Bwana wangu anaendesha bodaboda, nifanyaje?

Bwana wangu anaendesha bodaboda, nifanyaje?

Dear Money Penny

YAH: BWANA WANGU ANAENDESHA BODABODA
Mimi NI binti ambae sikuwahi kuwa kwenye mahusiano nikiwa chuoni.

Nilikuwa busy na masomo na ibada za casfeta.

Mapenzi yangu yalikuwa Kwa Yesu.

Baada ya kumaliza masomo sikupata KAZI, nikasota benchi Kwa Miaka 5, wenzangu nilisoma NAO walishaolewa na kuzaa na KAZI wanazo.

Nimevumilia lakini dadangu akaniambia tafuta bwana angalau uzae UMRI unaenda.

Siku Niko kwenye fellowship nikakutana na Kaka mmoja mlokole mwenzangu, nae NI graduate lakini Hana ajira
Amenunua bodaboda Kwa mkopo WA kampuni ya "WATU" pale Tegeta ndio anafanya nayo biashara apate kipato

Lakini ni mwaminifu, ananipenda mno na KAOKOKA,

Hatujawahi zini, Ila naogopa Sana kuolewa nae, maana kipato chake NI bodaboda Tu naona aibu mpaka aje kununua gari haya maisha yatakuwaje?

Kweli money penny bwana wangu anaendesha bodaboda lakini naona aibu kumtambulisha kwetu, ananipenda Sana nifanyaje??

Wako
Eliza."

Jamaa. Eliza anaomba msaada huku

View attachment 2724672
Kwanini anamuita bwana wake wakati bado hawajaoana wala jamaa bado hajapewa mbususu? Hawa bado wako katika kipindi cha uchumba.Hata hivyo kama wanapendana haina shida kuoana hata kama mwanaume ni mwendesha bodaboda wakioana maisha yatawanyookea mbele ya safari
 
Olewa na mpenzi wako yule anaepata basic salary 500k kabla ya makato au subr had utakapompata huyo unaemtaka mwenye uwezo wa kununua gari
 
Yaani yeye ana degree ana miaka 5 kakosa hata chakufanya ila mwemzie anakazi ya bodabodaa anataka ndoto zake zakumiliki gari amfanikishie,, ubinafsi wa hali ya juu sana na tamaa zisizomithilika.
Why so judgemental??
 
Back
Top Bottom