CAG: ATCL imeendeshwa kwa hasara kwa miaka 5 mfululizo

CAG: ATCL imeendeshwa kwa hasara kwa miaka 5 mfululizo

Kwaiyo bora zijiendeshe kwa hasara?

Umeona wafanyabiashara wengi walio hamia mbezi baada ya stendi kuanza? Mzunguko wa hela mbezi umeongezeka mji umepanuka maisha ya wakazi kuzunguka stendi yameboreshwa kuna faida nyingi indirect lakini sio kwa ndege
 
Waliojaribu kuonya kuwa suala la madege ni hasara tupu walidhalilishwa kuwa sio wazalendo.
Waandishi wa habari tutafutieni wale mawaziri na wabunge vilaza wa ccm waliokuwa wanachonga midomo waje watueleze misimamo yao sasa.....
 
Mmmhhh Bilion 60 unajenga uwanja gani? Au unafananisha kuchukua watu elfu 60? Embu tafiti kwanza?
Unabisha nn ww? Umeambiwa hasara imetengenezwa kwa miaka 5 mfululizo. Mbona huwa mnapenda kusifia penye hamna?
 
Kenya Airways imeingia hasara ya bilioni karibia 30 ndani ya mwaka mmoja kutokana na Corona.So issue ya Hasara kwenye makampuni ya ndege kwa kipindi hiki ni kawaida.
 
Akili sio kuuza ndege, akili ni kutafuta njia nzuri ya kupata faida. unataka kuniambia waethiopia waliletewa malaika kuongoza shilika lao likapata faida.
 
Mmmhhh Bilion 60 unajenga uwanja gani? Au unafananisha kuchukua watu elfu 60? Embu tafiti kwanza?
Nimeangalia gharama za ujenzi wa ile stadium..ni $53..hiyo loss ikiwa mara mbili uwanja unajengwa..
 
Kutengeneza Hasara tu haitoshi kama habari..., habari ya maana zaidi ni Je tutaendelea kutengeneza hasara au forecast inaonyesha tutaanza kupata faida lini au hata ku-break even...

Kama ni mwendo wa kuendelea kuchoma kodi zetu hii ni biashara kichaa
Kumbuka itatuchukua forever ku-break even na hii Pandemic inavyouma
 
Kenya Airways imeingia hasara ya bilioni karibia 30 ndani ya mwaka mmoja kutokana na Corona.So issue ya Hasara kwenye makampuni ya ndege kwa kipindi hiki ni kawaida.

Wana ndege nyingi kuliko sisi na zinazofanya safari nyingi kuliko sisi. Wao walikuwa kwenye lockdown sisi tunapeta. Kwanini wawe na hasara ndogo sisi tuwe na hasara kubwa?
 
Naomba utofauti
Kwa mfano umenunu coster M30,
Ukitegemea faida ya lak5 kwa mwezi
Lakini baada ya mwisho wa mwezi unakuta umefanya service ya ya laki 6 na mafuta umetumia ya laki 7, ila hela uliyoingiza ni laki tano tu,

So unahasara ya laki8
 
Back
Top Bottom