Ngoja nikupe vigezo
1: timu iwe inavaa jezi nyekundu simba βπ½ Na al ahly wanaingia hapa
2 : timu imiliki uwanja wake wa mazoezi βπ½ Timu zote zinaingia hapa
3: timu iwe (atlist) nimeamua kutumia na ka language uelewe ndani ya miaka 25 iliyopita imeingia makundi caf champions leagueππ½ Hapa wote tuna hicho kigezo
4: timu isiwe na mchanganyiko wa rangi za kijani na njano kwenye jezi zao ππ½ Hapa wote tumepita hadi mamelodi skuhz anavaa njano na buluuβπ½
5: timu mashabiki wake wawe hawajawahi kuitwa nyani na kocha ππ½Hapa napo naona wote tumefuzu tunaocheza
6: timu iwe haijawahi fungwa mara mbili mfululizo na ihefu fc ππ½ Hii nayo naona wote tupo sawa
7: timu iwe ina msemaji mmoja anaeeleweka kama msemaji ππ½hapa napo naona wote tumefuzu
Sasa ndugu wewe unayesema vigezo huelewi ni vipi nimejitahidi kukuelewesha kwa hivi vichache ambavo naona vitaeleweka
Lakini kabla sijaenda naomba nimalizie cha mwisho
Timu na washirika wake wawe hawajawahi piga msemaji wa timu nyingine πππ½ Hiki ndo kigezo muhimu kuliko vyote na ndo wanachokizingatia sana
Ahsante mwenye uziπ€