CAG: Uwanja wa Ndege Chato ni mradi usio na faida

Ni matumizi mabaya ya madaraka kwa kukiuka kanuni za fedha kwa makusudi kabisa kwa kuwa kiwanja cha ndege kinajengwa kwa aliyekuwa mkubwa wa nchi.Chondechonde viiongozi wetu tuondokane na tabia hii ya kinafiki ya kujipendekeza kwa watawala mpaka kupelekea kutozingatia sheria na kanuni mbalimbali zinazohusu fedha nk
 
Unafiki hautoisha nchi hii, CAG acha hizo kabla ya awamu hii hukuwepo?

professa Asad hakubumbabumba mambo ili kumtukuza mkuu hayati.
Ungesema kweli uwe shujaa wa kulipigania taifa.
 
Nyie ndio mnaleta ushabiki kwa sababu mnapingana na kila CAG kisa amemsema mtu wenu vibaya...ofisi ya CAG ilikuwa ikiibua madude tawala zote wala sio kwa Magufuli tu, ila kwa Magufuli anashambuliwa, kwa nini?
 
Nyie ndio mnaleta ushabiki kwa sababu mnapingana na kila CAG kisa amemsema mtu wenu vibaya...ofisi ya CAG ilikuwa ikiibua madude tawala zote wala sio kwa Magufuli tu, ila kwa Magufuli anashambuliwa, kwa nini?
Unaweza ukaleta hata Post moja humu niliyoshawahi kumsifia JPM ?

Mimi sio cheerleader kama mtu anafanya mazuri ni kazi yake ndio aliyochaguliwa kufanya kuanza kwangu kumpigia makofi kwangu naona ni kupoteza rasilimali muda..., kwa yoyote anayekosea mimi huwa nipo critical sababu ninamlipa kwa kutumia kodi yangu hence nahitaji value for my money...

Sasa huyu (siongelei Assad huyu jamaa) kama aliweza kuficha huu uchafu kipindi cha JPM ni mangapi anaficha sasa ili aje kuyaongea awamu ijayo ?
 
Hiyo ni imani yako hakuna mtu mwenye haki ya kukufanya usiamni unacho kiamini.

Ila ukweli jiwe aliharibu sana maisha ya watanzania na kutumia hivyo fedha za umma.
 
Boss sio unafiki, maoni kama hayo miaka miwili iliyopita ingeweza kuwa career suicide, Nape na Ndugai wanajua vizuri
Nape kimbelembele chake choote kilikwisha hadi akaamua kupiga magoti
 
Afadhali uwanja upo hata mkisema mpaka mapovu yawatoke ni sawa tu maana Geita utabaki uwanja wao! Ile sehemu mmepora madini sasa hivi kumebaki maandaki maana hata mchanga umabebwa, no replacement!
Madini mliobebea yakiisha siku moja tutapata watalii watakaokuja kutembelea mashimo waliochimba Geita!
 
Vipi kuhusu Chato kuwa mkoa bado mnaendelea kuota?
 
Mzee unajua huyu CAG hii ni ripoti yake ya pili, alitoa ya kwanza baada ya jiwe kufa
 
Sio sgr tuu tukianza kuongelea miradi tanzania hii ni mingi ikiwemo chato. Kukosa mlengo kama taifa na dira kuu ni chanzo cha yote aya.

Nilitaka sahau mzizi wa yote aya ni CCM. Pamoja na kuhusisha vyeo vya kiutendaji pamoja na siasa
Ulitaka miradi ianze lini?
Kama si maamuzi magumu Kuhamia dodoma ingekuwa ndoto, SGR n.k hapa kukaa na kulalamika ujinga haisaidii, tafuteni hela mmalize SGR NA bwawa la umeme!
 
Usizungumze kwa mahaba bila weledi.

Chato imejengwa airport, Musoma ni airstrip. Economic activities zilizopo Mtwara utalinganisha na za Chato? Ujue Mtwara kuna visima vya gas, kuna Bandari, ni makao makuu ya mkoa, wakati Chato ni kijiji chenye hadhi ya Wilaya, inayozidiwa kwa mbali na business settlements kama Makambako.

Chato wangeweza kujengewa airstrip ndogo, ingetosha sana kwa matumizi ya kawaida. Kuweka uwanja wa ndege kama ule Chato ni sawa na kuchukua semi trailer kwaajili ya kwenda kubeba gunia mbili za dengu.
 
Kipindi like kipi? Ameteuliwa CAG 2019, kabla ya kutoa ripoti yake ya kwanza jiwe akawa keshakufa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…