CAG: ATCL imeendeshwa kwa hasara kwa miaka 5 mfululizo

CAG: ATCL imeendeshwa kwa hasara kwa miaka 5 mfululizo

tutauza vipi wakati ndege zenyewe bado tunadaiwa mkuu?
 
Bilioni 60 hasara ambayo inatakiwa ilipwe ili turudi kwenye zero kwanza.
Bilioni 60 ingefanya mabadiliko kiasi gani kama ingewekwa kwenye kilimo au elimu?
Mradi kama stendi ya mabasi pale Mbezi Luis umeghalimu Tsh Billion 50..!!!! Mpaka mradi ujiendeshe kwa faida tunaitaji miaka mingapi? Hapa watu wanaodili na biashara wanaweza kutushauri zaidi.
 
Kutengeneza Hasara tu haitoshi kama habari..., habari ya maana zaidi ni Je tutaendelea kutengeneza hasara au forecast inaonyesha tutaanza kupata faida lini au hata ku-break even...

Kama ni mwendo wa kuendelea kuchoma kodi zetu hii ni biashara kichaa
 
Mradi kama stendi ya mabasi pale Mbezi Luis umeghalimu Tsh Billion 50..!!!! Mpaka mradi ujiendeshe kwa faida tunaitaji miaka mingapi? Hapa watu wanaodili na biashara wanaweza kutushauri zaidi.

Stendi,hospital,maji,umeme na barabara hizo ni huduma ambazo hata zisiporudisha faida zina manufaa kwa watumiaji na ni wananchi walio wengi. Dar ina watu 6 milion wanaotumia ile stand. Hizi ndege zina watumiaji wangapi?
 
Kwaiyo bora zijiendeshe kwa hasara?
 
Kenya Airways imetengeneza hasara ya 36 billions Kenya shilngs
Kenya Airways imetengezeza hasara kipindi cha Covid 19 wakati nchi zikiwa kwenye lockdown! Mfano Kenya airways ilikuwa inasafirisha mpaka UK Lakini UK walifungia ndege nyingi kuingia kwao na mpaka sasa hivi kama una kwenda UK lazima ujiweke quarantine kwa wiki mbili kwa gharama zako mwenyewe ambazo ni karibia £2000. Hii imewafanya watu wengi wasisafiri!

Labda ni sahihishwe kwamba Kenya Airways ilikuwa inajiendesha kwa hasara miaka mingi kabla ya Covid 19! ATC tunaambiwa ni miaka mitano sasa linalamba hasara!
 
Back
Top Bottom