View attachment 2816118
Cassie amefungua kesi ya dola milioni 30 dhidi ya Diddy akimtuhumu kwa ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia. Mwanadada huyo anasema muda mfupi baada ya kukutana na Diddy mwaka 2005, akiwa na umri wa miaka 19, alianza tabia ya kumdhibiti na kumnyanyasa ikiwa ni pamoja na kumlazimisha kutumia dawa za kulevya, kumpiga na kumlazimisha kulala na malaya wa kiume huku akirekodi filamu hizo.
Kesi hiyo imeibua hisia za watu wengi mtandaoni wakidai kuwa inaweza kuibua watu wengi waliofanyiwa vitendo kama hivyo na Diddy na kudai kuwa inaweza kuwa ndio mwisho wa Diddy.