Pre GE2025 Catherine Magige: Luhaga Mpina ni mtu wa ovyo ambaye haamini uongozi wa mwanamke

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

CCM bila vyombo vya dola, katiba mbovu, TumeCCM .

Ni weupe kama kile kichwa cha Makonda kilichopata division 0 kidato cha nne.
 
Wanasiasa buana, sasa si angempigia simu wamalizane wenyewe 😄
 
Wewe sio mwanaccm wewe ni chawa uliyejitoa faham kwa ajili ya tumbo;
 
Mpina si wakupigwa mkwara na boya kama huyu
 
Kwanza kabisa, nianze kwa kusema, tunavyosema Wanyamwezi, "I don't have a dog in this fight". Huu si ugomvi ambao nina upande wowote maalum kwa maana ya Mpina au Magige.

Inawezekana Mpina ana makosa yake, personally naona hata Mpina akiwa na point, presentation yake ni ya kukurupuka zaidi, kwa hivyo siko hapa kumtetea Mpina.

Lakini pia, kuna kitu nakiona kinajirudiarudia CCM, hususan kwa baadhi - msisitizo ni kwenye baadhi, si wote - baadhi ya wanawake wa CCM.

Hivi, kwanini mtu anayemsema Rais, kama Rais, si kama mwanamke, anachukuliwa kwamba anamsema Rais kwa kuwa ni mwanamke?

Kuna inferiority complex miongoni mwa wanawake hawa wa CCM inayowafanya waone kuwa, Rais anapokosolewa tu, basi ni lazima anakosolewa kwa sababu ni mwanamke, na si kwa sababu ni rais?

Watanzania tunataka Rais anayeweza kukosolewa, hatutaki Rais aliyevishwa bullet proof ya kutoweza kukosoleka kwa sababu ni mwanamke.

Ikiwa hivyo tutasema wanawake hawafai kuongoza, kwa sababu wakipata uongozi tunakatazwa kuwakosoa, tukiwakosoa tunaambiwa kwa nini tunakosoa wanawake?

Hawa wanawake wanaweza kumuangalia Rais Samia kama Rais kamili, kama Rais, na si kama Rais Mwanamke au Mwanamke?

Mlio nyumbani labda mtanisaidia vizuri, sijamfuatilia Mpina muda, I don't put anything past him either. So labda mimi ndiye niko out of touch na kauli zake za karibuni.

Kuna kauli mahsusi ya kunyanyapaa mwanamke ambayo Mpina ameitoa imemfanya Magige aseme hivi?

Labda kuna kauli mahsusi ya kunyanyapaa wanawake kaisema Mpina sijaisikia mimi jamani?

Maana isije kuwa wanasiasa wanaamua kujificha kwenye chaka la uanamke, na kutaka kupata kinga Rais asisemwe na mtu, na akisemwa tu, wanakimbilia kulalamika kwamba Rais anasemwa kwa sababu ni mwanamke.

Kufanya hivyo kutakuwa ni kumvunjia heshima rais na kuwavunjia heshima wanawake.

Mbona marais wote wamepingwa? Mbona Nyerere kapingwa mpaka kafanyiwa njama za kupinduliwa mara mbili?

Nyerere alikuwa mwanamke?

Mbona Mwinyi kapingwa mpaka kachorwa na Punch?

Mwinyi ni mwanamke?

Mbona Mkapa kapingwa mpaka kasomewa risala za kupinga ubinafsishaji?

Kwani Mkapa alikuwa mwanamke?

Mbona Kikwete kapingwa mpaka kwenye nomination za CCM urais kapata mpinzani kutoka CCM John Shibuda, wakati Kikwete akiwa Rais? (Kitu ambacho CCM wengine wanataka kuzuia 2025)

Kwani Kikwete ni mwanamke?

Mbona Magufuli kapingwa sana mpaka kapiga marufuku mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani Tanzania?

Kwani Magufuli alikuwa mwanamke?

Kuna kauli gani Mpina kaitoa kunyanyapaa wanawake kwa Samia?

Vinginevyo, msimnyime Rais Samia haki yake ya kupingwa sawa na marais wote waliopita, kwa sababu yeye mwanamke tu.

Ukubwa gunia la chawa. Kalitaka mwenyewe. Nyerere alisema Ikulu si sehemu ya kukimbilia pale, kuna matatizo chungu mbovu.
 
Haya yameshapangwa, huyo mpina 2025 hapitishwi na CCM, na kura zitaibwa ili asishinde
Huyu mdada ni collateral tu kwa kuwa ni non elect member ndio maana anatumika
Hii nchi hakuna wa kuishinda CCM, the rest is history
 
Nilichogundua hii nchi viongoz wengi hawana uzarendo kabisa ila wanateuana kwa lengo la kulindana na kulinda masrah yao tu.
Mkuu mbona Hilo la pili ndiyo uhalisia?

Nchi hii hakuna kiongozi mwenye nia ya dhati ya kuwaongoza wananchi kwenye kutafuta maendeleo.

Wote wanaingia kujitafutia mali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…