CAG: Mradi wa ujenzi wa Uwanja Arusha ulikadiriwa bilioni 187, mkataba ukasainiwa bilioni 338

CAG: Mradi wa ujenzi wa Uwanja Arusha ulikadiriwa bilioni 187, mkataba ukasainiwa bilioni 338

Wewe pia ni Muhanga wa Hesabu, Unawezaje kufananisha vitu ambavyo havifanani????
Mbona mnapenda kuanza na kebehi?
Uwanja wa Everton unabeba mashabiki takriban 53,000 na wa Arusha unabeba mashabiki 30,000 almost Nusu?
Uwanja wa Everton umegharimu zaidi ya mara 7 ya uwanja ambao ni nusu ya ukubwa wake. Kwa hizo hesabu yako. Kwa hizo hesabu zako uwanja wa Arusha bado ni nafuu sana maana ulipaswa kugharimu angalau £300 milioni.
Uwanja wa Talanta wa Kenya ambao ni mara mbili ya uwanja wa Arusha utagharimu £270,000,000.00. Ukilinganisha kwa hesabu za juu juu, basi wa Arusha ungegharimu £135 milioni ambazo ni zaidi ya hiyo £99 milioni ya mchina.
Hata tukirudi kwenye Uchumi; Unajua nguvu ya Uchumi wa Uingereza wewe?
mfuko wa Cement ukiuzwa kule 52,000 inaonekana bei ya kawaida wakati kwetu unauzwa shs 17,000
Sehemu kubwa ya gharama za ujenzi wa stadium haitokani na simenti au nondo. Gharama ni katika miundo mbinu ya umeme, mawasiliano, usalama, matangazo n.k. ambavyo vyote tunaagiza kutoka nje. Na hata hiyo simenti haipimwi kwa mifuko bali kinachonunuliwi zege inayokuja kumwagwa tu kwenye eneo husika. Na hata kwenye huo mfano wako wa simenti, bei uliyotaja ni mara tatu tu ya bei ya huku kwetu. Na mara nyingi katika mradi kama huu wanaweza hata kuagiza simenti kutoka Kenya au nchi nyingine ambako ina bei nafuu.
Narudia tena: Usifananishe vitu ambayo havifanani.....ukubwa wa uwanja, nguvu ya Nchumi wa Nchi husika nk nk
Nguvu ya uchumi wa nchi inahusika vipi hapa kwenye gharama za ujenzi?

Nimetoa mfano wa Everton kwa kutaka kuonyesha kuwa gharams ya kujenga stadium ya kisasa ni kubwa bila kujali nchi husika. Hao waliotoa estimates hawana uzoefu wa ujenzi wa stadium za aina hiyo ndio maana wakaja na estimate ya chini sana. Hata CAG ameliona hilo.

Na kwa vile imejengwa kwa hiyo bei sitashangaa kama baada ya muda mfupi tutatumia kiasi hicho hicho cha pesa kwa ajili ya ukarabati kama ilivyo kwenye uwanja wa Mkapa.

Amandla...
 
Kummama mae walai, ndio maana hawa ******* wakiambiwa katiba mpya wanafura, wako radhi kumwaga damu za wenzao ili maslahi yao wayalinde.

Mwaka wa ngapi huu ripoti ya CAG inakuja na madudu lakini hakuna hatua inachukuliwa.
Kwa loopholes za kwenye katiba yetu uwajibikaji ni ngumu saana, na tutazidi kudumbukia kwenye shimo hatutatoka kamwe
 
Wakati mwingine namwona CAG anaongea maneno ya kisiasa zaidi. Makadirio na Actual payment ni vitu viwili tofauti kabisa nilitegemea yeye kama CAG aje na taarifa ya kitaalamu zaidi kama mkataba ni halali ama la! Sasa anatuachia sisi wananchi ndio tufanye ukaguzi ama nini?
Msayngay
 
CAG namuonaga kama mpiga kelele tuu hana ishu, kila siku utumbo kibao Ila hakuna hatua yoyote
 
Huko si ndo wamesema polisi watavazaa sare maalumu kutangaza utalii
 
Wakati mwingine namwona CAG anaongea maneno ya kisiasa zaidi. Makadirio na Actual payment ni vitu viwili tofauti kabisa nilitegemea yeye kama CAG aje na taarifa ya kitaalamu zaidi kama mkataba ni halali ama la! Sasa anatuachia sisi wananchi ndio tufanye ukaguzi ama nini?
Mkataba unakuwaje halali ikiwa hata mzabuni hajashindanishwa?
 
We Kichere mzima kweli wewe ?

Kwa nini unasema tatizo ni makadirio ? Unajuaje tatizo sio budget padding, hela imepigwa ?

Na kama tatizo ni makadirio, kwa nini unasema kungekuwa na ushindani wa wakandarasi gharama ingeshuka ??? Huoni unaji contradict ?

Halafu skendo la mabilioni na mabilioni lakini hela ambayo unaitaja haijatumika sawa ni ka bilioni tatu ka gharama za majadilioano. Na suala lenyewe unaliita

"mapungufu"!

Umeufyata!

Mapendekezo unashauri wizara ya michezo ijiimarishe katika usimamizi wa manunuzi. Hivi hili ni suala la wizara ya Michezo tuuuu ????? Mradi kama huu haupiti cabinet, Ikulu, bungeni ? Na mfumo mzima wa kiserikali na kisheria katika michakato ya manunuzi ya umma haupaswi kuangaliwa ?? Ni kawizara ka michezo!

Umemwogopa Samia ??? Umeufyata mkia mwanamme mzima.

Na kwa nn huwa hutaji specific protocols, taratibu zilizopo zilizovunjwa ???

Unawaambia wakajitazame. Umeufyata. Umelamba utamu wa kuwa kwenye system. Huna uzalendo. Who you taking us for, fools ???

Nilitegemea weledi zaidi ya huo Kichere. Siku zile za Tambaza na Shycom kumbe ulikuwa unakimbiza kwa kukariri tu. Umechemka mbaya sana.
 
Makonda anaonewa, aliyehusika ni Damas Ndumbaro kama waziri, Mwnafa naibu, Msigwa katibu mkuu wakati huo Makonda alikuwa mkuu wa mkoa.
Hiyo rushwa ni kubwa mno kufanywa na waziri mmoja tena mdogo vile.
Hiyo ni Joint embezzlement deal ina baraka zote kutoka presidency.
Kwa kauli ya leo, nimeamini Rais anahofia utawala wake kufupishwa halfway kama yule kaka yake
 
Ripoti ya CAG, ikiunganishwa na ripoti ya Ile tume ya Kodi itakuonesha kwa Nini Mimi natamani kujifia kila ninapo LIPA Kodi
Nauliza katika Ili la uwanja wa mpira Makonda na yule aliyekuwa mbunge wa Arusha wanaponaje?
Maccm majizi jaman jaman jaman.
 
Wakati anaapishwa mbona mamaduro alisema hadharani anampeleka kwa kazi maalum? Kenge akil zetu bana, ndio kazi yenyewe ati, nyie mlifikiri ni kupanga landrover barabarani! Mzigo ushaenda mahali salama, tunaandaa kingoma cha kuwasuta wanaochonga! Tarumbeta zipo njiani toka china



View: https://www.youtube.com/watch?v=nhk6vELtTjA
 
Back
Top Bottom