mama D
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 20,458
- 36,481
Hakuna mtu wa kitu kisichobadilika duniani Mabadiliko ndio maendeleoTatizo la watu kama wewe ni kwamba hamjui historia ya kweli ya upepo wa mageuzi uliotuletea mfumo wa vyama vingi. Mmedandia tu gari kama Mrema alivyodandia mageuzi baada ya kuachwa kwenye mataa na CCM wakati wa uchaguzi mkuu wa kwanza mwaka 1995.
Mbowe alikuwa mwanamageuxi toka mwanzo kabisa na mwana Chadema toka kuasisiwa kwake hivyo tafadhali usimfananishe Mbowe na vitu vya ajabu. Mrema pamoja na Dr. Slaa walidandia upinzani wakisaka uteuzi kwa Mrema kugombea Urais kupitia NCCR na Dr. Slaa kugombea Ubunge kupitia Chadema.
Hao wawili hakuna aliyeonja machungu katika mapambano ya kudai mageuzi. Na kama kawaida kwa mamluki kama hawa hivi sasa moja ni CCM-B na mwenzake karudi CCM-A . mama D, jaribu kufanya utafiti na kama hujui kitu uliza. Mh Mbowe ni mwana mageuzi wa kweli na alihangaika juani ili wadandiaji kama Mrema na Dr. Slaa wale kivulini.
Muda utasema