CCM rudini shule mkasome Kiswahili. Rais Samia ni mwingi wa tafsida

CCM rudini shule mkasome Kiswahili. Rais Samia ni mwingi wa tafsida

View attachment 1755807

Maana ya neno tafsida ni utumiaji wa lugha ya adabu na heshima ili kuondoa ukali/ukakasi wa lugha na kuleta staha.

Kundi fulani la wanaCCM limeshangilia sana mama Samia aliposema yeye na JPM ni kitu kimoja. Wanasahau kuwa huyu mama mtu wa Pwani ambako kiswahili ndiyo chimbuko.

Angekuwa sawa angemtumbua Bashiru?
Angekuwa sawa angepiga marufuku uporaji wa TRA?
Angekuwa sawa angetoa Uhuru wa vyombo vya habari?
Angekuwa sawa Safari za ndege za Chato zingesitishwa?

Muungwana ukimuomba kitu akikujibu "tutaangalia" ujue kakataa.
Sasa ninyi wakoromije endeleeni kupiga makofi.
They are still dreaming nice things. Don't wake them up.
 
Wabunge wametukanwa kistaarabu ila walivyo mazwazwa, wakashangilia kwa nguvu. Ndugai na msaidizi wake wao wametukanwa tusi kubwa zaidi. Kuruhusu udemkaji bungeni ni udhaifu mkubwa sana wa kiti cha Speaker
 
View attachment 1755807

Maana ya neno tafsida ni utumiaji wa lugha ya adabu na heshima ili kuondoa ukali/ukakasi wa lugha na kuleta staha.

Kundi fulani la wanaCCM limeshangilia sana mama Samia aliposema yeye na JPM ni kitu kimoja. Wanasahau kuwa huyu mama mtu wa Pwani ambako kiswahili ndiyo chimbuko.

Angekuwa sawa angemtumbua Bashiru?
Angekuwa sawa angepiga marufuku uporaji wa TRA?
Angekuwa sawa angetoa Uhuru wa vyombo vya habari?
Angekuwa sawa Safari za ndege za Chato zingesitishwa?

Muungwana ukimuomba kitu akikujibu "tutaangalia" ujue kakataa.
Sasa ninyi wakoromije endeleeni kupiga makofi.
Samia anaongea kwa ajili ya taifa au CCM
 
Ukiisiliza na kuichambua kwa utuo historia ya Mama Samia aliyoitoa mwenyewe kwenye kongamano la siku ya wanawake utagungua kuwa sio wa kwao kama wengi wa wanaccm wanavyofikiri. Sema walimbeba juu juu na kumtwiga majukumu ambayo hakuyatarajia.

Mama ni Muungwana sana sema mfumo uliomzunguka ni ngumu kujitenganao japo anajaribu kwa akili sana.

Mama anaonekana kutumia hekima na busara nyingi sana kwy mambo yake, anaonekana hapendi kukwazana na wenye nacho ila kupitia hekima hiyohiyo na busara anapata maarifa zaidi.

Bado nina imani naye na tayali kaonyesha utofauti mkubwa hata kumsikiliza tu anatoa dalili za faraja mbeleni.
Ana lugha ya kiungwana na anao uungwana.

Ukishakuwa na mamlaka ya urais inabidi ukubali kuchafuliwa ile haiba yako, ni cheo kizuri kuwa nacho na ukapimwa na wenye akili lakini ni mzigo kwa nchi hizi za kiafrika ambazo tunapenda sana kushikana uchawi.
 
Huu ndo mtaji wa sisiem, Low Thinking Capacity kama ya huyu mama..
Kwa kifupi: Mama kakiri nguvu ya wanamtandao. Wanapiga mziki hadi yeye anasikia na kuona wabunge wake wakiucheza. Kazeni mwendo wana JF na wanamitandao wengine wote. "You are a force that can effect changes including constitutional reforms".
 
Hahaha! Neno "kudemka" mbunge Msukuma nina uhakika 100% atakuwa hajalielewa.

Atakuwa amechanganya na like neno la kisukuma "kudamka" likimaanisha kuamka asubuhi na mapema.
hahahahha, nimecheka sana, mpaka watu wamenishangaaa
 
Vyama vya upinzani havipo kupinga kila kitu cha serikali /Rais/chama tawala
Hao ni kuleta mawazo mbadala,yenye fikra na mitazamo tofauti yenye nia ya kujenga ama kuboresha wazo kwa maslahi ya taifa au wote na sii kwa kundi la wachache.Ama kuleta ama kuchochea dhana ya uwajibikaji.
 
Kwa kifupi rais SSH ameliambia bunge lipuuze ya mitandaoni

Ni kweli kabisa, maana ameona mijadala ya mitandaoni ni digital, wakati mijadala ya bungeni bado ni analogia. Sasa kaamua kuepusha aibu.
 
Back
Top Bottom