Uchaguzi 2020 Canada wataka uchunguzi ufanyike dhidi ya waliokiuka haki za binadamu katika Uchaguzi Mkuu 2020

Uchaguzi 2020 Canada wataka uchunguzi ufanyike dhidi ya waliokiuka haki za binadamu katika Uchaguzi Mkuu 2020

Aisee, umemaliza hoja yako ?
===
Tuseme mara ngapi kuwa Tanzania tunatakiwa kufanya maamuzi yetu sisi wenyewe, yaani TUJITEGEMEE? Huo ndiyo uhuru, Mkuu. Kwa sasa tumeanza mdogomdogo kujitegemea kwa kupunguza bajeti ya uchaguzi kuwategemea wafadhili. Upo?

Sasa unapoleta habari za EU, binafsi nakushangaa haswa!!
Shida tukijisimamia wenyewe Kuna genge linapoka haki za wengine.Usawa unapotea ndio maana mtu anaona Mara Mia waje mabeberu watusimamie kuliko tukijisimamia wenyewe.Kwa mfano Kampeni za mwaka huu,jinsi TBC walivyokuwa wanafanya Kuna mtu ataziamini Taasisi za ndani? TBC mwanzo mwisho imemhubiri Magufuli pekee yake
 
....TBC mwanzo mwisho ....
Vyama vya upinzani vilionyesha 'bad impression' mara tu baada ya kuanza kampeni dhidi ya vyombo vya habari. Mfano pale Mbagala, Chadema wakiongozana na uongozi mzima wa Chama, wadhalilisha waandishi habari na watangazaji wa TBC.

Mara kadhaa, Ndugu Antipasu amesikika akivishambulia vyombo vya habari vya hapa nchini! Huku badala ya kunadi sera na ilani ya chama chake, Ndugu antipasu alijikita kutoa lugha za kuudhi dhini viongozi wa serikali na wagombea wenzake kwenye uchaguzi. Pia ametoa kauli nyingi za kuzusha kiasi cha vyombo vya habari kukosa cha kuwalisha wananchi kutoka kwa Antipasu.

Katika mazingira haya unaanzaje kulaumu vyombo vya habari hapa nchini ikiwemo TBC?
 
Mgejitenga na kauli hizi za hao jamaa! Ingewasaidia sana Kisiasa kiasi cha baadhi ya watanzania kurejesha imani yao kwenu. Lakini kadri mnavyozidi kujihusisha na matamko ya jamaa hawa ndiyo mnazidi kuwachefua watanzania!
Watanzania gani?
Sema wanufaika wa mfumo Magu
 
Nchi haina the elders?

Hadi nchi zingine ziseme?
Mkuu elders wenyewe hukuona wanajengewa nyumba za kuishi na serekali, na mwingine mwanawe kapewa ulaji zanzibar kwa hizi kura feki. Mkuu usitegemee lolote toka kwao.
 
Vyama vya upinzani vilionyesha 'bad impression' mara tu baada ya kuanza kampeni dhidi ya vyombo vya habari. Mfano pale Mbagala, Chadema wakiongozana na uongozi mzima wa Chama, wadhalilisha waandishi habari na watangazaji wa TBC.

Mara kadhaa, Ndugu Antipasu amesikika akivishambulia vyombo vya habari vya hapa nchini! Huku badala ya kunadi sera na ilani ya chama chake, Ndugu antipasu alijikita kutoa lugha za kuudhi dhini viongozi wa serikali na wagombea wenzake kwenye uchaguzi. Pia ametoa kauli nyingi za kuzusha kiasi cha vyombo vya habari kukosa cha kuwalisha wananchi kutoka kwa Antipasu.

Katika mazingira haya unaanzaje kulaumu vyombo vya habari hapa nchini ikiwemo TBC?
Vyama vya Upinzani Ni CHADEMA pekee yake? Kuna ACT Kuna CUF Kuna CHAUMA Kuna vyama kibao.Hata hao CDM mgogoro wao waliumaliza.Sasa sijui Kwanini TBC walibaki na Mgombea wao mmoja bila kuwaona wengine
 
Back
Top Bottom