Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) litachezesha droo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na Shirikisho ya TotalEnergies CAF 2024/25.
Unaweza kufuatilia droo moja kwa moja Leo Jumatatu, tarehe 7 Oktoba 2024, kutoka huko Cairo, Misri: Kupitia Hapa JF
Droo itaanza na droo ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la TotalEnergies CAF saa Saba Mchana saa za Afrika Mashariki, ikifuatiwa na droo ya Ligi ya Mabingwa ya TotalEnergies CAF saa Nane saa za Africa Mashariki
Vilabu Vilivyofuzu kwa Hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa ya TotalEnergies CAF:
1. Al Ahly SC (Misri)
2. Al Hilal SC (Sudani)
3. AS FAR (Morocco)
4. AS Maniema Union (DR Congo),
5. CR Belouizdad (Algeria)
6. Djoliba AC De Bamako (Mali)
7. GD Sagrada Esperanca (Angola)
8. Espérance Sportive de Tunis (Tunisia)
9. Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)
10. MC Alger (Algeria)
11. Pyramids FC(Misri)
12. Orlando Pirates (Afrika Kusini)
13. Raja Casablanca (Morocco)
14. Stade d’Abidjan (Cote d’Ivoire)
15. TP Mazembe (DR Congo)
16. Young Africans SC (Tanzania).
Mfumo wa Droo ya Hatua ya Makundi
Timu zitagawanywa katika vikundi vinne kulingana na viwango vyao vya CAF.
Kikundi cha 4 kitakuwa na timu zenye kiwango cha chini zaidi, ikijumuisha:
- MC Alger (Algeria)
- AS Maniema Union (DR Congo)
- Djoliba de Bamako (Mali)
- Stade d’Abidjan (Cote d’Ivoire)
Droo ya kikundi hiki itazipanga timu katika moja ya makundi kama ifuatavyo:
- Mpira wa kwanza utakaochaguliwa utaenda moja kwa moja kwenye Kundi A katika nafasi ya A4.
- Mpira wa pili utaenda Kundi B katika nafasi ya B4.
- Mpira wa tatu utaenda Kundi C katika nafasi ya C4.
- Mpira wa nne utaenda Kundi D katika nafasi ya D4.
Kikundi cha 3. kinajumuisha:
- Al Hilal (Sudani)
- Orlando Pirates (Afrika Kusini)
- GD Sagrada Esperança (Angola)
- AS FAR (Morocco)
Upangaji wa timu kutoka Kikundi cha 3 utafanyika kwa namna sawa:
- Mpira wa kwanza utakaochaguliwa utaenda Kundi A katika nafasi ya A3.
- Mpira wa pili utaenda Kundi B katika nafasi ya B3.
- Mpira wa tatu utaenda Kundi C katika nafasi ya C3.
- Mpira wa nne utaenda Kundi D katika nafasi ya D3.
Kikundi cha 2. kinajumuisha:
- CRB (Algeria)
- Raja CA (Morocco)
- Young Africans (Tanzania)
- Pyramids FC (Misri)
Utaratibu wa droo kwa Kikundi cha 2 utafuata mfumo ule ule:
- Mpira wa kwanza utakaochaguliwa utaenda Kundi A katika nafasi ya A2.
- Mpira wa pili utaenda Kundi B katika nafasi ya B2.
- Mpira wa tatu utaenda Kundi C katika nafasi ya C2.
- Mpira wa nne utaenda Kundi D katika nafasi ya D2.
Kikundi cha 1, kinachojumuisha timu zenye viwango vya juu, ni:
- Al Ahly SC (Misri)
- Espérance Sportive de Tunis (Tunisia)
- Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)
- TP Mazembe (DR Congo)
Droo ya mwisho kwa Kikundi cha 1 itazipanga timu kama ifuatavyo:
- Mpira wa kwanza utakaochaguliwa utaenda Kundi A katika nafasi ya A1.
- Mpira wa pili utaenda Kundi B katika nafasi ya B1.
- Mpira wa tatu utaenda Kundi C katika nafasi ya C1.
- Mpira wa nne utaenda Kundi D katika nafasi ya D1.
UTARATIBU WA SHIRIKISHO UTAKUWA HIVYO HIVYO KAMA KB.
Vilabu vilivyofuzu kwa Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho la CAF la TotalEnergies:
1. USM Alger (Algeria)
2. CS Constantine (Algeria)
3. Bravos do Maquis (Angola)
4. CD Lunda Sul (Angola)
5. Orapa United (Botswana)
6. ASEC Mimosas (Ivory Coast)
7. Al Masry (Misri)
8. Zamalek (Misri)
9. Stade Malien (Mali)
10. RS Berkane (Morocco)
11. Black Bulls (Msumbiji)
12. Enyimba (Nigeria)
13. Jaraaf (Senegal)
14. Stellenbosch (Afrika Kusini)
15. Simba (Tanzania)
16. CS Sfaxien (Tunisia).
Tukutane Mida ya Alaasiri...