Captain ya Yanga Dickson Job akimtambia Captain wa Simba Shomari Kapombe kabla ya kuanza mchezo

Captain ya Yanga Dickson Job akimtambia Captain wa Simba Shomari Kapombe kabla ya kuanza mchezo

DELETED ACCOUNT

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
9,805
Reaction score
15,476
Ukiwa unajiamini bwana, raha sana. Unajua kabisa matokeo yatakayokuwa, unaweza kutamba utakavyo.

Kabla mechi haijaanza, wakati macaptain wa Simba na Yanga, Shomari Kapombe na Dickson Job wakiwa na waamuzi kuchagua upande wa kuanza, Job alimwambia mwamuzi Arajiga na Kapombe kuwa hakuna haja ya kurusha shilingi, Kapombe achague mwenyewe anataka kuanzia upande upi. Kapombe akabaki kumshangaa na waamuzi wakaangua kicheko.

Yanga kumfunga Simba sasa ni sawa na CCM kushinda uchaguzi. Kibaya zaidi, DNA ya mashabiki wa Yanga ni kama ya watu wa CCM, kwao haijalishi ushindi umepatikanaje. Wanaamini mtizamo wa wamakonde wanaosema "the end justify the means".

Wanasimba poleni sana, mtaendelea kuumia saaana aiseee.
 
Wengine wana laumu refa, wengine kocha, wengine wachezaji, wengine Mangungu, wengine CCM wengine wasaliti, siku mkija kumpata mchawi itakua too late
Kwa mpira ni jambo la kawaida kabisa kupitia kwenye hali zote , Liverpool alisubiri miaka 30 kunusa kombe la epl , na kulaumu kwa mshabiki ni jambo la kawaida pia
 
Wachague sehemu moja ya kupeleka lawama zao
Usiwapangie hata yanga walilalamika mpaka wakajipachika jina la utopolo, binafsi naona simba ipo vizuri sana , msimu uliopita walicheza fainali ya africa na kumaliza nafasi ya pili tena kwa game ya mwisho , na uchovu mwingi wa mechi mfululizo , kwa highlight ya game ya yanga pia walicheza vizuri mno ni vile tu mpira lazima uwe na matokeo.
 
Usiwapangia hata yanga walilalamika mpaka wakajipachika jina la utopolo, binafsi naona simba ipo vizuri sana , msimu uliopita walicheza fainali ya africa na kumaliza nafasi ya pili tena kwa game ya mwisho , na uchovu mwingi wa mechi mfululizo , kwa highlight ya game ya yanga pia walicheza vizuri mno ni vile tu mpira lazima uwe na matokeo.
Msimu uliopita bila mbeleko za waamuzi wangekua nafasi ya nne
 
Watu waheshimu football sio wakishinda wao ni bora akishinda mwingine GSM mara CCM jana wamepata clear chances tano wanakosa lawama anapewa refa
Huwezi kuwapangia watu namna ya kuelezea hisia zao ,haya yallikua yanalalamikiwa hata ulaya ndio maana unaona ni kosa mpira kuwa na siasa , ndio maana unaona VAR , ndio maana unaona ni marufuku udhamin wa timu nyingi kwenye ligi moja
 
Udhamini una haribu nini? Azam ambae pia ni mdhaimi wa ligi na FA cup anapata advantage gani kwenye matokeo? Simba anafungwa kila siku nae kadhaminiwa na GSM?
 
Huwezi kuwapangia watu namna ya kuelezea hisia zao ,haya yallikua yanalalamikiwa hata ulaya ndio maana unaona ni kosa mpira kuwa na siasa , ndio maana unaona VAR , ndio maana unaona ni marufuku udhamin wa timu nyingi kwenye ligi moja

Mo kaisha dhamini Coastal union msimu huu
 
FIFA hawajakataa udhamini wamekataa umiliki ndio maana Fly Emirates imedhamini timu kibao tu Europe na zinacheza champions League
GSM alifuata nini kwenye yanga day ,unafahamu pia zipo sheria za udhamini na mipaka yao kama itatokea atadhamini klabu zaidi ya moja zenye migongano ya kimaslahi ndani ya ligi?

Kibongo bongo kanuni nyingi sana zina vunjwa klabu zote tu
 
Back
Top Bottom