CAG: Uwanja wa Ndege Chato ni mradi usio na faida

CAG: Uwanja wa Ndege Chato ni mradi usio na faida

Sijui hapo unataka kusema Nini? Kwamba watu waendelee na hofu aliyoipandikiza Magufuli? Au sijui unataka kusema nini!
Watanzania tuna unafiki mwingi. Enzi huo uwanja unajengwa, CAG alikuwepo! Lakini hakumshauri Rais wa wakati huo kusitisha ujenzi wake.

Hivyo Taifa linatakiwa liwe na watu wenye ujasiri wa kumwambia Mfalme ukweli. Kama yuko uchi, aambiwe ukweli, ili ajisitiri!

Kuna makosa mengi Rais aliyepita, aliyafanya! Lakini wasaidizi wake walitumia muda wao wote kumsifia na kumtukuza tu! Badala ya kumshauri na kumuambia ukweli.
 
Watanzania tuna unafiki mwingi. Enzi huo uwanja unajengwa, CAG alikuwepo! Lakini hawakumshauri Rais wa wakati huo kusitisha. Na sababu kubwa ilikuwa ni kulinda ugali wao.

Hivyo Taifa linatakiwa liwe na watu wwnye ujasiri wa kumwambia Mfalme ukweli. Kama yuko uchi, aambiwe ukwli, ili ajisitiri! Kuna makosa mengi Rais aliyepita, aliyafanya! Lakini wasaidizi wake walitumia muda wao wote kumsifia na kumtukuza! Badala ya kumuambia ukweli.
Mi naonaga mda mwingine watanzania hatunaga hata maana Jiwe kapanua barbara ya morrocco mwenge kwa fedha za sherehe za uhuru na baadae akaamuru pia fedha za uhuru zikapanue barabra ya mwanza airport lakini kuna watu hapa wanajidai kufata utaratibu wa zabunimili wapige dili zao lakini matokeo sifuri. Kkikubwa tunataka matokeo zabuni ni maneno tu.
 
Kipindi kile alisemaje ?

Kama kipindi kile alikaa kimya kwa kuogopa Mamlaka tunajuaje kama kipindi hiki hasemi kila anachotakiwa kusema ili mradi tu kuridhisha mamlaka ?

Hii nchi unafiki mwingi sana kwamba ingebidi aombe wananchi msamaha na ajiondoe kwenye hio kazi sababu inaonyesha ni bendera fuata upepo
 
CAG kwa hili sijui kama yuko sahihi Mapori yaliyoko Kule mijambazi ya Rwanda na Burundi ilikuwa inasumbua sana

Magufuli akatangaza kuwa yale maeneo ni mbuga za taifa sababu kuonekana mbugani kama sio mtalii unapigwa risasi .umefuata nini mbugani

Kwa kuanzisha mbuga akawa kakomesha utekwaji magari na mabasi kwenye yale Mapori sababu majambazi wanyarwanda na warundi walijikatia mapori yale wengine wakaanzisha hadi mashule na vituo vya ujambazi .Tatizo hilolimekuweko Serikali zote Magufuli Ndie alibadilisha hiyo hali

Tatizo Serikalini coordination hamna kilichotakiwa ni wizara zote kushirikiana ku push agenda ya utalii kule ili uwanja uwe active
Lakini pia Jeshi huo uwanja ungewasaidia!!

Sasa tuchukulie mfano Serikali iseme hauna faida ufungwe wanatakaje na zile mbuga zifungwe wanyama warudishwe walikotoka na mapori yale waachiwe Majambazi wa kinyarwanda na kirundi waendelee kuteka mabasi na magari na Kuua raia?

Anyway huo ni uamuzi wa Serikali

Ila Nadhani siku ingine CAG akifanya ukaguzi ni vizuri kupata information za kutosha zaidi ya hizo za profit and loss
 
Kipindi kile alisemaje ?

Kama kipindi kile alikaa kimya kwa kuogopa Mamlaka tunajuaje kama kipindi hiki asemi kila anachotakiwa kusema ili mradi tu kuridhisha mamlaka ?

Hii nchi unafiki mwingi sana kwamba ingebidi aombe wananchi msamaha na ajiondoe kwenye hio kazi sababu inaonyesha ni bendera fuata upepo
Unayasema hayo huku rohoni mwako unajua kabisa kuwa jiwe alitumia mabavu kwenye miradi mingi bila kufanya tathmini ya kitaalam
 
Back
Top Bottom