CCM chini ya Mwenyekiti wake Samia Suluhu Hassan iko imara kuliko kipindi chochote


Ni hivi, mpake mafuta huyo mama kwa mgongo wa chupa utakavyo, lakini iko wazi kuwa ccm sio chama cha kizazi hiki. Ccm ni chama cha watu wa kizazi kilichopita, na wako madarakani kwa shuruti. Hawana uwezo tena wa kushinda uchaguzi wowote kihalali zaidi ya kutegemea vyombo vya dola. Ni kweli huyu mama hana siasa za kihayawani kama alivyokuwa Magu, lakini hana ubora wowote wa kiuongozi.
 
 
Daaah! Mnamdanganya sana mama yetu.

Hatutaki afe na presha tunamhitaji ni hazina yetu.

Tumwambie ukweli.

CCMimemaliza mvuto kwa wananchi na wanachama wake. Sababu ni msoga
CCM iko imara, nimezunguka mikoa yote ya Tanzania nimeona imani ya Vijana na Watanzania kwa ujumla waliyo nayo kwa Chama cha Mapinduzi na kwa Rais Samia Suluhu Hassan
 
Mkuu CCM hii ni imara kuliko kipindi chochote..Hakuna upinzani utakao wenza shindana na Ccm hii ya Samia
 
Kabisa!

Ukiona hata machadema yameunga tela kumsifia mama ili kumkomoa marehemu jiwe jua hapo kuna jambo.

Yani ccm na hangaya 2025 watakuwa na kazi rahisi sana.

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app

Dhalimu hakomolewi bali alikuwa kiongozi mshenzi. Ww ndio ulikuwa unashoboka naye.
 
Tunaomba CCM imara msimamie Serikali ya mama kwenye bei ya mbolea maana tunajua kuna vita huko Ukraine ila sio kwa kupanda hivyo.
Mkuu ROBERT MICHAEL kuwa na imani na Ccm, Ccm ya sasa ina macho na masikio, Mwenyekiti wetu anawaambia Wananch ukweli vitu vingi vinapanda bei kwa sababu ya vita ya Russia..
 
Yanatoka moyoni au ndio zile fitina mnazosema kinaa kuwa ni mwiko hapo mtaani kwenu[emoji848]
Nikiwa Mtanzania tena Mzalendo, nimetemebea kusini na kaskazin, mashariki hadi magharibi, kwa kweli vyumba vya madarasa vinavyojengwa, zahanati, vituo vya Afya, hospital, miradi ya maji etc kwa kweli haya ninayoongea yanatoka moyoni
 

Chini ya Magufuli ccm ilitoka kuwa chama cha siasa na kuwa chama cha mumiani, chini ya utawala wa Magufuli chaguzi zote ziliendeshwa kihayawani. Kuteka, kubambikizia kesi, mauaji nk. Alitawala kwa kiburi cha madaraka, ndio maana idadi ya wapiga kura ilishuka kuliko maelezo, hadi ikabidi apike idadi ya wapiga kura. As a result wananchi kwa sasa wamelipuuza box la kura, na sitegemei kuona tena wapiga kura wengi, labda ipatikane katiba mpya.
 
Vijana wa CCM kazi yao kusifia hata kama nchi inaelekea shimoni
Mkuu nini nilichosifia ambacho ni uongo? Je hupiti vijijini ukaona Wananchi walivyo na furaha sasa? Wanafunzi wote wanakaa kwenye viti, Zahanati kila kijiji, vituo vya Afya kila Kata, Hospital za Wilaya zinaboreshwa, Maji safi na salama kila sehemu..Je yakufaa nini kudanganya fahari ya macho yako?
 
Mkuu CCM hii ni imara kuliko kipindi chochote..Hakuna upinzani utakao wenza shindana na Ccm hii ya Samia
Ccm ni chama outdated na haitakaa iwe na mvuto tena. Hiyo ccm ni kama bendi za sikinde na Ottu jazz, muda wake wa kung'aa ulishapita. Usitegemee kama bendi hizo zitakaa zipate mvuto tena maana kizazi chao kilishapita.
Labda kama unaishi Sayari tofauti na hii lakini kiuhalisia Ccm kwa sasa hali ni mbaya hamna mvuto tena kama kipindi cha Mzee JPM

Chini ya Magufuli ccm haikuwahi kuwa na mvuto bali ya vitisho na ulevi wa madaraka.
 
Mkuu Amini nakwambia, kama Wapinzani watashindwa kufanya siasa kipindi hiki basi ni bora kuwa na mfumo wa Chama kimoja, mnyonge myongeni ila haki yake mpeni, Mama Samia ametengeneza neutral ground katika nyanja ya siasa ndani ya mwaka mmoja...Ndugu yetu Mbowe alienda kwenye kongamano Iringa hakuna aliyemzuia..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…