Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Baada ya kuonywa mara nyingi na wadau, sasa CCM imeanza kuelewa.
Na mimi kada nilionya huko nyuma, CCM ikiendelea kushupaza shingo, itavuna mabua 2025.
www.jamiiforums.com
Suala la Bandari na DP World CCM ililichukua kirahisi rahisi ikifikiri watu ni wakuelekezwa kibla bila upinzani wowote.
Ambacho CCM imegundua ni kwamba hata ndani ya CCM na serikali yake , mambo si shwari.
Wazee kama Mama Tibaijuka, Waziri Mkuu Mstaafu Warioba(mwanasheria) na wasomi kama Prof Shivji (mwanasheria), wameonya juu ya mapungufu ya mkataba wa Bandari na DP World kwa kitaalamu kabisa.
Baada ya Mkataba huo kupitishwa Bungeni na kutetewa na viongozi wandamizi kama Spika Tulia, bado moto uliendelea kujichochea kwa malalamiko juu ya mkataba huu.
Mbaya zaidi ni wanaharakati kama Wakili Mwabukusi na "banyambala" wa huko Mbeya walioli challenge sual zima la mkataba kwa kulipeleka Mahakamani.
Sasa CCM imeamka usingizi wa pono!
Hawawatumi tena vibaka wa kisiasa, kina Kitenge, Zembwela na Hando kutetea Bandari saga.
Sasa Chongolo Katibu Mkuu mwenyewe ni kiguu na njia kulielezea suala la Bandari nchi nzima.
Huko Mwanza, Chongolo sasa anasema;
"Mkataba huu siyo msahafu wala biblia kusema kuwa hauna dosari, kwani umeandikwa na binadamu"
Anaendelea Chongolo:
"...aliitaka serikali kufanya marekebisho katika maeneo yenye tija katika mkataa huo wa uwekezaji na kuhakikisha yanafanyiwa kazi haraka ili utekelezaji uanze haraka"
Ref Nipashe pg 1, pg 2(31/07/2023).
Hiki ndio watanzania walitaka kisikike kutoka CCM, kuwa;
- kwanza, kuna mkataba ulioingiwa kinyemela,
-pili, mkataba huo una makosa,
-tatu,mkataba huo urekebishwa
-na nne , uwekezaji uendlee kwa kutilia maanani maslahi ya Taifa
Kwa Chongolo kukubali kuwa kulikuwa na makosa, basi tusonge mbele, wenye akili watajua binafsi nani aliteleza.
Na mimi kada nilionya huko nyuma, CCM ikiendelea kushupaza shingo, itavuna mabua 2025.
CCM, kwa mtaji wa ukakasi wa suala la Bandari, kaeni mguu sawa kung'olewa!
Suala la Bandari linajadiliwa kwa marefu na mapana kila kona ya nchi. Maandamano ya vyama vya upinzani yameshaanza mikoani kupinga suala zima la ubinafsishaji/uuzwaji/ukodishaji, au hata kuigawa bure Bandari yetu na nyingine Tanzania. Tukubali tusikubali, serikali ya CCM imeingia mkenge mkubwa...