Don Vill
JF-Expert Member
- May 4, 2020
- 2,249
- 5,674
Kabisa , na hapo ujagusia watu wasio na ajira wala fursa zozote za kiuchumi + wavuja jasho , wasakatonge mamilioni wanaovvuja jasho kwa kufanya kazi ngumu na hatarishi ,zinazotweza utu na za ujira mdogo usioendana na hali ya maisha.Hakuna mtu atalalamika kama wote tutakuwa tunaishi kama mawaziri. Siku zote malalamiko hutokana na kutoridhishwa na hali na jambo hilo hutokana na kukosekana usawa.
Kuna matabaka makubwa sana ya watu kwenye jamii hii hii ambayo hao wana CCM wana mchango mkubwa sana kuitengeneza. Hakuna usawa ila inapokuja swala la haki. Hiki ndio kiini cha malalamiko ya vijana.
Haiwezekani mtu anaelipwa laki 4 anyimwe allowance na benefits za utumishi ila anaelipwa million 20 ajaziwe allowances na benefits kibao pamoja na seminar na masafari. Yani mwenye uwezo wa kukabili ugumu wa maisha kwa basic salary anaongezewa mihela kibao. Ambaye hawezi anapambana na matozo.
Hii ndio Tanzania ambayo huyo mpuuzi mtoa mada anataka kuwaambia watanzania waishukuru ccm kwa kuiendeleza mpaka tulipofika hapa.