Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Mambo mapya yameibuka kwenye mitandao ya kijamii baada ya aliyekuwa mwanahabari wa burudani, Carry Mastory, kuzungumzia sakata linalomuhusu mwanamitindo Hamisa Mobetto na kuvujisha sauti (voice note) inayohusu utambulisho wa baba mzazi wa mtoto wake, Dylan .
Katika maelezo hayo, Hamisa Mobetto amesisitiza kwa kukiri kuwa msanii Diamond Platnumz ndiye baba halisi wa mtoto huyo, akieleza kuwa yeye kama mama ndiye mwenye uelewa na ukweli kamili wa nani baba mzazi wa mwanaye .
Kupitia sauti hiyo, Hamisa pia amefunguka kuhusu changamoto na siri nyingi alizopitia wakati yupo kwenye mahusiano na Diamond Platnumz pamoja na mama yake mzazi, Mama Dangote.
Ameeleza kuwa hatua ya familia hiyo kumkana na kutomweka wazi mtoto huyo kwenye jamii inatokana na tofauti zao za nyuma , huku akidai kuwa miongoni mwa sababu za msingi za kumpiga vita ni yeye kukataa kujiunga katika makundi au mambo ambayo hakuwa radhi nayo .
Mwisho, Hamisa ametoa wito na ushauri kwa jamii kuweka mbele kumtanguliza Mungu katika kila jambo badala ya kuendekeza tamaa za kifedha, kwani ni vigumu kujua vyanzo halisi vya utajiri wa baadhi ya watu