🟡 1. Kuhusu Hoja ya Rais Samia "Kutokubalika"
Ni kweli kuwa hakuna kiongozi atakayekubalika na kila mtu, na hiyo ni hali ya kawaida katika demokrasia yoyote. Hata hivyo:
Dkt. Samia alichukua madaraka kihalali kama Makamu wa Rais kufuatia kifungu cha Katiba (Ibara ya 37(5)) baada ya kifo cha Rais Magufuli.
Katika uchaguzi wa 2020, CCM (ambayo yeye sasa anaiongoza) ilishinda kwa kura nyingi, ingawa kulikuwa na shutuma nyingi kutoka kwa upinzani kuhusu uhuru na haki ya uchaguzi huo.
Kwani kuna anayepinga hili? Ni kweli alichukua madaraka ya Urais kwa mujibu wa katiba
Ni katiba tu iliyompa uhalali na haki hiyo. Otherwise, John P. Magufuli asingekufa huyu asingeweza kuwa Rais either by hooks or by crooks baada ya huyu kutokana sifa hizihizi zinazotajwa katika mijadala, i .e kutokuwa na uwezo wa kushika nafasi ya juu kama hii (justified already), uanamke wake, uzanzibari wake na zingine lukuki...
Lakini kiuhalisia, kwa ushahidi wa kimazingira sasa na kwa sbb hizi, hakubaliki na zaidi ya Watanganyika 95%. Aende huko kwao Zanzibar, Tanganyika hstumhitaji tena..
Katika uongozi wake, kuna hatua za kurudisha hali ya mazungumzo ya kisiasa, kama alivyoanzisha Jukwaa la Maridhiano, akakutana na wapinzani (akiwemo Tundu Lissu), na akaanza mchakato wa marekebisho ya sheria.
Ulikuwa ni ulaghai. Hata haifai na hupaswi kuturejesha huko tena.
Where are her 4Rs? Anajaribu hata kuzisema sasa? Mnaweza kuzitetea?
One of 4Rs is "REFORMS". Why is she afraid of true and fair reforms kwa kwenda kwenye msingi wa kila tatizo, KATIBA..??
That was purely political scams na ndiyo inayomshushia heshima na hadhi yake. Ni aibu kwa Rais (malkia/mfalme) kuwa mwongo, scammer...!
🟡 2. Kuhusu Kutekwa, Mauaji, na Haki
Kumekuwa na ripoti kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu, watu kutoweka, na kukamatwa kwa wakosoaji. Ni hoja nzito, na serikali imekuwa ikikanusha au kutoa majibu ya taratibu, ingawa wengi hawaamini.
Majibu gani serikali imetoa? Kufunga kanisa la Josephat Gwajima kipuuzi tu? Really?
Mfano: Sakata la Joseph Mbilinyi (Sugu), Freeman Mbowe, na hata Lissu ni matukio yaliyotikisa imani kwa baadhi ya taasisi.
Sema yame - cement msimamo wa wananchi KUTOIAMINI SERIKALI na vyombo vyake. Ndiyo maana tunahitaji REFORMS za kisheria na kikatiba ili tuanze kwa kupata viongozi waadilifu kupitia chaguzi zilizo huru, wazi na haki. Kwa njia, tutabadilisha mfumo mzima wa kisiasa na utawala na ndilo suluhisho la kurudisha imani ya wananchi kwa nchi yao na serikali zao zitakazowaongoza. Hatuwezi kuendelea kuongozwa na viongozi wanaojiweka kwa nguvu madarakani na kutulazimisha tuwaamini tu. HAIWEZEKANI...!
Gwajima alitoa shutuma bungeni, lakini hadi sasa hakuna uthibitisho wa kisheria dhidi yake, na bado ni Mbunge.
What exactly do yo mean here? Je, una maana ya shutuma za kutekwa watu na mauaji ya raia wasio na hatia bila utaratibu wa kisheria kufuatwa? Na hili nyie serikali mnajifanya hamjui na mnataka ushahidi?
Kumbe, kwa ujinga huu, NI HALALI MTUKANWE NA MZOMEWE kwa sababu mnatufanya wananchi ni wajinga na wapumbavu kama nyie viongozi mlivyo!!
Kama wananchi hawaridhiki, mfumo wa haki upo (mahakama, Tume ya Haki za Binadamu, mashirika ya kiraia), ingawa ufanisi wake unazidi kuhojiwa.
Sio kuhojiwa tu. The whole system is completely rotten and it has to be overhauled. Ndiyo maana ya NO REFORMS NO ELECTION. Na reforms hizi, msingi wake ni katiba!
👉🏽 Badala ya kuchochea hofu ya "inchi kulipuka", ni muhimu kutafuta mabadiliko kupitia njia za kidemokrasia – si kwa jazba, bali kwa nguvu ya hoja, kura, na shinikizo la kisheria.
Samia na serikali yake hawataki. Wanajaribu kuwatia hasira wananchi waende kwenye njia za shari.
Mfano: Wewe unafikirije kuhusu kampeni ya CHADEMA ya NO REFORMS NO ELECTION? Ni kampeni ya kishari au ya kidemokrasia ya kudai mabadiliko?
Honestly speaking, hii kampeni ni wito wa kidemokrasia 100% wa kudai mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi Tanzania. Bahati mbaya ni kuwa CCM na serikali kwa ujinga wao, wanafanya kila njia kui - criminalize kampeni hii ili ife na wao waendelee kupata upendeleo wasiostahili kuwa nao!
🟡 3. Kuhusu Tume Huru ya Uchaguzi
Hili ni hitaji halali, na tayari:
Serikali imepitisha Mswada wa Marekebisho ya Tume ya Uchaguzi, ambao unalenga kuifanya iwe na uhuru zaidi.
Huwezi kuwa na sheria ya Tume huru ya uchaguzi bila kufanya kwanza mabadiliko ya kikatiba
Tume huru ya uchaguzi ni takwa la kikatiba na sio la kisheria tu.
It's Constitutional amendments first, then sheria. Je, wamefanya hivyo? Hapana. Bali wametanguliza mkokoteni mbele ya punda.
Hili nalo ni gumu kueleweka kwako?
Wapinzani wamesema bado haitoshi hoja yao ina msingi, lakini huwezi kupuuza kwamba hili ndilo jambo ambalo awamu ya Samia imelianza.
Hawajaanza. In fact hawajafanya lolote.
Uthibitisho ni uchaguzi wa mitaa na vijiji mwaka jana 2024.
👉🏽 Kama kweli dhamira ni uchaguzi huru, basi hoja ifanyiwe kazi kwa mjadala wa kitaifa na si matusi au vurugu.
Anayekataa hoja ya msingi na ya kweli kwa kuikimbia, kimsingI ndiye atakaye matusi na vurugu zimpate. Unadhani ni nani hao?
🟡 4. Kuhusu "Uzanzibar" na "Uanamke" wa Rais
Hii ni hatari sana:
Kumhukumu Rais kwa asili ya kuzaliwa (Uzanzibari) au jinsia (Mwanamke) ni ubaguzi na ni kinyume kabisa na misingi ya katiba ya Tanzania.
Uraia wake, jinsia yake, au dini yake havinyimi uhalali wa uongozi.
Tukiingiza hoja za asili au imani, tunajenga chuki, si hoja.
👉🏽 Mwananchi yeyote anaweza kumkosoa Rais, lakini si kwa misingi ya chuki ya kijinsia au kikabila bali kwa misingi ya sera, utekelezaji, na misimamo ya kisera.
Haya ni mazao ya kuukataa ukweli na kulazimishwa uongo wao uwe ukweli..
Wametulazimisha wananchi tuingie kuhoji na kushambulia maeneo ambayo hayakupaswa tufike huko kwa sbb ya ugumu wa mioyo yao..
Inafikia wakati mtu anajiuliza, labda Rais huyu anafanya haya kwa sbb yeye ni Mzanzibari na ni mwanamke..
Waambie CCM wasipambane na hitaji la wakati. ELECTORAL SYSTEM REFORMS
🟡 5. Je, CCM Itashindwa au Tanzania Itavurugika?
Hili ni tishio lisilo la lazima.
Ni tishio halisi na la lazima wasipotumia akili ktk kufanya maamuzi yao.
Wana dhamana hiyo ya kulinda amani ya nchi lakini si kwa njia na namna wanavyofanya.
Njia wanayotumia ni kuwapa majina mabaya wanaodai mabadiliko ili wapate sababu ya kuwashughulikia sawa na msemo wa "mpe mbwa jina baya ili umuue"
Hii sio njia ya kulinda amani na utulivu. Hii ni njia ya kuongeza tatizo na kuvuruga hiyo amani na utulivu!!
CCM na serikali yao waukubali ukweli unaowakodolea macho kodo. Kuukwepa na kuukimbia, ni ujinga na ujinga unapelekaga watu mashimoni na makaburini!
Tanzania imevuka vipindi vigumu – uchaguzi wa 1995, 2015, 2020 – na bado imebakia kuwa miongoni mwa nchi za amani barani Afrika.
It doesn't matter..
Sio kila siku ni Jumapili..
That was the past..
Hizi ni nyakati na majira mengine tofauti kabisa..
Hitaji la nyakati hizi MABADILIKO YA KWELI YA MIFUMO YETU YA KUSIMAMIA CHAGUZI ZETU.
Otherwise, NO REFORMS NO ELECTION itawazoa wengi sana..
Ndiyo, kuna changamoto za kisiasa. Lakini njia ya kuzitatua si kutabiri vita, maangamizi, au mfarakano wa kidini.
Hatuwezi kukubali wanasiasa wachache au hoja za chuki kuteka ajenda ya taifa zima.
Huwezi kulikwepa hili iwapo maisha yako ni kudhulumu haki za wengine..!
Tabia ya kupuuza na kudhulumu haki za watu iki persist ktk jamii, wanaodhulumiwa hutafuta njia ya kukataa kuonewa na kudhulumiwa na hivyo kuanzisha mapambano ya kujikomboa..
Ndiyo. Katika mapambano yoyote kuna kupata na kupoteza hata maisha. Lakini hii ni kwa pande zote. Msifikiri nyie mnaodhulumu haki za watu mtaua mnaowadhulumu tu. Hata nyie mtakufa kwa wingi pia..!
Swali linapaswa kuwa; Kwanini tufike huko? Sababu ni nini?
Jibu ni rahisi sana. Tunaweza kufika huko kwa tamaa ya walionacho visivyo halali yao kung'ang'ania kusema kuwa ni vyao tu na kutotaka hata kugawana nusu kwa nusu. Hii ndiyo tabia ya CCM na hawa ndio wavuruga amani na utulivu..
Tell them to make the right decisions before it's too late...
Wakitaka vita, itakuja na wataumia wao, watapoteza wao big time. Maana wanyonge walionewa ktk taifa hili kwa miaka mingi hawapigani wao bali mkono wa Mungu Jehovah (Mungu wa HAKI achukiaye dhuluma) anapigana upande wao, upande wa HAKI..!!
✅ Hitimisho la Hoja:
Una haki ya kutoa maoni. Lakini ni muhimu tujiulize:
Je, tunapinga mfumo kwa hoja au kwa hisia?
Absolutely..
Kama huzioni hoja za NO REFORMS NO ELECTION, basi wewe ni kipofu wa uelewa na ufahamu..!!
Je, tunajenga hoja zinazojenga au tunatoa matamshi yanayochochea hofu?
Waulize CCM hili swali.
Wao hata hawana hoja kabisa..
Hawatoi hoja zozote, bali wanatumia nguvu kutoa hoja zao na kisha kufanya maamuzi ya hovyo, ya kijinga na kipumbavu ambayo in real sense yanayochochea vurugu..
Hebu fikiri kidogo kwa kutumia akili yako vizuri. Tundu Lissu ana kosa gani la kisheria hata kumweka kizuizini? Kwa sababu anadai mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi? Na Askofu & Mchungaji Josephat Gwajima ana kosa gani hata hatua za hovyo kuchukuliwa dhidi ya kufuta usajili wa kanisa lote? Je, ni kwa sbb tu ameikosoa CCM na serikali yake kwa namna isivyo serious kushughulikia ishu ya utekaji na mauaji ya raia wasio na hatia na kutoa picha kuwa kuna possibility kuwa mauaji haya yanafanya na kufadhiliwa na baadhi ya wanasiasa wakubwa walioko CCM na serikalini?
Busara ya kawaida ilikuwa kufanyia kazi ushauri au kumsaka na kutaka kumdhuru mtoa ushauri hata kukomoa raia wasio na hatia kwa kuingilia na kuvunja haki yao ya kuabudu?
Hebu kama una akili kweli, tujibu maswali haya...
Je, tukisema "inchi italipuka" si tunakaribisha vurugu badala ya kuizuia?
Tunaposema "nchi italipuka" huwa kauli ya tahadhari au onyo. Na mara zote kauli hii huenda sambamba na condition "iwapo Rais Samia hawatakuwa/wataendelea kupuuza mawazo na ushauri wa wananchi"
Kwa hiyo, ndugu
Tamimu fuad, hii nchi Italipuka kwelikweli kama viongozi nyie huko mtaendelea kuweka akili na hekima yenu kwenye mifuko ya suruali zenu nyuma badala ya kuzitumia kufanya maamuzi sahihi...
Tatizo letu mnataka kuwa na vyote, hamtaki kugawana na wengine nusu kwa nusu. Hiyo haifai, na itawa cost..
Watakaoilipua nchi hii si
Demokrasia ni kazi ya pamoja.
Exactly, I totally agree with you..
Kama ni ya pamoja, kwanini hamuitaki? Kwanini hamtaki twende pamoja? Kama ktk 4Rs za Rais Samia kuna ya REFORMS, kwanini hamtaki kwenda kwenye true & genuine RECONCILIATION itakayotupeleka kwenye true & genuine constitutional REFORMS na kisha tuende kwenye Rebuilding our country and social relationship?
Unaweza kujibu maswali hayo ☝🏻☝🏻⁉
Tusiihatarishe kwa jazba. Tuitetee kwa hoja, busara, na mwisho kabisa twende tukapige kura
Hakuna jazba hapa ndugu
Tamimu fuad...
Hoja za NO REFORMS NO ELECTION ziko mezani kwenu...
Tunajua hazina majibu nje ya kwamba, constitutional reforms zitakazoleta electoral system reforms Tanzania ni za lazima..
Tatizo lenu mnazikimbia na badala yake mnatumia ubabe wa marungu, bunduki na mahakama kuwajibu watoa hoja..!
This is completely sanity (uchizi)!!
Haiendi hivyo bro.
Njia hiyo ni mbaya na italipua nchi hii kwa sbb ukizidi kumwonea mtu kiasi cha kumsukumiza hadi ukutani, hata mnyonge hupata nguvu na huamua kujitetea!