CAG Prof. Assad astaafu, Charles Kichere ateuliwa kuwa CAG mpya

CAG Prof. Assad astaafu, Charles Kichere ateuliwa kuwa CAG mpya

Hivi Tanzania nayo ina mungu ?ameacheje uovu wa viwango hivi kwa maskini wanaomlilia kila siku aponye nchi yao ? Tuendelee kushtaki kwa mungu au au twende front tu.ngoja nkanywe bia pale Hugoz nikitafakari mambo .
 
Kwa mtu mwenye mapenzi mema ya matumizi bora ya fedha za serikali CAG kama Assad angemuongezea muda ili kupunguza mianya ya matumizi mabaya ya fedha maana Prof. Assad alijipambanua kuwa ni mtu safi
Hapa ndipo nina poshindwa kumuelewa magufuri yaan haeleweki, kutwa kujipambanua kwamba anachukia wapigaji huku vichwa kama Assad anavichukia
 
Subira the princess hali ni mbaya sana watanzania wengi ni tuu wajinga tunashangilia hatuelewi juzi mkaguzi mwenyewe alitoa ripoti inayoonesha Magufuli ametumia bilioni 5 hivi ,kisheria ile ripoti ilitakiwa isomwe na watanzania tujue kinachoendelea matokeo yake baada ya Muda Assad kuanika uozo wote wa namna fedha ilivyotafunwa ,Spika wa bunge akamletea Assad majungu eti huyu bwana hafai kuwa mkaguzi ,ohh hawezi,lakini kifupi ni kuwa magufuli ni Fisadi wa kutisha hebu fikiria Spika wa bunge kwenye ile ripoti anatumia shilingi 128milion kwa ajili ya matibabu!!wabunge wenzake pamoja na Rais wamekaa kimya bila ile ripoti kuisoma baada ya kuwaona watanzania ni mabwege ,sasa leo jiwe anaona ni heri kumwondoa Assad ili aendelee kutafuna hizo fedha,
 

Attachments

  • c4vGt3Nh7QCrVkVB.mp4
    2.5 MB
Mshenzi Mkubwa wewe, udhaifu wake upo wapi? Wewe kama Mme wako ni dhaifu kitandani usichukulie wanaume wote ni dhaifu...

Acha kuokota maneno huo mtandaoni na kuleta humu ndani.
 
Lakini hajawahi kuwa CAG , ngoja tuone na tupime utendaji wake akiwa CAG.
 
Tutamkumbuka sana mwanazuoni aliyetukuka Prof. Mussa Assad. Alikuwa ni mtu jasiri, msomi na anayesimamia kile anachokiamini!

Kwa namna nilivyomuona huyo Kichere wakati ule alipotumbuliwa kwenye Ukamishna wa TRA kutokana na ulegelege wake kwenye maamuzi, na mwisho wa siku kupozwa na URAS wa Njombe, hakika tusitegemee miujiza.

Anaonekana wazi atakuwa ni CAG wa ndiyo mzee! Hana ujasiri wowote ule wa kuikosoa wala kuishauri serikali yake tiifu ya ccm! Zaidi atafukia madhaifu yote ili tu kuulinda ugali wake.
 
Awamu hii wanaotakiwa ni wale watu dhaifu, weledi duni na wanafiki wa kusifu na siyo critics. Ndiyo sababu kubwa ya mambo mengi kutokwenda kiuhalisia. Hatuitumii vizuri faida ya kuwa watu wengi wenye uwezo na fikra tofauti.
 
Yani kila siku mnalia humu ajira ni bomu, kaondolewa kipenzi chenu mmeanza kumtetea, hao mnaowapenda wakiendelea kuwa maofisini vijana watapata ajira lini?!

Nani sio bomu nchi hii?!
 
wasalaam, kuna habari zinasambaa kwa kasi sehemu mbalimbali nchini kwamba CAG mpya mh kichere ni dhaifu kutoka na historia yake ya utendaji huko nyuma. Habari zinasema kwamba bwana kichere ni mtu wa ndio mzee na kuanzia sasa ukaguzi wa hesabu za serekali utafanywa na serikali yenyewe kwa maelekezo kutoka pale nyumba nyeupe.

Tusubiri muda ni rafiki huenda ni majungu tu labda watu wanazusha. Maendeleo yana vyama usipochagua ccm hakuna kuletewa maendeleo.
Ova.
Aliushindwa ukamishna ataweza u CAG?
 
Back
Top Bottom