Hapa ndo bavicha hua siwaelewi.. Pamoja na kuamini hamtatenewa haki kwenye chaguzi mbalimbali bado mnashiriki. Yakitokea mliyohisi mngefanyiwa hamtaki kwenda mahakamani kwa kuwa mnaamini nako hamtatendewa haki. Viongozi wenu wakiwambia nendeni barabarani tukawaonyeshe tunaohisi hawajatutendea haki kwamba hatujaridhika, huko pia hamtokei...
Umeandika vizuri.
Kama umenisoma vema hapo juu nimetumia neno laiti, nikiwa na maana kwamba siwazuii viongozi wanaoona wameonewa majimboni waende mahakamani, lakini pia, ukweli lazima usemwe, kea utawala wa awamu hii sidhani kama kuna hakimu yeyote atakayethubutu kuwapa haki wapinzani ikiwa bosi wao alishatoa maelekezo kwa wakurugenzi mapema Chadema inatakiwa ife ifikapo 2020 na kilichotokea kwny uchaguzi ndio majibu yake.
Kuhusu kushiriki uchaguzi, utakuwa vipi na maelezo ya kujitosheleza au hata kupeleka ushahidi wa irregularities mahakamani kama hata huo uchaguzi hushiriki? locus standi yako itatoka wapi?! ni lazima washiriki uchaguzi, then patakapotokea baya km tulivyoona this time, ndio Chadema na wengine waende mahakamani kupinga matokeo, hivyo suala la kushiriki nalo halina mjadala.
Suala la kuandamana, hili nalo japo lipo kikatiba lakini utaweza vipi kuwalaumu wasioandamana kama unasikia kamanda wa jeshi la polisi akisema hadharani watakaoandamana watavunjwa miguu km vile kuandamana ni kosa kisheria? hapa badala ya kuwalaumu wasioandamana, ningekuona mjanja zaidi uwalaumu wale waliopewa mamlaka na sheria ya kuwalinda waandamanaji, lakini badala yake wanawatisha waandamanaji, kumbuka wao wana marungu waandamanaji hawana kitu.
Hivyo basi, sioni utoto wowote kwny hizo sababu nilizokuwekea hapo juu, wajibu wako km raia unaejielewa nchi hii unatakiwa kuzikumbusha mamlaka zitekeleze wajibu wao bila kuingiliwa na yeyote, au kumpendelea yeyote, hapo ndipo taifa letu litasonga mbele, lakini kuwalaumu waliofungwa kamba mikono iko nyuma eti kwanini hawachukui hatua ni kuwaonea.