CCM Fahamuni kabisa: Kilichofanywa na Asha Rose Migiro ni uhaini na atakilipia

Yeah Katiba inasema Rais anatakiwa kuwa Mwanachama wa Chama Cha Siasa.
Wewe nawe kumbe akili zilezile tu.

Katiba inasema hivi:

Mosi, kwa madhumuni ya kugombea nafasi ya Uraisi ni lazima uwe mwanachama.

Pili, kwa madhumuni ya kinidhamu na kuondolewa Uraisi/Umakamu, ambao ni utumishi wa ummah, hili ni suala la bunge.

Kitaalamu hivi ni vitu viwili tofauti ambavyo vinafanya lengo moja, kuthibitisha Uraisi.

A Concept of Stark-Dichotomy.


​
 
ok kama ni hvo sahivi ni VP asiyekuwa na Chama..Je, katika historia ya nchi yetu kumewahitokea VP asiyekuwa na chama cha kumuakilisha? KATIBA inasemaje na SHERIA za nchi zinasemaje.
Kwa Nchi Yetu haiwezekani
Kwa Sababu VP anachaguliwa na kuidhinishwa na Chama

Ndio maana hautakuja Kusikia VP hanachama Cha siasa
 
😃😃😃
Basi nimeelewa kwanini namba 2 alisema Wananchi wapambane kupata katiba mpya.
Kuna namna ni ngumu sana kutaka kupindua meza au kufanya mabadiliko yoyote ukiwa na hii katiba.
Alikuwa anajua hiki cha kulazimisha kujiudhulu Kwa Nia ovu, lipo njiani, kings yake ni hii Katiba, kwamba Bunge ndio wanauwezo wa kumtoa madarakani
 
Sio Swala la Bunge peke yake chama pia kina husika Kwa Asilimia 70

Kwa Sababu ndio kilicho muajili au kilicho muweka kwenye hiyo Nafasi.
 
Hebu kaa pale tulia bwana mdogo.

Tena utulie tukufunde vizuri sheria.

KWANZA KABISA: hivyo unachokisema wewe kitaalamu tunakiita The Doctrine of Mandate, ambayo inasema hivi. Mgombea anatakiwa anadi ilani na sera za chama "Party Manifesto & Policies" ambapo endapo atateuliwa atatakiwa kutekeleza zote bila kuacha hata kimoja. Hivyo kama asipotekeleza ni lazima awajibishwe kisheria.

GWIJI LA SHERIA duniani, Sir Alfred Denning a.k.a Lord Denning kwenye kitabu chake kiitwachoa "The Changing Law" akasema kwamba "The Doctrine of Mandate is unenforceable". Kwamba mgombea baada ya kuteuliwa siyo lazima atekeleze sera na ilani za chama chake kwasababu, kiuhalisia hajateuliwa na wanachama wake peke yake bali raia hata wasiokuwa wanachama.

Lord Denning akaenda mbali zaidi na kusema kwamba The Doctrine of Mandate ina changamoto kwasababu watu wanaweza kuteua kiongozi bila hata kufahamu sera za chama anachotokea. Mtu anaweza tu kupenda kitu kimoja kuhusu mgombea na vingine akavichukia. Hata wewe hapo nikikuambia uielezee ilani ya CCM nina uhakika hujawahi hata kuiona.

Hivyo sasa, kati ya Hamza Johari, Palamagamba Kabudi na Lord Denning, namfuata nani ?

BILA SHAKA, namfuata Lord Denning kwasababu yeye ni chanzo cha kimataifa kwenye somo la katiba ambaye anasomwa duniani kote, zaidi-zaidi kwenye nchi za Jumuiya ya Madola. Wewe kama unahisi Kabudi na Johari wako sahihi basi kalaghabao, wafuateeeee.
​
 
Sio Swala la Bunge peke yake chama pia kina husika Kwa Asilimia 70

Kwa Sababu ndio kilicho muajili au kilicho muweka kwenye hiyo Nafasi.
Kijana hebu kaa kwa kutulia.

Raisi ni mtumishi wa Ummah anayetumia wananchi wote, siyo CCM peke yake.

CCM ni chombo kinachotumika katika kutusaidia watanzania kupata Raisi bora, si vinginevyo.
​
 
Hayo mengine ni yenu, mimi nafuata nini katiba inasema!

Makamu wa Raisi ni mtumishi wa ummah, siyo mtumishi wa CCM.

Kujidanganya kwamba CCM inaweza kumvua makama wa Raisi nafasi na akapoteza sifa za kuwa Makamu ni uhaini na uvunjifu mkubwa wa katiba, kwasababu Makamu wa Raisi ameteuliwa na mamilioni ya watu hata ambao siyo wana-CCM, hivyo kumvua uanachama na kumtoa kwenye nafasi ni kuvunja haki ya kikatiba ya watanzania za kushiriki katika siasa za ummah kwa kuchagua viongozi au kuchaguliwa (Right to participate in political affairs of the state).
​
 
Tukianzia hapo kwenye nadhalia ya sir Alfred Denning

Ni kweli kwamba haiwezekani kuitekeleza Ilani Kwa Asilimia 100%, Kuna Wakati yatafanyika Maamuzi Kulingana na uhitaji,

Lakini saikologia inayo ishi ya siasa Zetu Tanzania

Ni kwamba Kiongozi anapo piga Kampeni ana nadi Ilani ya chama chake na sio mipango yake binafsi

Kwa hiyo ikitokea Raisi Yeye anafanya Mambo yake nje Kabisa na Ilani Kwa afrika na Tanzania atakuwa termed Kama dikteta na anae pokea maagizo kutoka nje

Kwa Sababu hakutakuwa na mawasiliano kati ya wabunge wa vyama vya siasa Wakuu wa mikoa, Wakuu wa wilaya na Raisi mwenyewe. (Kwa Sababu hao pia ni mapendekezo ya chama)
 
Mosi, Raisi ni mtumishi wa ummah, siyo mtumishi wa chama!

Pili, Ilani ya chama siyo nyaraka ya kisheria, katiba ni nyaraka ya kisheria.

Tatu, kama Raisi angekuwa ni mtumishi wa CCM basi wao ndiyo wangekuwa wanamlipa hadi mshahara na kila stahiki zake zote kama ulinzi na mengineyo. Raisi analipwa kwa kodi zetu sisi watanganyika wengi, siyo CCM.
​
 
Kijana hebu kaa kwa kutulia.

Raisi ni mtumishi wa Ummah anayetumia wananchi wote, siyo CCM peke yake.

CCM ni chombo kinachotumika katika kutusaidia watanzania kupata Raisi bora, si vinginevyo.
​
Labla tusaidiane kwanza,
Nini maana ya Chama Tawala
Na ukisikia chama kinasema kima shika Dora kina maanisha Nini?
 
Nimeshaandika humu kwenye Uzi wa britanicca kuwa Samia lazima ashitakiwe ICC ni suala la Muda tu pia nikaandika DGIS TISS Mr. Mombo naye ATAMALIZWA tu ni suala la muda , USALITI na kuvunja misingi ya Katiba au kuvunja work culture ya Taasisi haijawahi muacha mtu salama

Asante kwa kukazia hili la ICC
 
Yeah, sisi watanzania tunashindwa kufikiria mbele tunavyotunga vitu vyetu. Mara nyingi kanuni zinaanza kutungwa pale tatizo linapotokea.

Kuwa na akili mgando huwa ni kitu mbofu mbofu hivi 🤌
Hili katiba linampa mtu moja nguvu ya kuwanyongea wenzake halafu yeye yupo "SAFE" aguswi.

Huyu mtu anaweza kuuwa wote likataka kubaki yeye tu Tanzania
 
Ndio ni Mtumishi wa umma,
Lakini yupo pale kukiwakilisha Chama Cha siasa kilicho shinda uchaguzi,

Kinacho Tawala ni chama sio Mtu.
 
Labla tusaidiane kwanza,
Nini maana ya Chama Tawala
Na ukisikia chama kinasema kima shika Dora kina maanisha Nini?
CHAMA TAWALA ni neno la kikomunisti siyo neno la kisheria.\\

Muhuni Nyerere na wenzake ndiyo walipenda kulitumia kuwarubuni watanganyika.

Hilo neno halipo kwenye katiba, hivyo siwezi kuhangaika na tafasiri yake.
​
 
Sasa tufanyeje kutokA KWENYE HUU MKWAMO?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…