Kiongozi yeyote mzuri ni lazima atofautishe kwa kiasi kikubwa vitu viwili ambavyo vinaelezeka vizuri kwa kugha ya kigeni.
1. Corporate goals (malengo ya kitaifa).
2. Personal goals ( malengo binafsi).
Sehemu yeyote ya kazi ukiona inaongozwa kirafiki ujue haitakuwa na mwisho mwema na historia itamsuta kiongozi wa juu. Kiongozi mzuri ni yule tu anayeweza kutawala na kuongoza wafanyakazi wakorofi lakini wenye karama kubwa za kiutendaji.
Hayati mwalimu nyerere aliwahi kusema. " usichanganye urafiki na kazi, kama una rafiki yako basi ukanywe naye chai".
Viongozi wengi wa afrika wanaongoza kwa kutawaliwa na personal goals kiasi kwamba rafiki yake akipata madaraka anafurahia kwa sababu kwa kiasi kikubwa atanufaika na madaraka hayo. Ovyo kabisa.
Spika wa bunge hivi karibuni alisema "Tukiruhusu viongozi wa chini au hata juu kutumia madaraka yao kufanya vitu ambavyo vinazidi madaraka yao inchi itakuwa haitawaliki'.
Ukiacha mke kwa kufikiri kuwa hafai na kuoa mwingine ujue kuwa hutakaa salama. Utakae mwoa anaweza kuwa na matatizo kuliko yule wa kwanza na ukuthubutu kumwacha utaonekane wewe ndiyo mwenye matatizo mbele ya jamii.
Katika utawala "Rate of manpower turn over" haitakiwi kuwa kubwa hasa kwenye nafasi za juu.
Inapunguza sana ufanisi wa kazi na kuwafanya viongozi wa juu kufanya kazi kwa wasiwasi.
Wafanyakazi wa chini hawatawaheshi viongozi wao kwa sababu wanajua kuwa wanaweza kuondolewa wakati wowote.