CAG: Uwanja wa Ndege Chato ni mradi usio na faida

CAG: Uwanja wa Ndege Chato ni mradi usio na faida

Ni matumizi mabaya ya madaraka kwa kukiuka kanuni za fedha kwa makusudi kabisa kwa kuwa kiwanja cha ndege kinajengwa kwa aliyekuwa mkubwa wa nchi.Chondechonde viiongozi wetu tuondokane na tabia hii ya kinafiki ya kujipendekeza kwa watawala mpaka kupelekea kutozingatia sheria na kanuni mbalimbali zinazohusu fedha nk
 
Unafiki hautoisha nchi hii, CAG acha hizo kabla ya awamu hii hukuwepo?

professa Asad hakubumbabumba mambo ili kumtukuza mkuu hayati.
Ungesema kweli uwe shujaa wa kulipigania taifa.
 
Na kwa mitazamo hii ndio maana tupo hapa watu kama nyie ambao ni wafuasi wa mtu ni janga kwa mustakabali wa hili taifa..., mnachukulia nchi kama ushabiki wa simba na yanga, wao na sisi na sio kipi ni sahihi na nini sio sawa....

Binafsi sio mfuasi wa mtu yoyote bali ni mwananchi wa hii nchi, kwa mantiki hio fikra zangu ni kuongelea na kupinga lolote popote kama nikiona halipo sawa, be it kalifanya nani au mtu wa mlengo gani wa Kisiasa...

And right now mtu ambaye anatakiwa kufukua madudu kama anaonyesha yale tu ambayo mtawala hawezi kupingana nayo, it means na yeye ni walewale tu...
Nyie ndio mnaleta ushabiki kwa sababu mnapingana na kila CAG kisa amemsema mtu wenu vibaya...ofisi ya CAG ilikuwa ikiibua madude tawala zote wala sio kwa Magufuli tu, ila kwa Magufuli anashambuliwa, kwa nini?
 
Nyie ndio mnaleta ushabiki kwa sababu mnapingana na kila CAG kisa amemsema mtu wenu vibaya...ofisi ya CAG ilikuwa ikiibua madude tawala zote wala sio kwa Magufuli tu, ila kwa Magufuli anashambuliwa, kwa nini?
Unaweza ukaleta hata Post moja humu niliyoshawahi kumsifia JPM ?

Mimi sio cheerleader kama mtu anafanya mazuri ni kazi yake ndio aliyochaguliwa kufanya kuanza kwangu kumpigia makofi kwangu naona ni kupoteza rasilimali muda..., kwa yoyote anayekosea mimi huwa nipo critical sababu ninamlipa kwa kutumia kodi yangu hence nahitaji value for my money...

Sasa huyu (siongelei Assad huyu jamaa) kama aliweza kuficha huu uchafu kipindi cha JPM ni mangapi anaficha sasa ili aje kuyaongea awamu ijayo ?
 
Kwani nani hajui? bora Assad aliongea huyu alikuwa kimya na kuunga mkono, sasa hivi tunajuaje kama sio speaker ya propaganda na fagio la kumsafishia mama njia ?

Kama aliweza kuficha mambo hapo mwanzo kwanini asifiche mengine sasa..., Vipi kuhusu return on investment ya hizi safari za sasa kuna lolote anaongelea hapo ?

Huyu jamaa inaonekana anaweza kusema lolote au kuficha lolote depends na nani anamwambia aseme nini, mimi kama mlipa Kodi sina Imani na huyu Bwana / Hiki Kitengo
Hiyo ni imani yako hakuna mtu mwenye haki ya kukufanya usiamni unacho kiamini.

Ila ukweli jiwe aliharibu sana maisha ya watanzania na kutumia hivyo fedha za umma.
 
Boss sio unafiki, maoni kama hayo miaka miwili iliyopita ingeweza kuwa career suicide, Nape na Ndugai wanajua vizuri
Nape kimbelembele chake choote kilikwisha hadi akaamua kupiga magoti
 
Afadhali uwanja upo hata mkisema mpaka mapovu yawatoke ni sawa tu maana Geita utabaki uwanja wao! Ile sehemu mmepora madini sasa hivi kumebaki maandaki maana hata mchanga umabebwa, no replacement!
Madini mliobebea yakiisha siku moja tutapata watalii watakaokuja kutembelea mashimo waliochimba Geita!
 
Afadhali uwanja upo hata mkisema mpaka mapovu yawatoke ni sawa tu maana Geita utabaki uwanja wao! Ile sehemu mmepora madini sasa hivi kumebaki maandaki maana hata mchanga umabebwa, no replacement!
Madini mliobebea yakiisha siku moja tutapata watalii watakaokuja kutembelea mashimo waliochimba Geita!
Vipi kuhusu Chato kuwa mkoa bado mnaendelea kuota?
 
Watanzania tuna unafiki mwingi. Enzi huo uwanja unajengwa, CAG alikuwepo! Lakini hakumshauri Rais wa wakati huo kusitisha ujenzi wake.

Hivyo Taifa linatakiwa liwe na watu wenye ujasiri wa kumwambia Mfalme ukweli. Kama yuko uchi, aambiwe ukweli, ili ajisitiri!

Kuna makosa mengi Rais aliyepita, aliyafanya! Lakini wasaidizi wake walitumia muda wao wote kumsifia na kumtukuza tu! Badala ya kumshauri na kumuambia ukweli.
Mzee unajua huyu CAG hii ni ripoti yake ya pili, alitoa ya kwanza baada ya jiwe kufa
 
Sio sgr tuu tukianza kuongelea miradi tanzania hii ni mingi ikiwemo chato. Kukosa mlengo kama taifa na dira kuu ni chanzo cha yote aya.

Nilitaka sahau mzizi wa yote aya ni CCM. Pamoja na kuhusisha vyeo vya kiutendaji pamoja na siasa
Ulitaka miradi ianze lini?
Kama si maamuzi magumu Kuhamia dodoma ingekuwa ndoto, SGR n.k hapa kukaa na kulalamika ujinga haisaidii, tafuteni hela mmalize SGR NA bwawa la umeme!
 
Hivi uwanja wa ndege wa Chato unatofauti gani na Uwanja wa Ndege wa Musoma unaojengwa? Au wa Mtwara? Hizo faida anazotaka CAG ni zipi? Zionekane baada ya mda fani? Maana nina hakika ata ujenzi wa terminal 3 Mwaimu Nyerere bado hatujaanza kupata faida

Sent using Jamii Forums mobile app
Usizungumze kwa mahaba bila weledi.

Chato imejengwa airport, Musoma ni airstrip. Economic activities zilizopo Mtwara utalinganisha na za Chato? Ujue Mtwara kuna visima vya gas, kuna Bandari, ni makao makuu ya mkoa, wakati Chato ni kijiji chenye hadhi ya Wilaya, inayozidiwa kwa mbali na business settlements kama Makambako.

Chato wangeweza kujengewa airstrip ndogo, ingetosha sana kwa matumizi ya kawaida. Kuweka uwanja wa ndege kama ule Chato ni sawa na kuchukua semi trailer kwaajili ya kwenda kubeba gunia mbili za dengu.
 
Kipindi kile alisemaje ?

Kama kipindi kile alikaa kimya kwa kuogopa Mamlaka tunajuaje kama kipindi hiki asemi kila anachotakiwa kusema ili mradi tu kuridhisha mamlaka ?

Hii nchi unafiki mwingi sana kwamba ingebidi aombe wananchi msamaha na ajiondoe kwenye hio kazi sababu inaonyesha ni bendera fuata upepo
Kipindi like kipi? Ameteuliwa CAG 2019, kabla ya kutoa ripoti yake ya kwanza jiwe akawa keshakufa
 
Back
Top Bottom