa rais anatokea huko. Maelezo ya Lisu yanaeleweka. Na kama kiongozi sio dictator hawezi kudhubutu kufanya upendeleo wa wazi hivyo.
Uwanja wa ndege aliojenga Mobutu kijijini kwake
20210112_211355.jpg
20210112_211401.jpg
20210112_211406.jpg
20210112_211410.jpg
 
Hatakama unajipendekeza kwa watawala ndio unaujidhalilishe kwa kiwango hiki?

Why Chato
Kwanini isiwe Sumbawanga au Tunduru?

Nimeishi sana Chato, sioni sababu ya kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa hapo
Sioni sababu ya kujenga majengo makubwa ya TRA chato
Najiuliza mahakama ya Chato inafanana na mahakama nyingine za wilaya?

Kwanini Chato na sio Geita?
 
Arusha na Moshi kuna viwanja vya ndege ambavyo ni vidogo, viwanja hivi vilijengwa kwenye kila mji wakati wa ukoloni na KIA ukajengwa kushika nafasi ya hivyo viwili, usipotoshe.

Kwahiyo huo wa Geita umejengwa ili kushika nafasi ya huo wa Mwanza kwakuwa ni mdogo?
 
Hata uwanja wa ndege Mobutu aliujenga nchini kwake, lakini kijijini kwao. Na Lissu amesema kabisa, kilichofanyika huko hakikuwa kwenye mpango kazi wowote wa dira ya Taifa, bali mambo hayo yamefanyika kwakuwa rais anatokea huko. Maelezo ya Lisu yanaeleweka. Na kama kiongozi sio dictator hawezi kudhubutu kufanya upendeleo wa wazi hivyo.
Wewe ni mwelewa sana.Nimekutunuku u doctor.
 
Rais angechagua watu wenye akili timamu wa kumtetea na kutengeneza propaganda, tena ikibidi wapigwe darasa kali sana la kutetea na kueneza propaganda. Sasa huyu ametetea nini hapa? Hakuna utofauti wa anachokifanya Uncle magu na hao madictator wengine labda utofauti wa nyakati na muda walioutumia kuyatekeleza matakwa yao.

Najiuliza hivi hakuna wenye akili huko au haya mambo hayana utetezi kiasi kila mtu anajikanyaga kanyaga tu.
Mpaka wewe umecomment!
Basi hili jambo ni zito na limegusa wengi
 
Unahangaika bure kamanda mkuu. Kwa usalama hata kama ndege kubwa imeshindwa kutua Mwanza, basi chato ni karibu.

Pia kama ilani ya Ccm ilitamka kuwa kila mkoa uwe na uwanja wa ndege sioni kama ni tatizo.

Mbona sikuelewi, huo uwanja wa Chato ni backup ya uwanja wa ndege wa Mwanza, au ni kwakuwa ilani ya ccm inataka kila mkoa uwe na uwanja mkubwa wa ndege? Maana Utetezi wako wa mwanzo naona kama unauacha.
 
Umaskini ndio unawasumbua watu mpaka wanashindwa kufikiri vizuri. Hii nchi niliyopo ina viwanja vya ndege kila mji kama sio kila kijiji, yaani unaweza ukawa na kandege kako unatoka zako Mbagala unatua Ubungo kula bata ukimaliza unaruka unatua Kibaha kumsalimia pisikali halafu unarudi kulala Kndoni
 
Mbona sikuelewi, huo uwanja wa Chato ni backup ya uwanja wa ndege wa Mwanza, au ni kwakuwa ilani ya ccm inataka kila mkoa uwe na uwanja mkubwa wa ndege? Maana Utetezi wako wa mwanzo naona kama unauacha.
Huwezi kuelewa maana unajibu mada kwa chuki.

Lakini ukweli ni kuwa ili kuwa na usalama wa urukaji ndege,kiwanja cha Mwanza lazima kiwe na kiwanja kama cha Chato,kama kuna dharula.

Mbali ya hayo,hakuna tatizo mkoa wa Geita kujengewa uwanja maana ilani ya Ccm imetanabaisha kila mkoa kuwa na uwanja wa ndege.
 
Na backup ya huo uwanja wa ndege ikaonekana Chato ndio sehemu sahihi na sio Geita mjini? Na unataka niamini kuwa Magufuli asingejuwa rais, huo uwanja ungejengwa Chato na sio Geita mjini?
 
Na backup ya huo uwanja wa ndege ikaonekana Chato ndio sehemu sahihi na sio Geita mjini? Na unataka niamini kuwa Magufuli asingejuwa rais, huo uwanja ungejengwa Chato na sio Geita mjini?
Maswali ya kichawi siwezi kujibu.
 
Salaam Wana JF.

Nimesoma na kuona andiko la Bwana Tundu AM Lissu kutoka Ubelgiji akijenga hoja juu ya maendeleo ya vitu na watu ndani ya eneo la Chato anapotoka rais wa sasa Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Sijaona mantiki ya Lissu kupotosha umma wa Watanzania dhidi ya maendeleo ya sasa kwa Chato. Aidha, kabla ya kujenga hoja zangu dhidi ya hoja za Lissu, nitumie jukwaa hili kukanusha upotoshaji wa kumfananisha Rais Magufuli na Madikteta wa Kiafrika akina Mobutu Sese Seko, Felix Houphouet-Boigny, Hastings Kamuzu Banda na wengineo, Kwa hoja hii Lissu umepotosha umma na awatake radhi Watanzania na Rais Mwenyewe, kamwe uwezi kuzifananisha sifa za Mobutu na JPM labda kama hujui uovu na ukatili wa Mobutu Sese Seko.

Aidha Bwana Lissu unaporejea Kitabu cha Peter Kenyon "Dictatorland, The Men Who Stole Africa" Anachokiongelea Mwandishi Peter kwa viongozi wa Kiafrika walionajisi nchi zao hakina uhalisia na kinachofanywa na Rais Magufuli kwa sasa ndani ya eneo la Chato, Mantiki ya Peter Kenyon ni kuwamulika viongozi waliotawala Afrika na kujitajilisha wao wenyewe kimaendeleo dhidi ya Umma yaani wenye nchi, Rais Magufuli anatajilisha Umma kimaendeleo badala yake binafsi ndipo hoja iliposimama hapa.

Bwana Lissu kama unavyojua ni ngumu sana kuzuia watu kusema lakini linapokuja suala la upotoshaji ni sharti tujenge hoja kuepusha kikombe hiki kutamalaki, Bwana Lissu kinachofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli katika Mkoa wa Geita wilayani Chato ni Jambo la kawaida kwa mantiki kuwa kusudio la Maendeleo hayo ni kwa manufaa ya Watanzania wote bila kujali eneo unalotoka, Umerejea awamu zilizopita ukiwataja viongozi wa awamu hizo nne kuwa hawakufanya kinachofanywa kwa sasa, Bwana Lissu nikujulishe kuwa kila nyakati na mambo yake.

Wakati wa Mwl. Nyerere alifanya kulingana na uhitaji na mipango ya wakati ule lakini pia alinyoshewa kidole na wakosoaji wake wa masuala ya maendeleo, Hivyo hivyo kwa Mwinyi, Mkapa na Kikwete kwahiyo lawama za namna hii hazikuanza leo na kamwe huwezi kuzimaliza lakini zinapopotosha zinajibiwa kimantiki, hata hivyo kila utawala utofautiana kiutawala, tunachokiona sasa sio kile tutakachokiona awamu ijayo ya sita.

Tunge jenga hoja za kumushambulia Rais Magufuli endapo tu kama angekuwa anafanya maendeleo ya namna hii nje ya Tanzania, hata mimi ningeunga mkono hoja kwa kitendo hicho lakini kinachofanywa ni ndani ya ardhi ya Tanzania, Aidha ninge hoji na kukosoa endapo tu Rais Magufuli angekuwa anafanya kwa maslahi yake binafsi na familia yake, lakini kinachofanywa ni kwa maslahi ya umma, Je nongwa inatoka wapi? Au ni husuda tu wa kisiasa kwa sababu ya itikadi za vyama vyetu?

Bwanba Lissu unadriki kulinganisha Mobutu Sese Seko ,Felix Houphouet-Boigny na Rais Magufuli, Je unajua viongozi hawa walitumia kodi za walala hoi kufanya starehe na anasa nyingine za kufuru hata zilizokuwa kinyume na amri kumi za Mungu kwa kujenga majumba ya kifahari kwa familia zao na kuwekeza mapesa mengi kwenye makampuni yaliyo je ya mataifa yao, Kinachofanywa Chato ni uwekezaji wa anasa au kwa mustakabari wa maendeleo ya watu kwa kizazi cha leo na hapo badae? Je baada ya rais muda wake yote yaliyofanyika ndani ya geita yatakuwa mali ya serikali au familia ya Magufuli?

Je, hoja ya kupinga maendeleo ya Chato inatoka wapi na ina mantiki ipi? Hata hivyo bwana Lissu unapo ongelea kisa cha Rais wa zamani wa Afrika Kusini bwana Zuma aligeuza kijiji chake cha Nkandla kuwa kama ambavyo Magufuli anaigeuza Chato Si kweli, Tuhuma za Zuma ni kujenga Jumba la Kifahari na baadhi ya mambo mengine ya anasa kwa kutumia kodi ya Wana Afrika Kusini badala ya kutumia pesa yake binafsi, na ndo maana mahakama iliamuru arudishe hela na akarudisha, Je ufanano wa Zuma na Magufuli upo wapi hapa bwana Lissu?

Nihitimishe andiko hili kwa kusema kinachoendelea mitandaoni kuhoji na kushambulia kile kinachofanyika Mkoani Geita wilayani chato kama kitu kisichokubalika kwa umma ni upotoshaji ambao sharti Watanzania tuupuuze na tuungane kwa pamoja kuendelea kuijenga nchi yetu katika dhana ya maendeleo na watu wake, Maendeleo hayana ukanda ilimradi tu kinachofanyika kiwe ndani ya ardhi ya Tanzania.

Deogratias Mutungi
Unapaswa kudharauliwa na kupuuzwa maana unajipitisha mdomo juujuu kama changuflani
 
Hatakama unajipendekeza kwa watawala ndio unaujidhalilishe kwa kiwango hiki?

Why Chato
Kwanini isiwe Sumbawanga au Tunduru?

Nimeishi sana Chato, sioni sababu ya kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa hapo
Sioni sababu ya kujenga majengo makubwa ya TRA chato
Najiuliza mahakama ya Chato inafanana na mahakama nyingine za wilaya?

Kwanini Chato na sio Geita?

Kama unataka kujua tabia ya Dikteta Magufuli ni sawa na ya dikteta mwenzake Mobutu Seseseko wa Zaire........Jiulize ILE FEDHA YA KUJENGA:
1. UWANJA wa ndege.
2. MBUGA YA WANYAMA BURIGI.
3. CHATO REFFERAL HOSPITAL.
4. CHUO CHA VETA CHATO.
5. STREET LIGHTS MJINI CHATO.
6. n.k.
Ni Bunge gani lilipitisha Bajeti ya miradi mikubwa kama hii kama siyo Magufuli na mtoto wa dadake Dotto James.?...?
 
Nimecheka kwa nguvu mpaka mtoto wangu mdogo ameamka usingizini. Hii aibu haijibiki boss.
We unaweza kujua kama JPM asingekuwa rais huu uwanja usingejengwa? Mbona Chafo ina barabara ya lami kwenda Bk ambayo inathamani kubwa kuliko huu uwanja? Chochote kinaweza kutokea.
 
Back
Top Bottom