Mbunge viti maalum Arusha Catherine Magige amvaa kwa matusi mbunge mwenzake.
Amemshambulia kwa matusi mbunge Mpina utadhani wapo vyama tofauti.
Hii ni dalili tosha kuwa CCM sasa hivi kuna moto unawaka chini kwa chini.
Hakuna amani tena.
Tuombe Mungu azidi kuukoleza na sisi wazalendo kazi yetu ni kuongezea Kuni tu.
View attachment 2877418
Kwanza kabisa, nianze kwa kusema, tunavyosema Wanyamwezi, "I don't have a dog in this fight". Huu si ugomvi ambao nina upande wowote maalum kwa maana ya Mpina au Magige.
Inawezekana Mpina ana makosa yake, personally naona hata Mpina akiwa na point, presentation yake ni ya kukurupuka zaidi, kwa hivyo siko hapa kumtetea Mpina.
Lakini pia, kuna kitu nakiona kinajirudiarudia CCM, hususan kwa baadhi - msisitizo ni kwenye baadhi, si wote - baadhi ya wanawake wa CCM.
Hivi, kwanini mtu anayemsema Rais, kama Rais, si kama mwanamke, anachukuliwa kwamba anamsema Rais kwa kuwa ni mwanamke?
Kuna inferiority complex miongoni mwa wanawake hawa wa CCM inayowafanya waone kuwa, Rais anapokosolewa tu, basi ni lazima anakosolewa kwa sababu ni mwanamke, na si kwa sababu ni rais?
Watanzania tunataka Rais anayeweza kukosolewa, hatutaki Rais aliyevishwa bullet proof ya kutoweza kukosoleka kwa sababu ni mwanamke.
Ikiwa hivyo tutasema wanawake hawafai kuongoza, kwa sababu wakipata uongozi tunakatazwa kuwakosoa, tukiwakosoa tunaambiwa kwa nini tunakosoa wanawake?
Hawa wanawake wanaweza kumuangalia Rais Samia kama Rais kamili, kama Rais, na si kama Rais Mwanamke au Mwanamke?
Mlio nyumbani labda mtanisaidia vizuri, sijamfuatilia Mpina muda, I don't put anything past him either. So labda mimi ndiye niko out of touch na kauli zake za karibuni.
Kuna kauli mahsusi ya kunyanyapaa mwanamke ambayo Mpina ameitoa imemfanya Magige aseme hivi?
Labda kuna kauli mahsusi ya kunyanyapaa wanawake kaisema Mpina sijaisikia mimi jamani?
Maana isije kuwa wanasiasa wanaamua kujificha kwenye chaka la uanamke, na kutaka kupata kinga Rais asisemwe na mtu, na akisemwa tu, wanakimbilia kulalamika kwamba Rais anasemwa kwa sababu ni mwanamke.
Kufanya hivyo kutakuwa ni kumvunjia heshima rais na kuwavunjia heshima wanawake.
Mbona marais wote wamepingwa? Mbona Nyerere kapingwa mpaka kafanyiwa njama za kupinduliwa mara mbili?
Nyerere alikuwa mwanamke?
Mbona Mwinyi kapingwa mpaka kachorwa na Punch?
Mwinyi ni mwanamke?
Mbona Mkapa kapingwa mpaka kasomewa risala za kupinga ubinafsishaji?
Kwani Mkapa alikuwa mwanamke?
Mbona Kikwete kapingwa mpaka kwenye nomination za CCM urais kapata mpinzani kutoka CCM John Shibuda, wakati Kikwete akiwa Rais? (Kitu ambacho CCM wengine wanataka kuzuia 2025)
Kwani Kikwete ni mwanamke?
Mbona Magufuli kapingwa sana mpaka kapiga marufuku mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani Tanzania?
Kwani Magufuli alikuwa mwanamke?
Kuna kauli gani Mpina kaitoa kunyanyapaa wanawake kwa Samia?
Vinginevyo, msimnyime Rais Samia haki yake ya kupingwa sawa na marais wote waliopita, kwa sababu yeye mwanamke tu.
Ukubwa gunia la chawa. Kalitaka mwenyewe. Nyerere alisema Ikulu si sehemu ya kukimbilia pale, kuna matatizo chungu mbovu.