CCM inahitaji pongezi nchi hii, tulipotoka tunapajua wenyewe. Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni

CCM inahitaji pongezi nchi hii, tulipotoka tunapajua wenyewe. Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni

Kabla ya 1961 palikuwa na mfumo wa Vyama vingi.

Umewahi kujiuliza vingeendelea kuwepo, na chama cha upinzani kingechukua uongozi mwaka 1970,

Tungekuwa wapi kama Nchi hivi Leo?
Angalia historia ya vyama vyote vile na ulinganishe ubora na weledi wake na chama cha TANU.Fanya hivyo kwanza afu tuendelee kujadili kaka.Karibu sana
 
Nakazia:
Naipongeza CCM kwa kututoa kwenye umasikini na kutupeleka kwenye ufukara.
Ukuwa kama kijana wa taifa la kesho ni muhimu kujua mchango wa serikali yako.Lugha za kebehi na matusi hazisaidii kutatua changamoto zinazoikabili jamii
 
Angalia historia ya vyama vyote vile na ulinganishe ubora na weledi wake na chama cha TANU.Fanya hivyo kwanza afu tuendelee kujadili kaka.Karibu sana
Kabla ya kwenda huko,

Sababu za kufuata mfumo wa Vyama vingi tulipopata uhuru zilikuwa sawa?
 
Usitake kutawmabia kuwa umeishi Colonial era kama vile unawaelewa vizuri. Fact zinazungumza walikua bora mno kulinganisha na CCM
Mdogo wangu kweli unajua hali halisi za watu wakati wa ukoloni????Au umesoma tu kwenye vitabu???
 
Ukuwa kama kijana wa taifa la kesho ni muhimu kujua mchango wa serikali yako.Lugha za kebehi na matusi hazisaidii kutatua changamoto zinazoikabili jamii
Kaka,
Kama Dar es salaam tu peke ake Bado huduma za jamii ni Duni, na hiyo CCM imeshakaa madarakani miaka 60.
Je tuwape muda Tena?
 
Kwa wale waliozaliwa miaka ya 60 na 70 na 80 wanaelewa tunaposema japokua mapungufu yapo ila serikali ya Tanzania chini ya CCM inahitaji pongezi kwa tulipofika mpaka sasa.

Vijana wa nchi hii wanahitaji kuelimishwa zaidi katika hili maana wamekua mabingwa wa kulalamika tu. Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni.
Hakuna mtu atalalamika kama wote tutakuwa tunaishi kama mawaziri. Siku zote malalamiko hutokana na kutoridhishwa na hali na jambo hilo hutokana na kukosekana usawa.

Kuna matabaka makubwa sana ya watu kwenye jamii hii hii ambayo hao wana CCM wana mchango mkubwa sana kuitengeneza. Hakuna usawa ila inapokuja swala la haki. Hiki ndio kiini cha malalamiko ya vijana.

Haiwezekani mtu anaelipwa laki 4 anyimwe allowance na benefits za utumishi ila anaelipwa million 20 ajaziwe allowances na benefits kibao pamoja na seminar na masafari. Yani mwenye uwezo wa kukabili ugumu wa maisha kwa basic salary anaongezewa mihela kibao. Ambaye hawezi anapambana na matozo.
 
Zilikua sawa kabisa na mwalimu alikua sawa kabisa kufuta mfumo wa vyama vingi ili kujenga nchi
Ndipo tulipofanya kosa la msingi kabisa.

Vyama vingi vinazuia vp Nchi kujengwa?

Mawazo na mfumo wa chama kimoja ndo chanzo Cha Umaskini wa watz.
 
Tumefika wapi eti? Hebu tuelezee maana mie sioni kwakweli.
 
TANU ilikuwapo tangu 1954 Hadi 1977.

Miaka 23 Bado haikutosha kuruhusu vyama vingi, ndo kwanza kikaanzishwa chama kimoja CCM.

Ni dhahiri CCM inapaswa ikae pembeni ijitafakari.
 
TANU ilikuwapo tangu 1954 Hadi 1977.

Miaka 23 Bado haikutosha kuruhusu vyama vingi, ndo kwanza kikaanzishwa chama kimoja CCM.

Ni dhahiri CCM inapaswa ikae pembeni ijitafakari.
Unatumia vigezo vipi kusema hivyo mdau??
 
Back
Top Bottom