CCM kutogawa bure sare za chama kwenye uchaguzi mkuu 2020, wanachama waelekezwa kujinunulia wenyewe

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
143,138
Reaction score
288,731



Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Mh Bashiru Ally ,



lengo kubwa la mpango huu ni kutunisha mfuko wa chama ili kupata fedha za kugharamia shughuli za chama , utaratibu huu mpya umeleta sintofahamu kwa wanachama na wapenzi wa chama hicho , ambao walitegemea sare hizo kama mavazi rasmi katika maisha yao ya kila siku
 
Imekuuma
Nyie mnaoendelea kugawa bure mbona Wilayani hazizidi 10
Katuhabarisha tu naona wewe ndio umeumia, Maana kuna viongozi huku mtaani walikuwa wanazikusanya halafu wanauza bukubuku. Mimi kwamaono yangu isijekuwa watu wanataka kutakatisha pesa, wanapiga pesa za serikali zinatumika kwenye kampeni, uchaguzi ukiisha wakaguzi wakitaka kujua gharama/chanzo cha pesa za mabilioni yaliyotumika kwenye uchaguzi, uuzaji wa sare za chama utatajwa kama chanzo kimoja wapo.
 
Hahahaaa....... Umenikumbusha yale masweta ya Chadema mliyovalishwa na Mbowe kwenye uchaguzi wenu!
 
Mkuu CCM ni chama kikubwa kinapata ruzuku kubwa kwanini wanachama nao wasifaidi matunda ya Ruzuku kupewaJezi za Chama Bure?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amini nakuambia mkuu, hili suala halitowezekana na halitafanyika. Wana-Ccm wengi hali zao zinajulikana.

Na ikitokea wamejaribu, Wengi wao watavaa majani ambayo kimsingi rangi zinafanana na sare zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…