UHURU JR
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 16,543
- 7,880
Mleta mada analinganisha Tanzania ilivyo sasa na huko zamani na kuhitimisha kuwa serikali ya chama cha mapinduzi imefanya kazi kubwa sana kwamba hali ilivyo sasa ni juhudi za ccm hivyo tuipongeze, sasa najiuliza kama Tanzania ilivyo sasa ccm wanahitaji kupongezwa je vp Tanzania ingekuwa endapo ccm isingekuwa imefanya vizuri kwa mtazamo wa mleta mada?
Kwa sababu zipo nchi ambazo zina umri sawa na sisi ila zimetupita mbali sana kimaendeleo bila ya shaka nao kama wasingefanya juhudi basi wangekuwa kama sisi maana tulikuwa wote sawa, ila sisi tunajilinganisha sisi wenyewe et tulipotoka na tulipo kwa miaka yote 60 na kujiona tumefanya makubwa sana.
Rais Samia anasema tusijilinganishe na nchi za wenzetu huko zilizoendelea zenye miaka zaidi ya 200, sawa ila mbona hata nchi zenye miaka sawa na sisi pia zimetupita mbali kimaendeleo?
Kwa mitazamo ya mleta mada anataka kuzidi kudumaza akili zetu kujiona tunaenda sawa na wakati katika maendeleo, miaka 60 ya kujitawala bado tu watu wanakosa hata maji safi ya kunywa na wanafunzi wanakaa chini kwa kukosa madawati achilia mbali ubovu wa elimu yenyewe halafu mtu anataka tupongezane kwa hali hiyo sasa kinyume chake ndio hali ingekuwaje?