CAG: Mradi wa ujenzi wa Uwanja Arusha ulikadiriwa bilioni 187, mkataba ukasainiwa bilioni 338

Mkataba unakuwaje halali ikiwa hata mzabuni hajashindanishwa?
Single source ni njia halali ya kutafuta mkandarasi. Sio lazima wazabuni washindanishwe. Single source inatumika kwa kibali maalum.

Amandla...
 
Huyo CAG report zake hazinaga meno so sioni impact yoyote yenye maana katika hizo report sana sana zinachangia kuwaumiza watanzania wanaposoma hizo report na kuona madudu yanayo fanywa na watumishi wa serikali jinsi wanavyo tafuna Kodi zao inachangia kuongeza chuki hasira na makasiriko Kwa wananchi dhidi ya serikali Yao kwasababu report zinasomwa Kila mwaka halafu wale wezi wote waliipiga hizo pesa na kuhujumu uchumi hatuoni kabisa wakichukuliwa hatua zozote zile
 
Yeye ni kusoma report tu
Bora anyamaze

Ova
 
Single source ni njia halali ya kutafuta mkandarasi. Sio lazima wazabuni washindanishwe. Single source inatumika kwa kibali maalum.

Amandla...
CAG kasema hakuonyeshwa mazingira yoyote ya dharula inakuwaje wakatumia single source?
 
CAG kasema hakuonyeshwa mazingira yoyote ya dharula inakuwaje wakatumia single source?
With all due respect CAG si mtaalam wa ujenzi. Kibali cha kutumia Single Source kinatolewa na PPRA, sio yeye. Wao wakiridhika, CAG hana la kusema. Alipaswa kuwahoji pia PPRA kwa nini walitoa kibali na sio kuishia kwa mwenye mradi. Awaulize kwa nini hawakushauri ifanyike pre qualification kama walikuwa wanakimbizana na muda na walitaka makandarasi wenye uwezo tu ndio waombe kazi. Mimi binafsi nahisi kweli muda wa kualika tenda ulikuwa hautoshi hasa kama michoro ilikuwa haipo.

Amandla....
 

Unajua nyie mkishasikia uwanja wa mpira au uwanja wa ndege basi mna anza tu kufananisha kama vile unafananisha mchele wa mbeya na mchele ya Shinyanga
Mfano ukisikia Mwanza (MWZ) International Airport au Kilimanjaro (JRO) International Airport Halafu ukutane na mtu kama wewe una anza kufananisha na Singapore Changi (SIN) international airport au, Beijing Daxing PKX international airport au pengine; Doha Hamad (DOH) international Airport
Tofauti yake ni kubwa ni kama vile kufananisha Toyota Passo na V8 japo vyote ni International airport
Sawa na wewe kufananisha Arusha Stadium na Everton stadium Kweli? eti kwa sababu tu vyote ni viwanja vya mpira
 
Tofauti ya uwanja wa Everton na wa Arusha ni nini ukiondoa idadi ya watazamaji? Au ulitaka nifananishe wa kiwanja cha Ali Hassan Mwinyi Tabora? Au Nyamagana?
Ukitaka kujenga uwanja wa ndege wa Dodoma haulinganishi na ule wa Songwe bali unaangalia wa Doha, Dubai n.k. ili kujifunza.
Pamoja na yote hayo nimekuwekea mfano wa uwanja unaojengwa Nairobi. Au wakenya nao wametuzidi kiasi hatuwezi kujifananisha nao?

Amandla...
 
kwani uwanja wa Benjamini Mkapa ulitumia tsh ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…