Uchaguzi 2020 CASE STUDY - Jimbo la Hai - Walitumia teknolojia gani kupata matokeo sahihi ya kila kituo ndani ya saa 8?

Uliposema tu kwamba, Jimbo la Hai ndilo Lili kuwa "the most wanted person" nikajua hauna kitu kwenye ubongo wako.

Sijaona hoja..

Hata hivyo, asante kwa kushuriki kutoa maoni yako kwa style hii..
 
Vp kihusu ule uchaguzi wa Serikali za Mitaa?? Mlichukua hatua yeyote au mlishangilia??
Mlifanya uchafu kule mkaachwa, bahati mbaya mmekuja kurudia tena uchafu wenu huku, hamvumiliki.
 
Ni kweli mkuu, jamaa hawajui walitakalo na ukitoa ushauri unaonekana wewe ni ccm hata kama huna chama.

Ajabu ni kuwa, walitangaza maandamano kuelekea hadi ofisi za tume ili watoe malalamiko yao. Lakini ni tume hiyohiyo hawaitaki na kusema sio huru. Sasa, watakupokeaje wakati uwatambui?

Yaani nikutie ngumi, uumie then unaandamana kuja kwangu kunistakia kuwa nimekupiga ngumi. Wana akili kweli hawa kama sio kutaka kuleta vurugu tu.

Kama huiamini tume, yupo aliyeteuwa tume kwa sheria, mfuate huyo mwambie uliyemuweka hanipi haki yangu, ni mwonevu. Il tume ajitetee.
 
Porojo tupu; jimbo la Hai siyo kubwa kiasi cha kushindwa kumaliza kujumlisha kura hizo ndani ya masaa kumi. Walimaliza kuhesabu na kujumlisha kura zao alfajiri; na siyo huko tu walikomaliza kuhesabu alfajiri, majimbo mengi hali ilikuwa hivyo...

Labda huna kumbukumbu..

Matokeo ya jimbo hili yametangazwa kati ya saa 8 na 9 usiku..!

Wizi ungekuwa umejificha kidogo kama wangetangaza ungalau saa 3 au 4 asubuhi kesho yake tarehe 29/10/2020..

Mchakato wa uchaguzi hauko guided na ukubwa ama udogo wa jimbo bali ni teknolojia ya ukusanyaji matokeo..

Kumbuka, sisi kila kitu ni kutumia mikono na kichwa. Kila hatua kazi inafanyika manually..

Narudia tena kusema, haiwezekani kazi ya kujumuisha matokeo kuanzia vituoni, katani na jimboni na kushughulikia migogoro ya kura zote ifanyike ndani ya masaa kati ya 6 hadi 8 kwa jimbo zima baada ya vituo vya kupigia kura kuwa vimefungwa..!!

Nasema tena HAIWEZEKANI bila kujali ukubwa ama udogo wa jimbo unless muamue kufanya udanganyifu na ofcoz ndicho kilichofanyika Hai na maeneo mengine na Tanzania nzima...!!!
 
Ulivyoanza kwa thread kuiandika uthibitisho ni kama kweli uthibitisho wenye valid ushahidi kumbe ni imagination tu.
 
Wanhechelewa kutoa matokeo pia ungekuja kusema walikuwa waachakachua kura kwanza...Binadam hawana maana
 
Imeisha hiyooooo. Tuliposema kuwa tunafuta upinzani wa kijinga mwaka huu wa 2020 mlidhani tunatania? Pumbavu kabisa nyie.
 

Unajua sifa ya uchaguzi halali na wa kweli?

Kinacholalamikiwa ni nchi kuongozwa na watu walioingia madarakani kwa HILA na UDANGANYIFU na WIZI WA KURA kwa kutumia uhalali wa hiki kinachoitwa uchaguzi wakati huu ni ujambazi dhidi ya demokrasia..!!
 
We ni kunguru kama kunguru wengine,mnakuja kuleta ushahid baada ya kuchazwa na dogo kabsa yule,mbona hukuyaleta hayo unayoyasema hapa au ulikua unasubiri posho kwanza ndo uje ujitapishe huku??ni hiv mmepigwa nje ndan mpk hamwamin kilichowakuta
 
Imeisha hiyoooooo. Tuliposema kuwa tunafuta upinzani wa kijinga mwaka huu wa 2020 mlidhani tunatania? Pumbavu kabisa nyie.
Ndivyo akili yako finyu inavyokutuma kuamini hivyo siyo?

You are absolutely wrong..

Huwezi kumpoteza mtu fulani kwa kumnyang'any'a nguo zake za kuvaa na kutoka hapo ukishangilia kama juha kuwa "nimemuua huyo, nimemuua huyo" badala ummalize kabisa kwa risasi za SMG ama AK47...!

Mtu huyo ni wewe...
 
Waangalizi wa Jumuiya fulani huko wao wasema huru bin haki! Ila Ndege wafanano huruka kwa pamoja!
 
Kuna mahakama au shina la CCM?
 
Achana naye anaishi kwa shemeji yake, maumivu anayapata dada ake
 
Nikishaelwa aina ya watu kama nyinyi huwa sipendi kujipotezea muda.
 
Nchi ipi? achana naye, hiyo nchi Jenga wewe
unahisi taarifa hii itabadilisha maamuzi na kwamba mbowe wako ashinde ??? Nini faida ya uzi wako wakati huu?? Au unawafariji wenzako mkuu???

AchAna na mambo ya uchaguz yamepit.. chapa kazi tuijenge nchi
 
Ulivyoanza kwa thread kuiandika uthibitisho ni kama kweli uthibitisho wenye valid ushahidi kumbe ni imagination tu.

Ndugu, mimi sijaleta mashtaka yanayohitaji ushahidi. Hoja yangu iko katika sura ya "personal observation based on my personal opinions"..

Nimekuletea "study" ambayo ina hoja zenye maelezo ya kutosha kabisa kwa mtazamo wangu..

Mada yangu haina kichwa cha habari kisemacho "HAYA NDIYO MATOKEO HALISI YA KURA JIMBO LA HAI"...

Ingekuwa hivi halafu nisilete " figures" zinazothibitisha matokeo hayo yaliyo kinyume na yanayolalamikiwa, basi hoja yako hii ingekuwa na mantiki..

Nilichokifanya mimi ni kukueleza kwa hoja ni kwanini uchaguzi wa 28/10/2020, jimbo HAI - Kilimanjaro likiwa kama reference yangu umekosa credibility ya kuitwa uchaguzi kwa sbb matokeo halisi yaliyotangazwa si yale yaliyotokana na uchaguzi wenyewe bali matokeo ya mfukoni mwa mtu tu...!!

Ushahidi ni mchakato mzima wa uchaguzi kugubikwa na kasoro nyingi na zisizorekebishika ili kuyafanya matokeo haya kuwa halali...

Kwa ishu hapa wala siyo matokeo. Kwa sababu matokeo yenyewe yametokana na mchakato haramu. Kwa sbb hii matokeo yote yanakosa uhalali wa kisheria na kimaadili...!!
 
Watu walalamikaji ndiyo hivyo; matokeo yakichelewa watalalamika kuwa wasimamizi wanachakachua kura, yakitoka mapema pia watalamaiko hivyo hivyo. Unajuaje kuwa labda Jimbo la Hai lilikuwa na wafanya kazi wengi na wakamaliza mapema.

Muda gani yametangazwa siyo hoja kabisa. Jimbo la Hai halikulalamikiwa kuhusu mawakala, vituo vyote vilikuwa na mawakala wa CHADEMA pia lakaini hawajatoa malalamiko yoyote. Mbowe Mwenyewe akikaa kimya baada ya kushindwa wala hakutoa sababu yoyote ya kuchakachuliwa kura. Waliolalamika ni Mdee na Zitto tu.
 
Unaniuliza mimi kwa kutumia "phrase ya " umejuaje kwani...."

Kama ni hivyo, thibitisha wewe sasa kwa kutuambia kuwa HAI waliwahi kutoa matokeo kwa sababu walikuwa na "special and unique" wasimamizi wa vituo..

Lakini ninachoweza kukuambia na kukuhakikishia ni hiki;

Kwamba, mfumo wetu wa uchaguzi kuanzia uteuzi wa wagombea, kampeni, kupiga na kuhesabu kura, kutoa na kutangaza matokeo unafanana kila jimbo na nchi nzima..

Mfumo waliotumia jimbo la Kilosa, Mororogoro au Tandahimba nk ni uleule uliotumika HAI au Arusha mjini..

Na nikuambie jambo jingine moja;

Kwamba, bahati njema mimi nimeshiriki chaguzi karibu zote za vyama vingi; 1995, 2000, 2005, 2010, 2015 na huu wa juzi 2020..

Hakuna jimbo lililowahi kukamilisha mchakato uchaguzi (kupiga kura, kuhesabu kura, kushughulikia migogoro, kukusanya masanduku na kufanya majumuisho katani na jimboni) ndani ya masaa 6 hadi 8 baada ya mtu wa mwisho kwa kila kituo kupiga kura na kisha kumtangaza mshindi...!!

Nimeanza kuona HAI mwaka huu na Arusha na Kawe na Mbeya na Iringa na maeneo mengine..!!

Kuanzia mwaka 1995 hadi 2015, matokeo katika majimbo ya wabunge huanza kutoka kesho yake ingalau kuanzia saa 6mchana na kuendelea na kuna majimbo mengine huenda hadi siku 4 ndipo mshindi anatangazwa...!!

Kumbuka kuwa, mimi sisemi kuwa kuchelewa sana kutangaza matokeo ni vyema. Pia sisemi kuwa, kuwahi sana kutoa matokeo ya kura ni jambo baya..

Hapana. Hoja yangu ni kuwa, at least there is a "standard duration of time"..

Ukiwahi sana "under the standard duration of time", kama msimamizi wa uchaguzi, lazima kutakuwa na maswali utakayopaswa kujibu..

Vivyo hivyo ukichelewa sana kutangaza na wewe kama msimamizi umeshapokea matokeo ya vituo vyote na kufanya compilation, pia utakuwa na maswali ya kujibu..

Kila kitu kikizidi, kina madhara...
 
Tume hata kama mbovu ndiyo inayohusika na uchaguzi, ulitaka waende bungeni kwa Ndugai?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…