CCM msipombadilisha Rais Samia, Tanzania inaenda kusambaratika ndani ya Uongozi wake

Dr.Ulimboka!mwembe chai
Ulimboka haikuwa nzuri lakini ilikuwa kama tukio moja, la Mwembe Chai inategemeana upo upande gani na lipo ya Bucha za Nguruwe au nini na sababu zake ni zipi ukilinganisha na hili la maneno Tu
 
Wenyewe ndio wanapoteza, huyo mnaye mlaumu katiba inasema ni alama tu ya taasisi, jiulize watawala ni kina nani?
Ni yeye..

Na inaelekea hata hujui kuwa Rais wa nchi ndiye kamungu na kameenea kila mahali, juu huko hadi chini huku..

Au hujui kuwa Rais ndiye;
1. Mkuu wa serikali?
2. Mkuu wa nchi? na;
3. Amiri Jeshi mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi na usalama?

Sasa kama, ame surrender haya mamlaka kwa watu wengine, ni ujinga na upumbavu wake. Na huu ndio tunaousema kuwa ni UDHAIFU na MAKOSA yake yanayom - disqualify moja kwa moja kuwa Rais wa nchi hata kwa miezi miwili tu ijayo..!

Alivyo huyu mama (kwa mantiki yako), tunaweza kumlinganisha na Baba mwenye nyumba mwenye hadhi ya "Kichwa cha Familia" aliyopewa na Mungu, ambaye kanyang'anywa mamlaka yake ya uongozi wa familia na mtoto wake wa kuzaa..

Unaonaje akiulizwa na Mungu aliyempa mamlaka hayo, mbona hutendi wajibu wako wa kimamlaka halafu utetezi wake uwe "si ni huyu mtoto uliyenipa kachukua nafasi yangu!". Unadhani reaction ya mtoa mamlaka hayo itakuwaje? Atamfanya nini?

Bila shaka ni kumtoa kwenye nafasi hiyo na kumpa mwingine!

KWA HIYO: Ktk scenario hii, Bi Samia na u - Chura Kiziwi chake, atawajibika yeye na kila ubaya, sisi hatumjui mwingine.

Na kwa kweli, as it is for now, SHE HAS BEEN REJECTED hawezi kwenda popote!
 
Kabisa nchi imemshinda na pumzi inakata No Reforms no election
 
kwahiyo kumbe tatizo lenu ni samia wala sio mageuzi ya tume ya uchaguzi?
 
Sisi tunasema huko CCM hakuna mwingine anayekubalika zaidi ya Samia,maana watu wamemchoka
Mbona Magufuri kalibu kila mtu alimpenda na hakutumia nguvu kulamisha watu wampende
nyie sindomlisema maguful ni dictator akina saanane walipotea kipindi kipi?
 
VIJANA wakishiba sana pia tatizo wanalala na ndoto zao walizowaza mchana au kuongea sana iyo siku !!

kila siku wanakuja na Story za kuwafurahisha na maono ndoto sio ajabu kijana mwengine akaja na kutwambia Lisu Tayali ndio Rais amemuona akikagua gwaride Uwanja wa Uhuru!!!!!

Utoto sio ugonjwa wakikuwa Wataelewa CCM ni alfa na umega awa awa watoto wanaokichafua umu leo baada ya miaka 30 watakua CCM kindaki ndaki!!!

leo wanasaau kama kususiwa CCM washasusiwa na akuna chochote Wasusajii walipata !!!

CCM wamejipanga kias akuna Upinzani wa aina yoyote utawasumbua utanipuuza lkn utaelewa uko mbele kwann nimeandika ivi ukubwa dawa!!!

Lisu anateseka bure akuna chochote Upinzani utanufaika kwa yeye kukaa ndani kipindi ichi!!!

kimsingi Upinzani umejivua nguo wenyewe kwa kukubali kipind cha Rais JPM RIP kuamia CCM kutoka Upinzani walipokuwa kile kitendo kimeuwa nguvu energy ya Vijana wengi Tanzania !!!

Mfano Mbeya vijana wengi wamekasilika na wameamia CCM !!

nina rafiki zangu walikuwa CHADEMA na ndio walikuwa wanalinda kula usiku na mchana apo Mbeya !!!

wengi leo wamajisajili CCM yani CCM Mbeya aijawai sajili vijana wengi kama kipindi ichi !!!

waliokuwa wanasupport Upinzani nchi kote fikiria vijana walikesha vituoni kulinda kula siku adi 7 afu Mgombea anaamia CCM !!!

ndiomana ata Vijana wakuandamana kwasasa akuna waliobaki awa watoto wenyekuota Usiku asubui mbio kuja kuanzisha UZI !!!!

ukweli Upinzani itawachukua miaka 20 au 25 ijayo japo wapate Support ya Wananchi kama ile ilikuwa kabla ya Rais JPM RIP !!!!

narudia Lisu kukaa kwake ndanI ni kujitesa tu akuna mavuna yoyote yatapatikana !!

tofaut na arakat zake izi angefanya baada ya miaka 25 uko mbele pengine angepata Support kubwa ya wananchi vuguvugu lingekuwa kubwa kuliko sasaivi !!!

kwasasa Upinzani upo ICU ujumbe huuu ni kwaajili ya watu wenye umri kwanzia miaka 30 to 80 ndio wataelewa kwann Upinzani upo ICU !!!

kelele za Chedema No + No zitaisha wkt Kampeni zikianza CCM itajaza watu kwenye mikutano yao kias No + No itayayuka kama barafu kwenye maji ya Moto.!!!

Mwisho vijana punguzeni kuwatukana wakubwa wenu !!!

kampeni zikianza ndio mtajua mkubwa ni mkubwa na CCM ni Alfa na Omega
 
Asante kwa kushiriki maoni yako.
Hili ni suala nyeti linalogusa uongozi, haki, demokrasia, dini, na mustakabali wa taifa. Na kwa sababu hiyo nakiri dhahiri kuwa hii mada nzito, hoja zako zitajibiwa kwa utulivu, hoja za msingi, na uhalisia si kwa jazba, si kwa ushabiki.

🟡 1. Kuhusu Hoja ya Rais Samia "Kutokubalika"

Ni kweli kuwa hakuna kiongozi atakayekubalika na kila mtu, na hiyo ni hali ya kawaida katika demokrasia yoyote. Hata hivyo:

Dkt. Samia alichukua madaraka kihalali kama Makamu wa Rais kufuatia kifungu cha Katiba (Ibara ya 37(5)) baada ya kifo cha Rais Magufuli.

Katika uchaguzi wa 2020, CCM (ambayo yeye sasa anaiongoza) ilishinda kwa kura nyingi, ingawa kulikuwa na shutuma nyingi kutoka kwa upinzani kuhusu uhuru na haki ya uchaguzi huo.

Katika uongozi wake, kuna hatua za kurudisha hali ya mazungumzo ya kisiasa, kama alivyoanzisha Jukwaa la Maridhiano, akakutana na wapinzani (akiwemo Tundu Lissu), na akaanza mchakato wa marekebisho ya sheria.


👉🏽 Hoja muhimu hapa ni: Samia hakujichagulia kuwa Rais. Mfumo wa kikatiba ulimweka hapo, na chama kilichompa ridhaa bado kina nguvu kihalali kwa sasa.

🟡 2. Kuhusu Kutekwa, Mauaji, na Haki

Kumekuwa na ripoti kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu, watu kutoweka, na kukamatwa kwa wakosoaji. Ni hoja nzito, na serikali imekuwa ikikanusha au kutoa majibu ya taratibu, ingawa wengi hawaamini.

Mfano: Sakata la Joseph Mbilinyi (Sugu), Freeman Mbowe, na hata Lissu ni matukio yaliyotikisa imani kwa baadhi ya taasisi.

Gwajima alitoa shutuma bungeni, lakini hadi sasa hakuna uthibitisho wa kisheria dhidi yake, na bado ni Mbunge.

Kama wananchi hawaridhiki, mfumo wa haki upo (mahakama, Tume ya Haki za Binadamu, mashirika ya kiraia), ingawa ufanisi wake unazidi kuhojiwa.


👉🏽 Badala ya kuchochea hofu ya "inchi kulipuka", ni muhimu kutafuta mabadiliko kupitia njia za kidemokrasia – si kwa jazba, bali kwa nguvu ya hoja, kura, na shinikizo la kisheria.


🟡 3. Kuhusu Tume Huru ya Uchaguzi

Hili ni hitaji halali, na tayari:

Serikali imepitisha Mswada wa Marekebisho ya Tume ya Uchaguzi, ambao unalenga kuifanya iwe na uhuru zaidi.

Wapinzani wamesema bado haitoshi hoja yao ina msingi, lakini huwezi kupuuza kwamba hili ndilo jambo ambalo awamu ya Samia imelianza.


👉🏽 Kama kweli dhamira ni uchaguzi huru, basi hoja ifanyiwe kazi kwa mjadala wa kitaifa na si matusi au vurugu.

🟡 4. Kuhusu "Uzanzibar" na "Uanamke" wa Rais

Hii ni hatari sana:

Kumhukumu Rais kwa asili ya kuzaliwa (Uzanzibari) au jinsia (Mwanamke) ni ubaguzi na ni kinyume kabisa na misingi ya katiba ya Tanzania.

Uraia wake, jinsia yake, au dini yake havinyimi uhalali wa uongozi.

Tukiingiza hoja za asili au imani, tunajenga chuki, si hoja.


👉🏽 Mwananchi yeyote anaweza kumkosoa Rais, lakini si kwa misingi ya chuki ya kijinsia au kikabila bali kwa misingi ya sera, utekelezaji, na misimamo ya kisera.


🟡 5. Je, CCM Itashindwa au Tanzania Itavurugika?

Hili ni tishio lisilo la lazima.

Tanzania imevuka vipindi vigumu – uchaguzi wa 1995, 2015, 2020 – na bado imebakia kuwa miongoni mwa nchi za amani barani Afrika.

Ndiyo, kuna changamoto za kisiasa. Lakini njia ya kuzitatua si kutabiri vita, maangamizi, au mfarakano wa kidini.

Hatuwezi kukubali wanasiasa wachache au hoja za chuki kuteka ajenda ya taifa zima.


✅ Hitimisho la Hoja:

Una haki ya kutoa maoni. Lakini ni muhimu tujiulize:

Je, tunapinga mfumo kwa hoja au kwa hisia?

Je, tunajenga hoja zinazojenga au tunatoa matamshi yanayochochea hofu?

Je, tukisema "inchi italipuka" si tunakaribisha vurugu badala ya kuizuia?


Demokrasia ni kazi ya pamoja. Tusiihatarishe kwa jazba. Tuitetee kwa hoja, busara, na mwisho kabisa twende tukapige kura.
 
Acha kuni mention kwenye pumba muda wa kusoma hilo gazeti haupo
Stupid, usiwe mentioned wewe ni nani?

Hutaki kuwa mentioned, acha kuposti ujinga wako humu, potea na usionekane tena humu na hakuna mtu wa kukufuata nyumbani kwako au kwenye vyumba vyenu vichafu vya Lumumba..!!

Kama hutaki kutoka humu, basi nakutaka ujibu swali hili👇🏻👇🏻👇🏻👇🏻 haraka na sasa hivi:

Matokeo ya kura za Urais wa Magufuli na sasa Chura Kiziwi uchaguzi mkuu 2020 jimbo kwa jimbo yako wapi? Kwanini NEC haijayatangaza kwenye platforms za serikali ikiwemo tovuti ya Tume yenyewe kama sheria inavyotaka kuwa ndani ya miezi mitatu mara baada ya mshindi wa Urais kutangazwa, Tume ya Uchaguzi itapaswa kutangaza matokeo ya kura za uchaguzi wa Rais Jimbo kwa jimbo katika gazeti la serikali na ktk tovuti ya Tume?

Unajua hili kweli wewe? Au ni mbwa mnaoambiwa na mabwana zenu mbweke tu kama vichaa?
 
Wakati nikikubaliana na mengi uliyo andika kwenye mada yako, kamwe sikubaliani na mengine, hasa kama kichwa cha mada kilivyokaa:
"CCM msipombadilisha rais samia Tanzania inaenda kusambaratika ndani ya uongozi wake".

Sikubaliani kabisa na wazo la Tanzania KUSAMBARATIKA, kwa sababu tu ya kiongozi mbovu kabisa kama Samia Suluhu Hassan.
Hata CCM yenyewe tu, kama chama, wasipokuwa wajinga haitasambaratika kwa sababu tu ya kuwa na Mwenyekiti mbovu kama huyu mama.
WaTanzania hatuna hulka ya kusambaratika kwa mambo madogo kama haya.
Huyu Samia na Genge lake watawekwa pembeni, na nchi yetu itaendelea mbele, tena kwa mshikamano madhubuti zaidi.
 
Wewe una akili kama za kenge 100%

Shika na liweke hili 👇🏻👇🏻 kichwani mwako

NO REFORMS NO ELECTION 2025 OR FOREVER!!
 
Kuwa makini kutukanatukana watu mtandaoni utakuja kumtukana kibenten wa mamaako
 
👉🏽 Hoja muhimu hapa ni: Samia hakujichagulia kuwa Rais. Mfumo wa kikatiba ulimweka hapo, na chama kilichompa ridhaa bado kina nguvu kihalali kwa sasa.
Chama kipi "kimempa ridhaa". Kwa utaratibu upi? CCM ina nguvu kihalali kwa sasa? Unazungumzia CCM ipi; inayo tumiwa jina lake na Genge linalomshikilia Samia, au CCM ipi?
 
Uko sawa kabisa watanzania bado wamelala fofo
Labda wewe ni mgeni Tanzania hii, ila sisi wenyeji hatujawahi kuona watanzania wakiishinda serikali, nitasubiri nione, na hili likitokea nahama nchi.

Watanzani hawa hawa wanaoogopa mabomu ya machozi au watanzania gani unaowaongelea wewe?
Waingereza wana msemo wao kwamba "there is more than one way of skinning a cat."
 
Hapa umewasemea watu Ukiwa kiongozi huwezi kupendwa na watu wote na huwezi kuchukiwa na watu wote
 
CCM wanajitanya hawana AKILI TIMAMU,Mashehe wenye Akili TIMAMU wameongea kuhusu HAKI,Maaskofu ,mapadri ,wachungaji wote wenye Akili TIMAMU wameongea,sasa tunasubiri nani aongee,maana wakati mwingine waswahili wanasema sikio la kufa halisikii dawa.
 
Hatuwezi kukubali wanasiasa wachache au hoja za chuki kuteka ajenda ya taifa zima.
Kwa maana hiyo, unatuhimiza waTanzania tukubali siasa za "utekaji, upoteaji wa watu na kuuawa watu" kwa sababu za kisasa? Kwa nini kati yenu hili jambo ni kama halipo kabisa?
Kama wew huoni kuwa watu kupotea,kutekwa,kuuawa "siyo ajenda muhimu ya taifa", ni ajenda gani inayokustua wewe: Samia Kufurumushwa kwa nguvu toka ikulu?
Ndiyo, kuna changamoto za kisiasa. Lakini njia ya kuzitatua si kutabiri vita, maangamizi, au mfarakano wa kidini.
Unajuwa wazi kabisa, njia bora kabisa za kuzitatua hizo unazoziita changamoto ni rahisi kabisa: Fanya marekebisho husika, ili uchaguzi ufanyike katika mazingira tulivu, HURU na ya HAKI, ili waTanzania wakawachague viongozi wao kwa uhuru kabisa, bila ya mizengwe yoyote.
Hilo ndilo suluhisho msilolitaka, na hamuelezi kwa nini hamlitaki.
 
Kikwete alijitahidi sana kuishi na kila aina ya wakosoaji. Pongezi kwake
 
Gentleman,
peleka hiyo ramli na ushirikina wako nonsense kabisa kwenye chama na familia yako gentleman
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…