Mizania
JF-Expert Member
- May 17, 2023
- 3,812
- 3,277
Mkuu;Kwanza kabisa, nianze kwa kusema, tunavyosema Wanyamwezi, "I don't have a dog in this fight". Huu si ugomvi ambao nina upande wowote maalum kwa maana ya Mpina au Magige.
Inawezekana Mpina ana makosa yake, personally naona hata Mpina akiwa na point, presentation yake ni ya kukurupuka zaidi, kwa hivyo siko hapa kumtetea Mpina.
Lakini pia, kuna kitu nakiona kinajirudiarudia CCM, hususan kwa baadhi - msisitizo ni kwenye baadhi, si wote - baadhi ya wanawake wa CCM.
Hivi, kwanini mtu anayemsema Rais, kama Rais, si kama mwanamke, anachukuliwa kwamba anamsema Rais kwa kuwa ni mwanamke?
Kuna inferiority complex miongoni mwa wanawake hawa wa CCM inayowafanya waone kuwa, Rais anapokosolewa tu, basi ni lazima anakosolewa kwa sababu ni mwanamke, na si kwa sababu ni rais?
Watanzania tunataka Rais anayeweza kukosolewa, hatutaki Rais aliyevishwa bullet proof ya kutoweza kukosoleka kwa sababu ni mwanamke.
Ikiwa hivyo tutasema wanawake hawafai kuongoza, kwa sababu wakipata uongozi tunakatazwa kuwakosoa, tukiwakosoa tunaambiwa kwa nini tunakosoa wanawake?
Hawa wanawake wanaweza kumuangalia Rais Samia kama Rais kamili, kama Rais, na si kama Rais Mwanamke au Mwanamke?
Mlio nyumbani labda mtanisaidia vizuri, sijamfuatilia Mpina muda, I don't put anything past him either. So labda mimi ndiye niko out of touch na kauli zake za karibuni.
Kuna kauli mahsusi ya kunyanyapaa mwanamke ambayo Mpina ameitoa imemfanya Magige aseme hivi?
Labda kuna kauli mahsusi ya kunyanyapaa wanawake kaisema Mpina sijaisikia mimi jamani?
Maana isije kuwa wanasiasa wanaamua kujificha kwenye chaka la uanamke, na kutaka kupata kinga Rais asisemwe na mtu, na akisemwa tu, wanakimbilia kulalamika kwamba Rais anasemwa kwa sababu ni mwanamke.
Kufanya hivyo kutakuwa ni kumvunjia heshima rais na kuwavunjia heshima wanawake.
Mbona marais wote wamepingwa? Mbona Nyerere kapingwa mpaka kafanyiwa njama za kupinduliwa mara mbili?
Nyerere alikuwa mwanamke?
Mbona Mwinyi kapingwa mpaka kachorwa na Punch?
Mwinyi ni mwanamke?
Mbona Mkapa kapingwa mpaka kasomewa risala za kupinga ubinafsishaji?
Kwani Mkapa alikuwa mwanamke?
Mbona Kikwete kapingwa mpaka kwenye nomination za CCM urais kapata mpinzani kutoka CCM John Shibuda, wakati Kikwete akiwa Rais? (Kitu ambacho CCM wengine wanataka kuzuia 2025)
Kwani Kikwete ni mwanamke?
Mbona Magufuli kapingwa sana mpaka kapiga marufuku mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani Tanzania?
Kwani Magufuli alikuwa mwanamke?
Kuna kauli gani Mpina kaitoa kunyanyapaa wanawake kwa Samia?
Vinginevyo, msimnyime Rais Samia haki yake ya kupingwa sawa na marais wote waliopita, kwa sababu yeye mwanamke tu.
Ukubwa gunia la chawa. Kalitaka mwenyewe. Nyerere alisema Ikulu si sehemu ya kukimbikia pale, kuna matatizo chungu mbovu.
Nakuunga mkono, upo sahihi. Luhaga Mpina hajawahi kumpinga au kumkosoa Rais Samia wala kumkosoa kwa sababu ya jinsia yake.
Mpina amekuwa akikosoa mwenendo wa serikali na watumishi wake katika matumizi na kusimamia fedha za umma!
CCM kwa asili haipendi ukosoaji! Kwao inauma, hasa ukosoaji ukiwa unatoka kwa mwenzao! Magige anawakilisha hisia za wengi ndani ya CCM.
Hii ni dalili ya kuanza kufikia mwisho wa kutumia akili na uvumilivu. Hatua inayofuata kwa Mpina ni Kolimba style! Mpina kawashiwa taa, akae chonjo!!!