Yaani nilishasema wanaume tu ndiyo wanapendana lakini wanawake tunaoneana wivu wa kijinga sana.
Hii kauli ya Mbunge, tena mwanamke, kuhusu wafanyakazi wa ndege ATCL kuwa hawana mvuto na wafupi, huu ni wivu wa kuzodoa, kuwakejeli na kuwadhalilisha watoto wa kike wa mwanamke mwenzio au wanawake wenzio.
Wewe Hasna Mwilima, je wewe ni mrembo? Urembo wa mwanamke mwenzie unataka uufanyie nini?
Au unataka hao wanawake waachishwe kazi wakafanye kazi gani? Mpaka hapo umeisha poteza sifa za kuwa Mbunge, umewadhalalisha sana wanawake wa Tanzania.
Natamani niwafahamu watoto wako wa kike, nione urembo walio nao, wanawake tuna mambo ya ajabu sana, ambayo hata shetani ameshindwa kutudefine.
Nilitegemea kauli kama hii ingetolewa na Mbunge viti maalumu, kumbe tena Mbunge mwenye jimbo aliyepigiwa kura na kila aina ya mwanamke, wafupi, warefu, rangi tofauti tofauti, leo unawadhalalisha kiasi hiki.
Ufupi wa mwanamke si ulemavu wa kushindwa kufanya kazi, au hizo ndege ni madanguro? Inabidi tufahamishwe kazi ya ziada wafanyao hao wanawake.