Nimepata mateso makali ambayo sijawahi kuyapata tangu nizaliwe kwenye maisha yangu huu mwaka sitausahau kamwe katika maisha yangu yoote
CCM niliipenda bila kujali masilahi tangu nikiwa mtoto mdogo nilikuwa sijielewi nimeendelea kuipenda hata wakati wa dhoruba ya uchaguzi mkuu wa 2015 niliiamini sana CCM na Masada wake akina Nape, kinana, na wengine walituambia kuwa tutaleta CCM imara mgombea imara
Kweli Magufuli alishinda kwa mbinde sana lakini cha kushangaza kabisa walimgeuka
Makubwa yametokea baada ya msiba Mama ametugeuka kabisa hataki kutusikiliza ameziba masikio kabisa sisu tuliopiga kura ameanza kutuadhibu tena adhabu kali mimi binafsi nina maumivu makali sana jamani kiukweli naumizwa na Chama changu nilichokipenda kwa dhati
Mama Samia unatutesa sana sisi wapiga kura wa Chama cha mapinduzi wa enzi na enzi mama umeacha Hayati Magufuli anatukanwa ovyo wanaomtukana ndio unawasikiliza kumbe mama uko hivyo mama wanao sisi hautusikilizi tuliokipigania Chama bila malipo
Mama baba yetu ameondoka umetugeuka kumbe mama haukuwa na baba pamoja kwa nini mama unatufanyia hivi sasa wanao tumekukosea nini mama kwa kweli mama unafuata uongo unaozushwa mitandaoni ndo unaufanyia kazi kweli CCM mmenipa wakati wa mateso makali yasiyopimika