CCM Fahamuni kabisa: Kilichofanywa na Asha Rose Migiro ni uhaini na atakilipia

CCM Fahamuni kabisa: Kilichofanywa na Asha Rose Migiro ni uhaini na atakilipia

Jiulize hivi kimantiki:

CHAMA KIMEMFUKUZA, halafu BUNGE LIKAKATAA KUMTOA MAKAMU, nini kitatokea ???

Tena jiulize hivi:

Raisi/Makamu wamechaguliwa na watanzania hata wasiokuwa na chama, unapomfukuza uanachama unawaambia nini watanzania wasiokuwa wana-CCM, kwamba leo hii CCM ikiamua tu ndiyo basi ???

HAKUNA KITU CHA NAMNA HIYOOOOO!
​
Tanzania Uchaguzi hautambuliki Duniani ule haukua Uchaguzi bali Ulikua Mauaji
 
Sawa kabisa, hii ni sifa ya kugombea kwa dhumuni la uchaguzi (For Purposes of Election)

Nioneshe ni wapi katiba inasema moja kwa moja kwamba Raisi/Makamu akivuliwa uanachama basi anapoteza sifa kuwa Raisi/Makamu ???

Kwamba mnatafasiri katiba by a way of implication ???

Kwamba kwasababu kwenye uchaguzi ni lazima awe mwanachama, basi kwenye nidhamu nako itakuwa hivyo-hivyo ???

Sasa kulikuwa na maana gani ya kuweka Impeachment Sections ???
​
Screenshot_28-8-2026_13147_.jpeg




Screenshot_28-8-2026_13037_elibrary.osg.go.tz.jpeg



kufuatia ufafanuzi wa mwanasheria mkuu wa serikali,

(4) Mtu hatateuliwa kugombea au kushika kiti cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganoisipokuwa tu kama---


(4) A person shall not be nominated to contest for the office of VicePresident of the United Republic, save only if -


mliobobea kwenye hii sekta tupeni msaada wa huu utofauti wa toleo la kiswahili na la kiingereza,
ina maana nchi inaweza mpoteza rais kisa chama chake kimeweza mvua uanachama pia?
 
Ni sawa, lakini utaratibu sahihi uliopaswa kufuatwa ni:

1. HATUA YA 1; Ni kweli CCM wamefanya ya kwao, wamemfuta uanachama. Hilo hatuhoji wala hatuwaingilii, ni mambo yao

2. HATUA YA 2; Rais kwa kufuata utaratibu wa kikatiba, alipaswa kupeleka hoja au taarifa Bungeni kuwa liliridhie kuondoka/kuondolewa kwa VP kwa sababu 1, 2 nk hata kama ni hiyo ya kufutiwa uanachama

3. HATUA YA 3; Bungeni kupitia azimio lake maalumu, linaliridhia au linakataa kuikubali hoja hiyo

4. HATUA YA 4; Hoja hurudishwa kwa Rais/serikalini. Kama imekubaliwa, maana yake hoja sasa inarudi chamani huko kilichomdhamini kiendelee na utaratibu wake kama katiba kuu ya nchi inavyoelekeza..
==========
#Kinyume chake, kilichofanyika sasa, every step ni mchanyato, corrupted..

#Kwa kifupi ni kuwa, CCM wamefanya au wamepora mchakato wote ikiwemo ule wa kibunge..

# Msikilizeni Mwanasheria Mkuu wa serikali Hamza Johari anavyopata taabu kuliweka sawa jambo hili. Wamekosea na kuharibu na sasa wanaanza kufanya damage control

#Ukweli ni kuwa wamevunja katiba, wamefanya uhaini. Au hatujui kuwa kisheria na kikatiba as we speak this moment Dr Emmanuel Nchimbi still ni Makamu wa Rais? Yes, still ndiye untill 4th September 2026 na mpaka utaratibu wa kikatiba utakapokamilika!!
Upo sahihi
Uo ni utaratibu Kama VP asinge Tuma Barua ya kujihudhuru
 
Anapoteza sifa ya kuwa kwenye nafasi husika au ya kugombea nafasi? Maana kugombea nafasi vs umeipata nafasi ni vitu viwili tofauti.

Katiba inasemaje? Kama hujui Sema sijui mkuu usifanye spinning. It's ok kutokujua, hata mimi sijui ndo maana nauliza.

Mfano: Ili kupata kazi lazima uwe na wadhamini, ila ukishapata hiyo kazi nafasi ya mdhamini kwenye kukuondoa kazini ni finyu. Huu mfano nimekupa ili unielewe ninachouliza kuhusu kugombea nafasi na kuwepo kwenye nafasi.
Kwani Sheria ilikuwa hairuhusu mwanafunzi mwenye mimba kujiunga na Masomo,

Vipi Kama akipata mimba katikati ya Masomo utaratibu inakuwaje?
 
Sijui kama wanakuelewa.
Wengine kwenye chama na serikali watajikuta matatizoni bila kupenda.
Wakipinga huu uhuni nao watashughulikiwa kama Nchimbi, Mpina, Polepole na Simbachawene.
 
Kwanza Kabisa sifa za Mtu kugombea nafasi hiyo lazima awe mwanachama wa chama Fulani Cha siasa.

Hii tu Inatosha kumaanisha kwamba Kama Mtu hana chama chochote Tayari kapoteza sifa za kuwa kwenye nafasi husika.
BB_DANGOTE, kwa bahati mbaya sana katika hii nchi yetu watu wenye mindset kama zako ndio mmetamalaki na haya tunayopitia ndio matokeo yake.

Kweli huwezi kupanda mchicha ukavuna parachichi.

Nchi yangu pendwa iliyojaaliwa kila neema, tumekukosea nini? Kwamba baada ya nusu karne tuko pale pale...inashangaza, inasikitisha na inaudhi.

Chama kile kile, watu wale wale, fikra zile zile na akili zile zile...
 
Famahamuni haya fika.

Mfumo wetu wa Uraisi ulioanza mwaka 1995 wa mgombea mwenza tumeuiga kutokea nchi ya Marekani, ambapo Raisi na Makamu wake wanateuliwa kwa pamoja, na wanaanza kazi siku moja. Hivyo kinga ambayo anaipata Raisi ndiyo hiyo-hiyo anaipata Makamu wake. Kitaalamu hii tunaiita Functional Immunity (From Civil & Criminal Proceedings).

Emmanuel Nchimbi, unaweza usimpende lakini analindwa na katiba kama ambavyo Raisi Samia alilindwa na Katiba mwaka 2021 wakati akiwa Makamu wa Raisi asiyekuwa anaifahamu hatma yake. Wengi hatukutaka Raisi Samia awe Raisi, lakini Kikwete na Mabeyo ndiyo walimfanya Samia akawa Raisi. Wengi hatukupinga wala kulalamika kwasababu lilifanyika kikatiba.

SASA BASI, nchini Tanzania kuna haya yafuatayo ambayo yako bayana kabisa:

MOSI, Mamlaka ya nidhani (Disciplinary Authority) ya Raisi na Makamu wake ni Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Siyo Msajili wa vyama, siyo Jaji Mkuu, siyo Jeshi na wala siyo NEC ya CCM. Makamu wa Raisi hata kama Raisi hampendi anatakiwa apeleke mashitaka kwenye chama, halafu chama wapeleke mashitaka hayo bungeni ambako wataanzisha mchakato wa kumvua nafasi makamu wa Raisi (A motion of Impeachment), ambao utaishia na azimio maalumu ya kuthibitisha kwamba makamu atolewe au asitolewe (A Resolution Confirming Impeachment).

NEC ya CCM kumvua uanachama Makamu wa Raisi Emmanuel Nchimbi, ambaye kwa barua yake amesema ataondoka kwenye nafasi yake ifikapo tarehe 4 Septemba 2026 ni UHAINI. CCM imepoka madaraka ya Bunge na kutikisa taasisi ya Uraisi.

Fahamuni fika, kwamba leo hii akifariki Raisi Samia kabla ya tarehe 4 Septemba 2026, Raisi wetu atakuwa ni Dr. Emmanuel Nchimbi na siyo mtu mwingine. Hivyo ambacho mnakifanya sasa ni uhuni utakaokuja kuwatokea puani siku siyo nyingi, maana mshajenga mfano mbaya (A Bad Precedent)

PILI, Kinga ya Raisi ndiyo kinga ya Makamu Wake. Raisi na Makamu hawawezi kushitakiwa popote pale. Lengo la kumpa Raisi na Makamu wake kinga ni kuhakikisha ofisi ya Raisi inathibitika ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu makubwa ya kitaifa. Hivyo madai yote dhidi ya Raisi na Makamu ni lazima yapitie bungeni kwanza. Mtu hawezi kuamka tu akasema leo hii hatumpendi fulani basi tumvue uanachama ili apoteze nafasi yake ya Uraisi au Umakamu. Kama hili litakuwa linafanyika, hatutakuwa na nchi bali gulio ya washenzi, ambapo kila muhuni anaamka tu na anamuondoa Raisi akijisikia.

========================================================================

JAMBO LOLOTE BAYA, likimtokea Makamu Wa Raisi, Dr.Emmanuel Nchimbi kipindi hiki hata baada ya kuachia nafasi, sisi tutalichukulia hili kama UHAINI. Kinara wa huo uhaini ni Dr. Asha Rose Migiro na wengine. Mlipoka madaraka ya bunge kwa kuifanya CCM ivumbe Ibara ya 50 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na kwasababu mshaonesha nia ovu, hata baada ya 4 Septemba 2026, tutaangalia kwamba lolote litakalotokea kwa Dr.Emmanuel Nchimbi halikuanzia bungeni, hivyo ulikuwa ni UHAINI usio na uhalali.

JINAI haiozi, wote mliohusika na hili sakata, ombeni sana MUNGU hata siku moja asiingie mtu mwendawazimu kwasababu mtanyongwa na kupigwa risasi barabarani kama wanyama. Hili wala haliitaji ushahidi, tumeona mkivunja katiba waziwazi na kufanya mambo ambayo yanatishia usalama wa Makamu wa Raisi.
========================================================================

Wajinga wengi watatoa mfano wa kuondolewa kwa Aboud Jumbe Mwinyi, lakini ukweli ni kwambwa mwaka 1984, Mwinyi alikuwa Makamu wa Pili wa Raisi, ambaye aliongoza Zanzibar iliyokuwa haina hata KATIBA yake. Tena kubwa zaidi ni kwamba alikuwa anateuliwa na Wazanzibari tu, siyo watanzia wote.

Hili la sasa litasababisha matatizo makubwa mnoooo siku za karibuni.
=========================================================================

Wiki chache zilizopita wanasheria wa Tanzania wameenda ICC wakiongozwa na mwanasheria mkubwa ambaye jina lake hatutalitaja hapa. Kinachoendelea huko duniani ni kibaya na hata hii tume ya pili haitaweza kukizuia.

Binafsi huwa nasema hivi: NI SUALA LA MUDA TU..........


​
Uhuni wamefanya mwingi sana
 
Kama wabunge wakifutwa uanachama wanapoteza nafasi zao za ubunge katika majimbo ya wananchi wao waliowachagua basi pia ni hivyo hivyo kwa rais na makamu wa rais kwa sababu wote katiba inataka wawe na udhamini wa chama nyuma yao ili waweze kushika hizo nafasi. Spika wa bunge tu ndiye hawezi kuondolewa na chama madarakani kama ana sapoti ya wabunge wengi hata kama chama kikimfuta uanachama.
mwenye utashi wa maamuzi kwenye hii nchi ni rais tu Wala sio katiba,maamuzi ya rais kwa wakati huo ndio yenye nguvu Wala sio katiba wala sheria,rejea kesi ya wabunge wa covid 19 waliofutwa uanachama na chadema kwani waliondolewa bungeni!!?? Rais aliamua kwa manufaa yake kwamba wabaki bungeni japo alikuwa anavunja katiba.HII NCHI RAIS AMEPEWA MADARAKA MAKUBWA KUPITILIZA KIASI KWAMBA ANASIGINA MPAKA KATIBA
 
BB_DANGOTE, kwa bahati mbaya sana katika hii nchi yetu watu wenye mindset kama zako ndio mmetamalaki na haya tunayopitia ndio matokeo yake.

Kweli huwezi kupanda mchicha ukavuna parachichi.

Nchi yangu pendwa iliyojaaliwa kila neema, tumekukosea nini? Kwamba baada ya nusu karne tuko pale pale...inashangaza, inasikitisha na inaudhi.

Chama kile kile, watu wale wale, fikra zile zile na akili zile zile...
Huo ndio mfumo wa Nchi Yetu
Ulio kuwepo tangia Kipindi Cha waasisi wetu kina Mwl. Nyerere

Na Mtu yeyote akisoma makala Yao atatoka na mtazamo Huu.
 
Wahuni wametamalaki no mitigation wala consequences evaluation… wanalotaka wanafanya.
 
View attachment 3658843



View attachment 3658844


kufuatia ufafanuzi wa mwanasheria mkuu wa serikali,

(4) Mtu hatateuliwa kugombea au kushika kiti cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganoisipokuwa tu kama---


(4) A person shall not be nominated to contest for the office of VicePresident of the United Republic, save only if -


mliobobea kwenye hii sekta tupeni msaada wa huu utofauti wa toleo la kiswahili na la kiingereza,
ina maana nchi inaweza mpoteza rais kisa chama chake kimeweza mvua uanachama pia?
To contest vs To Hold....

Which is Which ???

Katiba mbili zinakinzana!

Hivyo hapa katiba ya Kiswahili ndiyo halali......!

Kushika na Kugombea ni vitu viwili tofauti kabisaaa.........!
​
 
Back
Top Bottom