CCM ndiyo chama kilichokaa madarakani kwa muda mrefu zaidi barani Afrika. Nini siri yao?

CCM ndiyo chama kilichokaa madarakani kwa muda mrefu zaidi barani Afrika. Nini siri yao?

kwa kuwafanya Watanzania kuendelea kuwa maskini na wategemezi
Chama cha CCM toka kinaitwa TANU na ASP kipo madarakani kwa zaidi ya miaka 60. Ndiyo chama kilichokaa madarakani kwa muda mrefu zaidi barani Africa.

Ni nini siri ya CCM kukaa madarakani kwa muda mrefu namna hii? Ni kwamba wanafanya kazi nzuri sana? Wapinzani wao ni wababaishaji? Au wanasiri nyingine ndani yao inayowafanya wakae madarakani muda mrefu hivyo?

Binafsi naogopa sana kuzeeka nchi ikiwa chini ya CCM.
 
Tunafanya kazi nzuri na wewe ni shahidi elimu bure matibabu bure
Mnafanya kazi nzuri ukifananisha na nani? Unajua kwamba wakati tunapata uhuru kimaendeleo tulikuwa sawa na Malaysia? Unajua malaysia wapo wapi sasa na sisi tupo wapi? Hayo matibabu bure yanapatikana hospitali gani?
 
MUNGU MMOJA akinijalia uhai hadi 2035 nitakuwa DIWANI kwa kupita chama langu CCM
 
Chama cha CCM toka kinaitwa TANU na ASP kipo madarakani kwa zaidi ya miaka 60. Ndiyo chama kilichokaa madarakani kwa muda mrefu zaidi barani Africa.

Ni nini siri ya CCM kukaa madarakani kwa muda mrefu namna hii? Ni kwamba wanafanya kazi nzuri sana? Wapinzani wao ni wababaishaji? Au wanasiri nyingine ndani yao inayowafanya wakae madarakani muda mrefu hivyo?

Binafsi naogopa sana kuzeeka nchi ikiwa chini ya CCM.
Ukondoo wa watanzania ndio siri ya CCM kuendelea kukaa madarakani kwa shuruti muda wote huo.
 
Mtaji wa CCM siku zote ni:-

1. Ujinga wa Watanzania

2. Katiba mbovu

3. Rushwa & ufisadi

4. Wizi wa kura

5. Kutumia vyombo vya dola kubaki madarakani

Soon mambo hayo yatabadilika/shwa.
 
Back
Top Bottom