CCM: Gazeti la Uhuru limepotosha; Rais Samia hakusema kuwa hatogombea 2025

CCM: Gazeti la Uhuru limepotosha; Rais Samia hakusema kuwa hatogombea 2025

Tunaposema ndani ya CCM kuna watu wanahujumiana au wanamhujumu Rais Samia hamtuelewi mambo yanaanza kuwa wazi sasa. Gazeti mama la chama haliwezi kuandika habari hii bila kuwa na mkono wa viongozi wakubwa ndani ya chama.

Mama shituka mapema you will thank me later.

View attachment 1888095

PIA, SOMA:
- Gazeti la Uhuru: Rais Samia hana wazo la kugombea Urais 2025
Chama hakijieleqi kwa sasa kabisa

huko kunafukuta KWA SANA

POLENI SAAANA

Sent from my Moto E (4) using JamiiForums mobile app
 
Chama cha Mapinduzi kimesikitishwa na upotoshwaji mkubwa uliyofanywa na gazeti la Uhuru toleo Namba 24084 la leo Jumatano 11 Agosti, 2021, gazeti hili limepotosha sehemu ya mahojiano aliyofanya Rais Samia Suluhu Hassan na BBC.

Katika habari yake kuu limeandika kichwa cha habari “Sina wazo kuwania urais 2025- Samia” Huu ni upotoshwaji mkubwa na kumlisha maneno Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan hakusema kabisa maneno hayo, hili ni kosa kubwa linalokwenda kinyume na sera inayoongoza vyombo hivyo, jambo ambalo halitavumiliwa hata kidogo hivyo HATUA KALI za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wote waliohusika katika uandaaji wake.

Gazeti la Uhuru ndiyo “Adam na Hawa” wa magazeti yote hapa nchini, linawajibika kuonesha weledi wa hali ya juu na sio vinginevyo.

Tunawaomba Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na watanzania kwa ujumla kupuuza habari hiyo kwani imeandikwa na watu wenye maslahi yao binafsi.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan fikra na nguvu zake kwa sasa zimejikita katika kuwatumikia watanzania na si vinginevyo” ——— Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
Itikadi na Uenezi. #MillardAyoUPDATES
 
Mama anatakiwa awe mjanja sana ashtuke mapema sana hilo genge mbona jepesi ila hayo mambo yake ya 'Hewala si utumwa' kwa kila anachoshauriwa na hao
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Bavicha mnataka kuaminisha uma kwamba kuna watu wana mhujumu mama.

Mwanzo mlifikiri hata kukamatwa kwa Mbowe ni hujuma ndani ya chama ila juzi mwenyewe kakiri anajua kila kitu!

Kivuli cha Magu bado kinawatandika. Yani hata baada ya Magu kufariki bado mnafikiri kushindwa kwenu ni kwa sababu yake.

Hao watu wanaomhujumu muwe mnawataja kwa majina na kwa vipi wanamhujumu
 
Tunaposema ndani ya CCM kuna watu wanahujumiana au wanamhujumu Rais Samia hamtuelewi mambo yanaanza kuwa wazi sasa. Gazeti mama la chama haliwezi kuandika habari hii bila kuwa na mkono wa viongozi wakubwa ndani ya chama.

Mama shituka mapema you will thank me later.

View attachment 1888095

PIA, SOMA:
- Gazeti la Uhuru: Rais Samia hana wazo la kugombea Urais 2025
Duuh, mnara wa Babel lazima uporomoke...

Yaani CCM ya upande wa kushoto na gazeti lao inaandika uongo juu ya Rais wao na m/kiti wao wa CCM taifa...

Halafu CCM ya upande wa kulia inakanusha kuwa hakuna kitu kama hicho halafu msajili wa magazeti kimyaaaaa...!
 
Mama kila siku tuna mshauri kuwa makini na masalia ya mwendazake lakini hatuelewi. Haya sasa ameanza kuhujumiwa wazi wazi na huenda hata miaka minne ya urithi asiimalize
Kwani yeye Samia ni salia la nani?
 
Kwahiyo unakubali kuna mgogoro.
Kawaida kila sehemu yenye watu zaidi ya mmoja, kama hutaki mgogoro nenda kaishi maporini na nyani, ambao nao utagombana nao tu pale mtapoanza kushare same resources! Jambo muhimu kwenye mgogoro ni vipi mnaushughulikia, hilo CCM wapo mbali sana. Hizi kelele za akina Gwajima na Polepole za hizi wiki 2 ingekuwa pande zenu huko tayari ingeitwa kamati kuu ya dharula na kuwavua uanachama.
 
Acheni ramli chonganishi, CCM huwa wanajua kushughulikia mambo yao ya ndani kwa weledi mkubwa! Kuna migogoro ilishaibuka huko mikubwa mnoo, ikatulizwa, mojawapo ni ule mgogoro wa 2015 ambao mwishowe waliwatupia takataka lao huko kwenu mkalimeza mazima, likawamaliza nyinyi. Hamna mgogoro CCM kwa sasa.
Umekumbusha mbali mno! Ungewakumbusha hili la karibuni la bwana Maembe
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Bavicha mnataka kuaminisha uma kwamba kuna watu wana mhujumu mama.

Mwanzo mlifikiri hata kukamatwa kwa Mbowe ni hujuma ndani ya chama ila juzi mwenyewe kakiri anajua kila kitu!

Kivuli cha Magu bado kinawatandika. Yani hata baada ya Magu kufariki bado mnafikiri kushindwa kwenu ni kwa sababu yake.

Hao watu wanaomhujumu muwe mnawataja kwa majina na kwa vipi wanamhujumu
Kukiri kwenyewe kuwa Mbowe ni gaidi ndio hujuma yenyewe atakuja kujua kuwa hajui baadae sana.
 
Kawaida kila sehemu yenye watu zaidi ya mmoja, kama hutaki mgogoro nenda kaishi maporini na nyani, ambao nao utagombana nao tu pale mtapoanza kushare same resources! Jambo muhimu kwenye mgogoro ni vipi mnaushughulikia, hilo CCM wapo mbali sana. Hizi kelele za akina Gwajima na Polepole za hizi wiki 2 ingekuwa pande zenu huko tayari ingeitwa kamati kuu ya dharula na kuwavua uanachama.
Kwani sisi tumesemaje?
 
Umekumbusha mbali mno! Ungewakumbusha hili la karibuni la bwana Maembe
Hahaha, huyo watasema alienda CCM B, si unajua wanavyojiona malaika? Nimewakumbusha kapi walilomezeshwa zimazima na bwana DJ
 
Mama anatakiwa awe mjanja sana ashtuke mapema sana hilo genge mbona jepesi ila hayo mambo yake ya 'Hewala si utumwa' kwa kila anachoshauriwa na hao
Mama kitu anachoshindwa kuelewa ni hivi
Kipindi mama ameingia madarakani timu Magu wakiongozwa na Veronica walikuwa wanampiga vita, watu wa upinzani na hasa wale waliokuwa wameumizwa na utawala uliopita ndio walikuwa wakimpa support kubwa na viongozi wa dini

Bahati mbaya sijui kwa maksudi au kushauliwa na watu wasiokuwa na nia njema nae wakamwingiza chaka akaanza kutoa kauli za majivuno na kuingia kwenye utawala wa kukandamiza upinzani (kesi ya Mbowe) na kuwaita wafanya fujo wanaotaka katiba mpya eti wanaleta chokochoko

Mwisho kaja kuharibu pande zote mbili na Sasa hana mtetezi.

Kiufupi mama kajamba kwenye maji
 
Back
Top Bottom