Tetesi: CCM kufukuza Wanachama 11 wakiwemo Vigogo hawa 3

Tetesi: CCM kufukuza Wanachama 11 wakiwemo Vigogo hawa 3

Kama hukubaliani na kiongozi wako ....dawa ni kwenda kule unapoamini wanafanya unachotaka ....otherwise wajifunze kwa mzee Mangula namna alivyoshughulika na Boyz II Men walipomshughulikia ....
 
Ila ccm haiwezi kufanya kosa kama hilo kuwafukuza wabunge hata kdg. wakifanya hivyo basi majimbo yote haya ni ya UKAWA.wajaribu waone!
 
Halote wanasema weka utiwe wale wengine wanasema jaza ujazwe, tupe source ya taarifa any way.
 
Kwahiyo Dampo chadema limesha jipanga!!
Hahaha kazi kwelikweli
Hivi Wasira alipotoka NCCR na kwenda CCM kisha akapewa Uwaziri inamaanisha nini mkuu? Hivi yule mzee aliyeondoka CCM mbona aliporudi alipokewa kwa shangwe!! Kilichotupwa dampo kinaporudi nyumbani hali yake inakuwaje na ukakipokea kwa shangwe tukufikirieje??? 😀😀😀
 
Magu asipoangalia atafukuza wanachama wote kisha atajifukuza na yeye mwenyewe. Kwa ambao hamjanielewa ni kwamba, chama ni wanachama. Sasa ukifukuza wanachama wote kutakuwa hakuna chama. Kwahiyo naye atakuwa amejifukuza toka ccm.
Mwanachama sahihi ni yule anaefuata itikadi za chama. Popote pale... Usipofuata katiba ya chama moja kwa moja umejivua uanachama.
 
Kiongozi yeyote mzuri ni lazima atofautishe kwa kiasi kikubwa vitu viwili ambavyo vinaelezeka vizuri kwa kugha ya kigeni.

1. Corporate goals (malengo ya kitaifa).

2. Personal goals ( malengo binafsi).

Sehemu yeyote ya kazi ukiona inaongozwa kirafiki ujue haitakuwa na mwisho mwema na historia itamsuta kiongozi wa juu. Kiongozi mzuri ni yule tu anayeweza kutawala na kuongoza wafanyakazi wakorofi lakini wenye karama kubwa za kiutendaji.

Hayati mwalimu nyerere aliwahi kusema. " usichanganye urafiki na kazi, kama una rafiki yako basi ukanywe naye chai".

Viongozi wengi wa afrika wanaongoza kwa kutawaliwa na personal goals kiasi kwamba rafiki yake akipata madaraka anafurahia kwa sababu kwa kiasi kikubwa atanufaika na madaraka hayo. Ovyo kabisa.

Spika wa bunge hivi karibuni alisema "Tukiruhusu viongozi wa chini au hata juu kutumia madaraka yao kufanya vitu ambavyo vinazidi madaraka yao inchi itakuwa haitawaliki'.

Ukiacha mke kwa kufikiri kuwa hafai na kuoa mwingine ujue kuwa hutakaa salama. Utakae mwoa anaweza kuwa na matatizo kuliko yule wa kwanza na ukuthubutu kumwacha utaonekane wewe ndiyo mwenye matatizo mbele ya jamii.

Katika utawala "Rate of manpower turn over" haitakiwi kuwa kubwa hasa kwenye nafasi za juu.

Inapunguza sana ufanisi wa kazi na kuwafanya viongozi wa juu kufanya kazi kwa wasiwasi.

Wafanyakazi wa chini hawatawaheshi viongozi wao kwa sababu wanajua kuwa wanaweza kuondolewa wakati wowote.
 
Yafukuzane tu! lakini CHADEMA muache kupokea makombo.
 
Kwa namna hii CCM inahamia upinzani bila kujijua na hata upinzani ukichukua nchi tutajikuta tuna watu walewale wa CCM
 
Mwanachama sahihi ni yule anaefuata itikadi za chama. Popote pale... Usipofuata katiba ya chama moja kwa moja umejivua uanachama.
Ni itikadi zipi zimekiukwa na Sophia ? Kisa alimuunga mkono mwanaccm mwenzake Lowassa uchaguzi uliopita ? Hii si ilikuwa haki yake ya kuchagua na kuchaguliwa ?

Ni itikadi gani wamekiuka hawa akina Nape, Bashe na Msukuma ? Kisa wametoa maoni yao ya kutokubaliana na mwenyekiti ktk mambo fulani fulani ? Demokrasia iko wapi ? Chama kimewekwa mfukoni mwa mwenyekiti hivi sasa.
 
Nyie fukuzaneni tu muwezavyo.,, si tunachokitaka mchanga wetu ubaki kwetu...!!
 
Back
Top Bottom