Uchaguzi 2020 CASE STUDY - Jimbo la Hai - Walitumia teknolojia gani kupata matokeo sahihi ya kila kituo ndani ya saa 8?

CCM walikuwa na matokeo yao ya mfukoni hata kabla ya kuanza kupiga kura.

Zoezi la kupiga kura ilikuwa ni kuhalalisha uharamia ndani ya Sanduku la kura.

Lakini itawasaidia nini CCM ambao wapo madarakani zaidi ya miaka 60 na bado umaskini umetamalaki kila kona ya nchii hii.

Chama kikongwe eti kipaumbele chake bado ni kupika matokeo ionekane kinakubalika .

Hapo ndiyo kinazidi kujichimbia kaburi.
 
Tume hata kama mbovu ndiyo inayohusika na uchaguzi, ulitaka waende bungeni kwa Ndugai?!
Nilitaka waende kwa aliyeteua tume, maana yeye ndiye mwenye mamlaka ya kuivunja. Tume haiwezi kujivunja yenyewe.
 
Nikishaelwa aina ya watu kama nyinyi huwa sipendi kujipotezea muda.
Hukutumwa kusoma wala ku comment, ni ujuha wako ndio uliokuleta kwangu.
short, jiheshimu nikuheshimu, sikumtukana wala kumkejeri yoyote yule. Najua na nina thamini maoni ya wote yenye staha.

Hatuwezi wote kufanana. Kuvumiliana ni sehemu ya maisha. Mimi sio mnafiki wa kusifia ujinga hata kama nina uwezo wa kuhoji. Sio muoga, nina tumia kichwa na uwezo niliopewa kutafakari na kuhoji pale panapo hitajika.
 
Unajua sifa ya uchaguzi halali na wa kweli?

Kinacholalamikiwa ni nchi kuongozwa na watu walioingia madarakani kwa HILA na UDANGANYIFU na WIZI WA KURA kwa kutumia uhalali wa hiki kinachoitwa uchaguzi wakati huu ni ujambazi dhidi ya demokrasia..!!
Sawa mkuu.
sasa toa muongozo nini kifanyike? kuanzisha vurugu? kukaa kimya? kuja kulalamika humu jf? Tunahitaji suluhisho lililo sahihi ili kuondoa hizo dhurma na kutenda haki.

Tuamini story zako tu bila kusikiliza wengine? Lazima tu balance story na sehemu pekee ya kutoa haki ni mahakama. Ndio maana nakushauri na kuwashauri wote wanaoweza kusaidia haki ipatikane hata kama wenye mamlaka wapinge, hao watu waende kwa viongozi wetu walionewa ili waidai.
 
Mahakama ipi unazungumzia? Kama ni hizi zilizo chini ya Prof. Juma afadhali wafanye mambo mengine.Upumbavu umetamalaki kote kote: si polisi,tume ya uchaguzi,wakurugenzi,dpp wala mahakamani.Msajili wa vyama ndiyo usiseme.EXTREMELY SHIT HOLE CHARACTERS!
 
Ulitaka aweke hayo yote hapa JF?
 

Mkuu napata taabu sana kuweka mchango wangu hapa, nimekuwa Jimboni Hai siku sita kabla, nilikuwa na reliable contacts 163 wakikusanya data kwenye vijiji vyote na mimi nilikuwa Mwowe Msikitini baadae nikaenda Lyamungo Sinde.

Mkuu kapigwa na hata wakirudia mara tano. Tatizo ni wananchi walikuwa na hamu ya kubadilisha mtu. Maneno yeyote mengine ni uwongo. ASANTE SANA.
 
Mbowe kadhibitiwa na dogo janja.

Safi sana Sabaya, wewe ni shujaa.
Sabaya, mkuu wa wilaya, mwenyekiti wa ulinzi na usalama wilayani, ana mamlaka ya kuamuru Polisi wafanye atakavyo anaweza kumtia ndani mtu yeyote kwa masaa 48, na mengine mengi. Huyu anakuwaje SHUJAA kwa kumtesa mtu ambaye hana jeshi, hana chochote?

Shujaa ni yule anayepambana na jitu lenye mabavu na kulishinda. Kama dogo Daudi alivyomshinda Goliati.

Kama kwa wizi huu ccm wanakuwa mashujaa, basi hawajitambui na ni wa kudharauliwa kabisa
 
Sikubishii maoni yako ila sikubaliani na theory yako ambayo ni conspiratorial tu. Umma wa watanzania tulishaamabiwa hata na viongozi wa upinzania kuwa mwaka huu tume iliandaa uchaguzi vizuri sana na upigaji wa kura ulikuwa smooth sana.

Kwa hiyo ule ucheklleweshaji wa zamani mwaka huu haukuwapo kwa vile tume ilikuwa imeandaa vitu vingi vya kura na vifaa vilikuwapo vya kutosha.. Ni ajabu kuwa baada ya kushindwa wote viongozi wa upinzani wanakuja na sababu tofauti kabisa na assessment yao ya kwanza.
 
Hongera mkuu, wewe ni hodari wa matusi. Mimi si fani yangu hii, kwa hio kwa hili nakupa ushindi kama mlivopata ushindi wa kupora haki za watu hongereni mabingwa wa wizi!
 
Sasa Mbowe si alitaka maridhiano! Haya ndio maridhiano yaani.
 
Umejitahidi sana kuelezea msimamo wako ambao ni haki yako. Lakini umemwacha msomaji bila majibu, baadhi ya maswali kadhaa ambayo msomaji anaweza kuuliza au wewe unaweza kuyajibu:
1. Je, matokeo yalitangazwa saa ngapi na siku gani? (ie baada ya masaa mangapi tangu kufungwa kwa uchaguzi? Je, ni jimbo pekee ambalo lilitangaza matokeo haraka kuliko jimbo lolote lile lenye uwiano wa idadi ya wapiga kura?

2. Je, utaratibu wa kuhesabu na kutangazwa amepewa nani?
3. Je, kwenye kuhesabu kura nani huwa wanashiriki, i.e. Wakala wa wagombea wanakuwepo wa pande zote mbili? Je, nani wengine wanahusika?

4. Je, nani wana dhamana ya kubeba masanduku ya kura? Je, kuna nani zaidi anayehusika kuona kwamba masanduku hayo hayabadilishwi au kwa namna yoyote ile kuhujumiwa?
5. Je, unao ushahidi usio na shaka kwamba JPM alihusika na hizo njama? Tupe ushahidi wako vinginevyo ni majungu tu.
 
Yani ni uongo na dhuruma za wazi,kuna majimbo gari la mwisho kuwasili Wilayani naambiwa ilifika SAA 5:30 alfajiri
 
Vp kihusu ule uchaguzi wa Serikali za Mitaa?? Mlichukua hatua yeyote au mlishangilia??
Aaah mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu...
Sijaona wala kusikia hatua zozote zilizochukuliwa baada ya kususia uchaguzi wa serikali za mitaa
Me mwenyewe ni miongoni mwa wale tuliopinga Maan niliona kama viongozi wameweka maslai ya chama mbele bila lengo lolote...
Ila kwa uchaguzi huu hatua zingechukuliwa tena za haraka sanaa maan wahusika ndo viongozi wenyewe
 
Halafu mkiona kuna shida mahali mngechukua hatua gani ?
Hatua nyingi Sanaa Mkuu.....
-Kwenda jumuiyaa za kimataifa..
-Maandamano ya Aman.. tena yangefanikiwa maan watu walikuwa na morale kubwa sanaa
-kufungua pingamizi mahakaman n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…