Maana ya neno tafsida ni utumiaji wa lugha ya adabu na heshima ili kuondoa ukali/ukakasi wa lugha na kuleta staha.
Kundi fulani la wanaCCM limeshangilia sana mama Samia aliposema yeye na JPM ni kitu kimoja. Wanasahau kuwa huyu mama mtu wa Pwani ambako kiswahili ndiyo chimbuko.
Angekuwa sawa angemtumbua Bashiru?
Angekuwa sawa angepiga marufuku uporaji wa TRA?
Angekuwa sawa angetoa Uhuru wa vyombo vya habari?
Angekuwa sawa Safari za ndege za Chato zingesitishwa?
Muungwana ukimuomba kitu akikujibu "tutaangalia" ujue kakataa.
Sasa ninyi wakoromije endeleeni kupiga makofi.