CCM kwa hiki mlichoufanyia Uwanja wa Benjamin William Mkapa, Mungu anawaona

CCM kwa hiki mlichoufanyia Uwanja wa Benjamin William Mkapa, Mungu anawaona

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,775
Reaction score
29,746
Dah,

CCM Mlijua kabisa Leo tarehe 11 October 2020 tutakua na mechi Muhimu ya Kimataifa ya Kirafiki kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars v/s Burundi lakini bado mkapitisha Fiesta lenu palepale. Uwanja wote umejaa vipara na zile ni nyasi halisi, kuota tena ni majaaliwa.

Uwanja sasa umeharibika, Mipira haitambai kama inavyotakiwa, huu ndio uzalendo kweli? Hivi hata tukifungwa si mtakua mnahusika nyinyi watu? Kweli kabisa mnathubutu kuharibu uwanja namna hii mkijua wazi utatumika tu soon? Kweli kabisa nyie ndio mnataka tuwape mitano mingine tena huku tukijua wazi hamna uchungu na rasilimali zetu?

Imenigusa sana hii,
1602431266575.png


1602423653440.png
 
Hakuna kiwanja kibovu cha Taifa kwa sasa Duniani kama hiki cha Tanzania, CCM mlichofanya sio haki kabisa.
 
Weka na ile picha ya baada tu ya shughuli...
 
Duh, aisee, pitch imeharibiwa vibaya sana. Hii ndio tatizo la kutawaliwa kienyeji. Mambo ya siasa ya upande mmoja imeharibu na kutowesha ladha ya uwanja wetu uliojengwa kwa kodi zetu lakini sasa ni kama mali ya fiscm.

Kweli imenikasirisha, Marehemu Mkapa alikuwa jeuri lakini hakuwahi kufanya kamepeni ya siasa ya chama chake kwenye uwanja wa Taifa. Safari hii tumeona mtu mwenye jeuri mbaya ya kulazimisha kufanya mambo ya ajabu, njia pekee ya kumwadhibu mtu wa aina hii ni kumwondoa madarakani kupitia box la kura tarehe 28/10.

Tuwe wazalendo na tukatae watu jeuri wasiojali matumizi bora ya miundo mbinu iliyojengwa kwa kodi zetu kiasi hiki
 
Wapuuzi wametuharibia uwanja kwa mambo ya kipuuzi kabisa hii ni dharau na kuonesha kutojali walishindwaje kuzuia pitch isiharibiwe.
 
Hivi huu uwanja si umejengwa kwa kodi zetu
Hivi una akili kweli wewe?
Kama unaangalia mpira muda huu utatambua juu ya hiki kinachojadiliwa hapa.
Uwanja umekuwa mbovu sana, kwann wasingetumia uwanja wa uhuru?
 
Back
Top Bottom