CCM mnajua kunivuruga. Niliwapenda, niliwakubali lakini sasa inatosha

Musiba Ni Nani anakutuma?
Mbona unataka kutuharibia nchi yetu?
 
Kumbuka hata mama aliteswa na mwenda zake ikizingatiwa kuwa alikuwa pale kupokea amri na siyo kutoa ushauri. Cha mno alijikaza kisabuni na kumuachia Mungu hadi alipopewa ukanda. Wengi walikuwa hata hawamheshimu kama makamu wa rais kwa vile walikuwa karibu na Jiwe. Mfano mdogo ni Dk Bashiru Ally Kakurwa na Humphrey Polepole. Hata hivyo, mama yenu ana huruma maana hawa asingewabakiza hata bungeni. Angewapangia kazi ya kukaa vijijini mwao.
 
Mkuu, you sound as if you are Ole Sabaya himself. Lazima utambue uzito wote wa gari wenye vyuma vingi huegemea chini kwenye matairi yaliyotengezwa kwa mpira kwa sababu maalum.

Basi utambue ya kuwa enzi mwendazake wengine nao walipata machungu wakati wewe ukikenua meno nje na kuwadhihaki. Kwa sasa kama ilivyokuwa kwa MATAGA wengine, hamna jinsi bali kusubiri sindano ziwaingie vizuri wakati wenye chama chao wakizidi kurekebisha mambo mliyoyaboronga.

Kuwa mvimilivu mwana. Dozi hii ni mpaka 2030.
 
Sabaya ulionywa sana ukakaza shingo,unavuna ulichopanda,na kwa taarifa ni kuwa jela inakuhusu. Wewe si ukiwateka watu ukaua,ukanyang'anya na wengine ukawalawiti,sasa zamu yako ya kulawitiwa imefika.
 
Kama vile kuna kaukweli kwa kwa mbaliii
 
Kwa jinsi Magufuli alivyotukana watu enzi za uhai wake siyo tu kwamba sasa hivi nae anapaswa kutukanwa bali pia anatakiwa afukuliwe kutoka kaburini atandikwe viboko.
 
Mama Samia kweli ni genius! Anawapooza wajinga wa awamu ya 5 huku anawapiga nyundo za kichwa!
Huyu MAMA ukitaka kujua u- genius wake fuatilia bunge la Katiba akiwa chini ya Samuel Sitta!
Watu waliojitoa ufahamu na kumuona Magufuli kama Mungu wao kuanzia Makonda, Sabaya,Chalamila,Hapi ,Musiba, Kabudi na wengineo wengi leo Wanaishi kwa hofu sana!
 
wapo waliolalamikia pia awamu ya tano kuwatenga baada ya kukipigania chama na kumuingiza jamaa madarakani dhidi ya EL mwenye nguvu...

Haya malalamiko tumeyazoea huko CCM, mnapaswa kujifunza kila zama na kitabu chake...hata ile zama wapo walioteseka kama wewe tukawacheka na kuwakebehi na majina kedekede...
 
Mkichukulia haya mambo serious soon tutasikia mmeanzisha vikundi vya waasi na kuanza kutusumbua mapolini huko....."everyday is the school day"
 
Hajui alifanyalo, wanaofanya hivyo wanajua nini wanakitaka, wanatambua wazi kwamba wapiga kura wengi ni wafuasi wa JPM, kumtukana JPM wanawachonganisha wapiga kura na chama hivyo watu watapiga kura za asira kukiadhibu chama, yajayo yanafurahisha, nadhani hawatambui nguvu ya JPM.
 
Najua kuna wengine wengi mmepoteza kandarasi zenu na wengine ajira zenu...kuna yale magazeti, wasanii, na watu mitandaoni na.mitaani wote kandarasi haipo sasa....Badirisheni tu mfumo wa maisha mje mtaani huku tupige kazi kwa vitendo...aka kazi iendelee...
 
Nani kakwambia CCM inashinda kupitia box la kura?.....Hii nchi ni mali ya CCM na CCM inawajulia Watanzania...
Unasahau zile chaguzi za awamu ya Tano, hamkuona watu walivyodhulumiwa?, mbona hamkusimama na kuwatetea? yale mabox ya kura 2015 hamkuyaona?...
 
Ni mtanzania mwendawazimu tu ndo angemnyima kura JPM, hizi multiple accounts za wenye vyeti feki, mafisadi na wauza ngada sio the majority, walitukana sana then na wako wakitukana sasa ili kuwawin wapiga kura wa JPM wenye hasira na yanayoendelea sasa.
 
Haha, nguvu kutoka kaburini? Acha kujilisha ujinga, marehemu ashasahaulika, watu wanasonga mbele. Alikuwepo Nyerere, alikufa na watu wakamove forward, sembuse hilo fisadi lenu ambalo kakirusi kamafua tu kamemlaza futi 6 chini?
 
Pole ndugu, haupo peke yako unayeumizwa na huyu mama! Mama ni MSWAHILI WA TOWN! Anaongoza nchi kishikaji kwa kuangalia hadhira ya mtandaoni akidhani watanzania wote wako huko! Binafsi najishangaa ghafla nimepoteza hata hamu ya kufaatilia hotuba za Rais achilia mbali kuangali taarifa za habari TBC, maana kila anachofanya naona mama anapambana na Mwenda zake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…