Unaniuliza mimi kwa kutumia "phrase ya " umejuaje kwani...."
Kama ni hivyo, thibitisha wewe sasa kwa kutuambia kuwa HAI waliwahi kutoa matokeo kwa sababu walikuwa na "special and unique" wasimamizi wa vituo..
Lakini ninachoweza kukuambia na kukuhakikishia ni hiki;
Kwamba, mfumo wetu wa uchaguzi kuanzia uteuzi wa wagombea, kampeni, kupiga na kuhesabu kura, kutoa na kutangaza matokeo unafanana kila jimbo na nchi nzima..
Mfumo waliotumia jimbo la Kilosa, Mororogoro au Tandahimba nk ni uleule uliotumika HAI au Arusha mjini..
Na nikuambie jambo jingine moja;
Kwamba, bahati njema mimi nimeshiriki chaguzi karibu zote za vyama vingi; 1995, 2000, 2005, 2010, 2015 na huu wa juzi 2020..
Hakuna jimbo lililowahi kukamilisha mchakato uchaguzi (kupiga kura, kuhesabu kura, kushughulikia migogoro, kukusanya masanduku na kufanya majumuisho katani na jimboni) ndani ya masaa 6 hadi 8 baada ya mtu wa mwisho kwa kila kituo kupiga kura na kisha kumtangaza mshindi...!!
Nimeanza kuona HAI mwaka huu na Arusha na Kawe na Mbeya na Iringa na maeneo mengine..!!
Kuanzia mwaka 1995 hadi 2015, matokeo katika majimbo ya wabunge huanza kutoka kesho yake ingalau kuanzia saa 6mchana na kuendelea na kuna majimbo mengine huenda hadi siku 4 ndipo mshindi anatangazwa...!!
Kumbuka kuwa, mimi sisemi kuwa kuchelewa sana kutangaza matokeo ni vyema. Pia sisemi kuwa, kuwahi sana kutoa matokeo ya kura ni jambo baya..
Hapana. Hoja yangu ni kuwa, at least there is a "standard duration of time"..
Ukiwahi sana "under the standard duration of time", kama msimamizi wa uchaguzi, lazima kutakuwa na maswali utakayopaswa kujibu..
Vivyo hivyo ukichelewa sana kutangaza na wewe kama msimamizi umeshapokea matokeo ya vituo vyote na kufanya compilation, pia utakuwa na maswali ya kujibu..
Kila kitu kikizidi, kina madhara...