CAG Atilia Shaka Malipo ya Sh Mil 830.7 Clouds & TBC

CAG Atilia Shaka Malipo ya Sh Mil 830.7 Clouds & TBC

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) imeeleza kuwa kituo cha televisheni cha Clouds kililipwa Sh 629.7milioni na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kiasi cha Sh201.4 milioni kwa ajili ya kuonyesha matangazo ya tamasha la urithi lakini hakukuwa na risiti zozote za kielektroniki zilizotolewa kuthibitisha malipo hayo.

Akizungumza leo Alhamisi Aprili 8, 2021 katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma CAG, Charles Kichere amesema kodi ya zuio ya Sh31 milioni na Sh10 milioni kutoka Clouds na TBC hazikukatwa kutoka katika malipo hayo.

“Wizara haikutimiza wajibu wake katika kukata hiyo kodi ya zuio, vilevile sikupewa ushahidi ukionyesha kuwa manunuzi ya huduma za matangazo kutoka TBC na Clouds yalipatikana kwa ushindani
 
Kweli chibu ndio maana anakwambia yeye ni kama maji kila mahala yupo pawe pasafi au pachafu.
 
Ripoti ya CAG imeonesha kuwa Clouds FM na TBC walilipwa shillingi za Kitanzania zaidi ya Milioni 800 kwa ajili ya kutangaza tamasha la Urithi, lakini malipo hayo hayana ushahidi wowote as hawakuonesha risiti ya kielektroniki (source: CAG report, 08 Apr 2021).

Kwa kuwa vyombo hivi vimekuwa mstari wa mbele kutetea wa nyonge na kuonyesha kuwa ni wazalendo, naomba wana JF wote tuwaombe warudishe fedha za wanyonge ili mama aendeleze kazi ya ujenzi wa nchi yetu. walijifanya wapo karibu na serekali ya awamu ya 5 kumbe ni mchwa.

Haiwezekani ku tweets tu ndo igharimu milion 600 zote hizo.

Rudisheni fedha zetu Clouds FM na TBC tafadhali
Malipo alifanya serkali, Mkaguzi anaanzia kwenye cheques zilizotolewa, atapewa na mlipaji yaani serkali. Sitegemei kwamba ni wajibu wa mlipwaji kutunza risiti unless unataka kuonyesha malipo ni hewa, in which case bado utaanzia kwa mlipaji je alimlipa nani? Ila ukisema hakuna ushahidi kwamba walitangaza kuasi cha thamani hiyo, hapo nitaelewa: hiyo wenyewe huita value-for-money audit. Hata hivyo bado sijaona utahamishaje jukumu la kujieleza kutoka kwa mlipaji: je, alilalamika?
 
Hii nchi yetu kwa nini kila kona kuna ubadhirifu wa fedha za umma? tatizo ni viongozi au nini haswa? au hakuna wataalamu wa kudhibiti?! ehh!! Mungu.
 
Sasa kwa ushahidi huu DPP anangoja nini kuchukua hatua? mambo yako hadharani kabisa, yaani ni utopolo km hizi report haziwi na impact au action yyote, ni bora wakae nazo kimya , wanokula wale tu.
 
Sasa kwa ushahidi huu DPP anangoja nini kuchukua hatua? mambo yako hadharani kabisa, yaani ni utopolo km hizi report haziwi na impact au action yyote, ni bora wakae nazo kimya , wanokula wale tu.

Acheni mchezo na hela jamani! Humu tunajifanya kulaani hato malipo kwa sababu hatujazifikia hizo hela. Lakini mngekutana nazo ana kwa ana ndiyo ungejua mwili unavyobadilika ghafla! Hapa ni fursa tu haijapatikana kuzifikia hizo hela kwa kila mmoja wetu!
 
watanzania wnaangalia na kusubiria je, vyombo vyetu vitachukua hatua kwa wahusika au wataamua kukaa kimya?!
ili watanzania wawe na imani basi hakuna budi kuwachukulia hatua kila mtu au kiongozi aliye husika au kujihusisha na ukwapuaji wa fedha za watanzania. kamwe lisibaki jiwe juu ya jiwe.
 
inasikitisha wakati tuliambiwa dai risiti hata ukinunua penseli au peni ,kama risiti haikutolewa wote munakosa mtoa huduma na mpokea huduma
Na swali je ni mwaka 19/20 tu au na miaka ya nyuma yake haya madudu?
Namshukuru raisi wa jamhuri ya Tanzania muheshimiwa Samia kwa uwazi na ukweli
 
Malipo alifanya serkali, Mkaguzi anaanzia kwenye cheques zilizotolewa, atapewa na mlipaji yaani serkali. Sitegemei kwamba ni wajibu wa mlipwaji kutunza risiti unless unataka kuonyesha malipo ni hewa, in which case bado utaanzia kwa mlipaji je alimlipa nani? Ila ukisema hakuna ushahidi kwamba walitangaza kuasi cha thamani hiyo, hapo nitaelewa: hiyo wenyewe huita value-for-money audit. Hata hivyo bado sijaona utahamishaje jukumu la kujieleza kutoka kwa mlipaji: je, alilalamika?
Value For Money Audit ..nimekuelewa sana

Sent from my VFD 301 using JamiiForums mobile app
 
Kwa TBC kama imeingia kwenye akaunti za serikali kwa control number, hamna hoja chapeni kazi wacheni majungu!
 
Back
Top Bottom