CAG: TSh. milioni 140 ambazo Wizara ya Maliasili na Utalii iliilipa kampuni ya Wasafi hazikuwa na Mkataba uliosainiwa

Kifo humstiri mtu na pia kifo Inakuwa njia pekee inayomnyamazisha mtu aliyejifanya mwema na kuwapa watu nafasi ya kujua maovu yake ambao alijigamba kuyasitiri katika Wema. Sasa tunaaza kuyajua Haya Yote. RIP mwenda zako but kuna watu itawabidi wakalie kwenye kaburi aise maana si kwa kuumbuka huku
 
Kibwangala amejikita kuwahoji maprofessa pale muhimbili methodology za kufanya utafiti ili atusahaulishe namna pesa ilivyotafunwa pale maliasili kwa kisingizio cha kutangaza utalii wa ndani......watu wanalipana pesa kama hazina mwenyewe...
 
Mkurugenzi Clods/CMG na viongozi wengine wachukuliwe hatua za kisheria,
TAKUKURU chukueni hatua ushahidi huo hapo kwenye ripoti ya CAG
 
Alafu Kigwangalla anakuambia pesa ya kulipia zike pikpik za Mo ni pesa alizopata kwa kuuza mchele🤣🤣🤣
 
Kwa hiyo Kigwangwalla na Diamond walipiga deal na kutafuna pesa za umma?
 
Hawa si wapo? Wazirejeshe tu hakuna namna nyingine! Dpp fanya jukumu lako hapa kwani ndio jukumu lako! Ile mahakama ya mafisadi inaelekea kupata wateja wa kutosha Sasa! Dpp amka fanya kazi yako kwani ushahidi unao na huhitaji uchunguzi mwingine!
 
Nje ya box yupo aliifanya wizara kama mali yake,sote tunakumbuka ugomvi wake na katibu mkuu wake, halafu leo hii ndio wa kwanza kumnanga mwendazake akijifanya msafi, si ajabu hata hao Wasafi hawakupata kitu.
 
😂😂😂 sitashangaa mkuu.
Hata mimi nakubaliana nawe , kwa ahadi kuwa watapewa dili lingine,katibu mkuu na waziri wote wapo na sasa katibu mkuu ni waziri na aliyekuwa waziri kawa mchunga ng'ombe,hawa wote wapo na Wasafi nao wapo ,mahakama zipo, tuanzie hapo .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…