CCM MP has said that ATCL air hostesses are not attractive

CCM MP has said that ATCL air hostesses are not attractive

Hata mimi sijapenda kauli yake ni kali sana na imewaathiri walengwa vilivyo,
Tukiangalia kwa jicho la tatu kwani hasa vigezo vya Air Hostess ni vipi?
 
Yaani nilishasema wanaume tu ndiyo wanapendana lakini wanawake tunaoneana wivu wa kijinga sana.

Hii kauli ya Mbunge, tena mwanamke, kuhusu wafanyakazi wa ndege ATCL kuwa hawana mvuto na wafupi, huu ni wivu wa kuzodoa, kuwakejeli na kuwadhalilisha watoto wa kike wa mwanamke mwenzio au wanawake wenzio.

Wewe Hasna Mwilima, je wewe ni mrembo? Urembo wa mwanamke mwenzie unataka uufanyie nini?

Au unataka hao wanawake waachishwe kazi wakafanye kazi gani? Mpaka hapo umeisha poteza sifa za kuwa Mbunge, umewadhalalisha sana wanawake wa Tanzania.

Natamani niwafahamu watoto wako wa kike, nione urembo walio nao, wanawake tuna mambo ya ajabu sana, ambayo hata shetani ameshindwa kutudefine.

Nilitegemea kauli kama hii ingetolewa na Mbunge viti maalumu, kumbe tena Mbunge mwenye jimbo aliyepigiwa kura na kila aina ya mwanamke, wafupi, warefu, rangi tofauti tofauti, leo unawadhalalisha kiasi hiki.

Ufupi wa mwanamke si ulemavu wa kushindwa kufanya kazi, au hizo ndege ni madanguro? Inabidi tufahamishwe kazi ya ziada wafanyao hao wanawake.
Acheni kuendekeza kauli za kujenga chuki, ni kweli alichokiongea kakosea, lakini we unaamini kilichompelekea aongee alichokiongea ni jinsia yake au tabia na akili zake? Au hujawahi kushuhudia mwanaume akizungumza maneno ya ajabu juu ya mwanamke, au hata juu ya mwanaume mwenzie na hakuna anayehusisha maoni yake na jinsia yake why women? Anza kujiuliza ni kweli wewe ni adui wa mwanamke mwenzio? kama kweli badilika
 
Hutakuja kunisikia nikisema mwanamke huyu ni mbaya huyu ni mzuri kwa kuwa hawakujiumba wao. Kwani nikosoe kitu kilicho nje ya uwezo wao kurekebisha.

Neno langu kwa huyo mbunge kilaza (wote tunazaliwa tukiwa wajinga ila baadhi yetu hupambana kwa bidii sana wabaki kwenye ujinga) uzuri unaweza ukaondoka ndani nusu dakika tu. Shukuru Mungu kwa jinsi ulivyo leo maana hujui kesho yako.
 
Huyu hata kibiashara kaiharibia ATCL yetu, Hawa watu wanakula kodi zetu DODOMA wamekaa tuu hawajui ugumu wa kutafuta masoko. Sisi tunapambana kubrand shirika yeye analeta masihala. CCM huyu mama mwakani wamuweke Pembeni kwa dharau izi hata fomu yake isiingie vikao vya awali kujadiliwa
 
Kweli mkuu, siwezi kumnyooshea kidole mtu kwa sura yake, mimi ni nani?
Hutakuja kunisikia nikisema mwanamke huyu ni mbaya huyu ni mzuri kwa kuwa hawakujiumba wao. Kwani nikosoe kitu kilicho nje ya uwezo wao kurekebisha.

Neno langu kwa huyo mbunge kilaza (wote tunazaliwa tukiwa wajinga ila baadhi yetu hupambana kwa bidii sana wabaki kwenye ujinga) uzuri unaweza ukaondoka ndani nusu dakika tu. Shukuru Mungu kwa jinsi ulivyo leo maana hujui kesho yako.
 
Kuhujumu uchumi sio tu kuiba hela bali pia kauli mbaya za kiongozi juu ya mali na uduma za umma ili zionekane hazifai ili zikataliwe na wateja nayo ni hujuma na mtuhumiwa anatakiwa akashitakiwe katika mahakama ya mafisadi.

Huyo ni kibaraka wa mabeberu! Mbunge wa Kigoma Husna Mwilima kwa kauli za kuwatukana mabinti zetu (air hostess) kuwa ni wabaya ni kulihujumu ATCL na kuhujumu juhudi za Rais wetu kulifufua ATCL ambayo kimsingi ilikuwa imekufa.

Kama Mbunge ana nafasi kubwa ya kuongea na viongozi husika kama waziri wa usafiri, utalii, mkurugenzi wa ATCL na kutoa maoni yake kuliko kwenda public na kuutangazia dunia kuwa huduma za ATCL ni mbaya.

Huu ni uhujumu uchumi wa nchi.
 
Ondoa uchama mkuu tujadili utu aliuzalilisha
Huyu hata kibiashara kaiharibia ATCL yetu, Hawa watu wanakula kodi zetu DODOMA wamekaa tuu hawajui ugumu wa kutafuta masoko. Sisi tunapambana kubrand shirika yeye analeta masihala. CCM huyu mama mwakani wamuweke Pembeni kwa dharau izi hata fomu yake isiingie vikao vya awali kujadiliwa
 
Wa kuonya kwa nguvu zote
Haya ndo matatizo ya kauli "mwanamke akiwezeshwa anaweza". Mwanamke mwenye akili ni yule anayepambana kama wanaume wanavyopambana na ukimkuta mwanamke aliyetoboa kwa kupambana na sio kuwezeshwa au kupewa nafasi za upendeleo anakuwa na akili kichwani. Mianamike ya dizaini ya Hasina Mwilima yanatia kinyaa hata tukikutana nayo katika ofisi za umma
 
Huyu inabidi aiangalie kwanza yeye anasura nzuri? Ile ni kazi kama kazi zingine tungekuwa tunaangalia sura asingepata ubunge huyu mwanamke
 
hakuna cha uadui wa nani nani? kasema ya kweli wale wahudumu wengi si warembo na mawigi yao kama kiota

shida kalisema wazi na bila busara (kalopoka) ila ni kweli 100% mambo ya uwajue watoto wake uone kama ni warembo hayana maana (maana sio wahudumu wa ndege, wale ndo tunataka wawe warembo) hata kuuliza yeye ni mrembo haina maana kwa sababu si muhudumu wa ndege.

chagueni watu kwa kufata sifa, acheni kubebana ndo madhara haya muhumudumi kakomaa ka mwana masumbwi
Aliyekudnganya wahudumu wa ndege wanatakiwa kuwa warembo ni nani? Umewahi kupanda japo ndege?
 
Binafsi naunga mkono hoja iliyowasilishwa na mheshimiwa mbunge ifike mahala biashara ifanywe serious huwezi kuweka watu ambao hawana sifa stahiki kwa kigezo cha udhalilishaji kuna mambo mengi yanawezwa kufanywa hapo ATCL na hao kina dada ikumbukwe Air hosters wapo pale kama wawakilishi wa urembo wa dada zetu hapa Nchini kwa hiyo iwekwe wazi tu kua wanatakiwa kua warembo msilete unafiki hapa
 
huyu inabidi aiangalie kwanza yeye anasura nzuri? ile ni kazi kama kazi zingine tungekuwa tunaangalia sura asingepata ubunge huyu mwanamke
Yeye sio Air hoster mkuu kwa hiyo urembo wake hauhusiani na mada tajwa hapa
 
Mnazingua tu...hamueeki hiyo video.
 
"Urembo wa mwanamke mwenzio unataka uufanyie nini?" Cutelove
 
Back
Top Bottom