CCM, Serikali Mbili Zilizoboreshwa, na Hatima Ya Muungano

Ila nakubaliana na wewe kuwa kadri muda unavyoenda, watanzania wengi wanazidi kuona umuhimu wa serikali tatu. Hii haitanizuia hata siku moja mimi kuwa na ndoto kwamba siku moja tutakuwa taifa moja hata kama siku hiyo sitaiona. Na nitawasisitizia vizazi vijavyo wawe watu wa taifa moja chini ya jamhuri moja. Ukiniona ni punguani, sawa tu ila ndiyo wish yangu na wewe una wish yako and I do respect that.

Kwani nani anasema serikali tatu ni zaidi ya jamhuri moja na nchi moja? Why are you making serikali kuwa synonymous to nchi na jamhuri? Hivi umeusoma mkataba wa muungano (1964)? Uliweka serikali tatu, nchi moja, jamhuri moja. Na ni hilo tume na hata mimi ndio tunajengea hoja. Lakini wapotoshaji wanajaribu lazimisha serikali na nchi viwe ni vitu synonymous.

Hapo juu nilisema pia kwamba baina ya takwimu na gharama kwa upande mmoja, na implications za katiba ya znz (2010), the later overshadows the former in significance. The former ni ya baadae, ya msingi ni ya katiba ya znz, je kwanini mnakimbia hilo tatizo na mnarukia gharama na takwimu? Mkiwa na majibu ya takwimu na gharama kwa wananchi, je yatajibu vurugu za kikatiba, kisheria, uporaji wa mamlaka ya muungano na mshirika mmoja wa muungano (znz)?

Wengi tunapenda serikali moja, then humo ndani we can decentralize via provinces etc, lakini serikali moja haiwezekani, znz hawawezi kubali hilo, kwanini mnapoteza muda na wishful thoughts wakati matatizo na hatari iliyopo mbele yetu ni contemporary? Majibu yako kwa hili ni muhimu yawe consistent na wewe kukiri hapo juu kwamba the trend among wananchi favours serikali tatu.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Corrections za bandiko hili, please review again cc Kobello:

Nachojaribu kukuelewesha ni kwamba hapa tunaangalia rasimu mbadala ya ccm. Nimeona sehemu zake kadhaa lakini sijafanikiwa kukamata nakala. Nyaraka hii bado ni ya siri sana ndani ya chama, wanataka surprise tu na kuburuza watu. NEC ya leo ina wajumbe zaidi ya 200, nadhani utakuwa unajua angalau mnec mmoja, muulize kuhusu haya niliyo andika.

Maelezo yangu kwa Kobello ktk bandiko hili was meant kuishia hapo juu na suala ya rasimu mbadala ya CCM.
Familia yangu yote ni TANU/CCM nani walalahoi tu, ila tunaamini misingi yake . Hawa jamaa waliopo sasa hivi najitahidi kuwaelewa lakini ninashindwa. Ila wewe tuachie tu, sisi tutapambana na kukisafisha.
Simjui hata MNEC mmoja, na ninaowafahamu wana simu nne na namba yangu ipo kwenye laini wanayoitumia kila baada ya miaka mitano.
 
Kobello,
Cc Nguruvi3,

Ebu tufanyie haki hoja hii ya takwimu.

Tuanze na uwasilishaji wa Warioba:

Hoja ya Kikwete ambayo ndio imezaa kina kobello et al ni hii:

Tuchambue:

Hapa tunaona kwamba Jaji Warioaba na Rais Kikwete wanaongelea data ile ile.

Tukiangalia kwa "face value", tafsiri zote zina logic, validity, pamoja na kwamba zinafikia hitimisho tofauti, lakini hitimisho kwa pande zote mbili linatokana na data zile zile. Kwa maana hii, tunaweza sema kwamba tafsiri zote mbili (Warioba na Kikwete/Kobello), zote zipo questionable kwani - zote zinategemea zaidi sample ambayo ni "self selecting" kama tulivyoona Kikwete alivyofanya, Kobello alivyofanya, na pia Warioba anavyokuwa accused kufanya na Kobello na Kikwete.

Lakini baada ya hapo, Kikwete na Kobello wanaanza kuachwa na facts za mathematics of probability, huku facts hizi zikimbeba Warioba. Nitafafanua:

Kwanza, takwimu za tume ni "more indicative" kuliko "conclusive", ndio maana mchakato unaishia kwenye kura ya maoni. Lakini kina Kobello wanang'ang'aniza takwimu zao ziwe conclusive.

Pili na muhimu zaidi, tafsiri ya warioba ikilinganishwa na tafiti nyingine zilizofanywa na other credible research institutes zinaoana zaidi na tume kuliko Kikwete na Kobello. Kwa maana nyingine, unlike Kobello and Kikwete, tafsiri ya tume has more popular support. Tuangalia tafiti za afrobarometer na twaweza, taasisi ambazo ni very credible nchini, huku afrobarometer ikiwa credible all over africa, asia, south america and middle east. Je wanasemaje?
(Source zipo website za twaweza na afrobarometer):

Mkiangalia tafiti za taasisi hizi, mwaka 2012, kabla ya rasimu ya kwanza kutolewa, 47% ya watanzania bara walipendelea serikali mbili ziendelee.
Kwa upande wa Zanzibar, 29% walipendelea serikali tatu.

Mwaka 2013, baada ya rasimu ya kwanza kutoka, hali ikabadilika. 26% tu ya watanzania bara walisema serikali mbili ziendelee, na upande wa zanzibar, 51% walitaka serikali tatu.

Rasimu ya pili ya katiba imekuja na takwimu hizo hapo juu. Tunachoona hapa ni vitu vitatu muhimu sana katika mathematics of probability ambavyo ni indication ya any good study: validity, reliability and replicability.

Kwanza - takwimu za warioba ni valid, reliable and replicable. Kina Kobello na Kikwete hakuna hiki kitu. Nitafafanua. Maana ya reliability in research ni - degree to which an assessment tool produces stable and consistent results. Kwa maana nyingine, a scientific experiment must be replicable katika details zake ili iwe considered valid.

Tukitazama takwimu za afrobarometer na za twaweza, we see kwamba zipo more consistent na za tume kuliko Kikwete na Kibello. Kwa maana nyingine, takwimu za tume zipo replicable na zile za afrobarometer na twaweza, kuliko za kobello na kikwete. Pia zipo proven valid kwa kuangalia hizi za twaweza na afrobarometer kwani kuna consistency, na kwa maana hiyo zipo reliable kwani ukienda kwenye same population,utakutana na kitu kinachofanana in terms of findings za tume, twaweza and afrobarometer.

Kuna fact nyingine muhimu hapa:

Kwa jinsi muda unavyozidi kwenda, wananchi wengi zaidi wanaendelea kutaka serikali tatu.

Ni kwa mantiki hii, Lukuvi, Kobello na wengine wameona hatari ipo wapi, nayo ni kwamba: Kura ya maoni italeta serikali tatu. Kwahiyo cha kufanya ni kuwavuruga wananchi na takwimu, kutishia wananchi jeshi kupindua nchi, na kujenga hoja za udini.

Kuna haja ya wahusiku kurudi katika hoja ya msingi - nayo ni je, what's the way forward kuokoa muungano kufuatia action ya zanzibar kikatiba na madhara yake kisheria za nchi, katiba, mamlaka ya washirika wa muungano, mamlaka ya rais...., je hoja ya gharama na takwimu ina umuhimu zaidi kuliko mgongano uliojitokeza? Please, don't derail the nation kwa ujinga wa kisiasa and put everyone's situation (including the union) at risk.
Mchambuzi data ambazo zilitakiwa ziwe indicative Kikwete na Kobello wamezifanya 'concusive' kama ulivyosema.
Data za Warioba zilikuwa kama straw poll ambayo ingetumika kufanyia kazi, in the end kura ya maoni inge prove validity ya data za Warioba 'conclusive'

Kikwete na Kobello wanafanya hypothesis kwa njia tofauti kidogo na inachanganya
1. Kikwete kasema 86% hawakuzungumzia muungano.
Hii haituelezi kuwa walikubali au walikataa, tunachojua hawakuzunguzia.

2. Kikwete na Kobello, wanasema data za Warioba si za kweli kuwa wananchi wanataka S3.
Fine, wapi matokeo ya ''null huypothesis'' yao kwamba wananchi hawataki S3?

Tume ya Warioba ina data zote zinazo wa back up ndio maana wanaweza kujenga hoja,
Kobello na Kikwete wanatumia asilimia 86 ambayo haijulikani kama ilitaka au haikutaka (kumbuka hawakuzunguzia kwa mujibu wa Kikwete). Hata kama kwa bahati mbaya wana data za ku fit kuwa wananchi wanataka S2 watawezaje kuzi back up wakati ambapo wanatumia asilimia 86% kama data zisizojulikana zinaelekea wapi au zinaelekeza nini (kumbuka, 86 hawakuzungumzia muungano kwa mujibu wa Kikwete)

Ukiangalia Kobello na Kikwete wame picku up namba 86 na kuifanya 'indicative na coclusive' hapo hapo.
Ndio maana hawataki suala lifike kwa wananchi, wanataka short cut wamalize mambo nyuma ya pazia Dodoma
Hata tukiwapa Kikweta na Kobello benefit of doubt, bado kuna maswali mengi yanajitokeza.

Hivi wanawezaje kusema asilimia 86(ambayo haikuzungumza kwa mujibu wa Kikwete) inataka serikali 2.
Je, idadi ya wabunge wa CCM 400 ndiyo back up ya data zao au ndiyo sample yenyewe?

Kama ina back up, ina back up nini(hawakuzungumzia kwa mujibu wa Kikwete) na kama 400 inasimama kama sample size, ipi ni kubwa ya Warioba au wabunge wa CCM?

Hata kama watasema wabunge wanawakilisha maelfu ya watu, bado conclusion itakuwa na matatizo.
Kwa maana kuwa haina reliability au replicability.
Wabunge 400 walioko gereza la uwazi Dodoma, ukiwaachia huru wapige kura bungeni au nje kwa siri hupati majibu sawa.
 
Last edited by a moderator:
Kwani nani anasema serikali tatu ni zaidi ya jamhuri moja na nchi moja? Why are you making serikali kuwa synonymous to nchi na jamhuri? Hivi umeusoma mkataba wa muungano (1964)? Uliweka serikali tatu, nchi moja, jamhuri moja. Na ni hilo tume na hata mimi ndio tunajengea hoja. Lakini wapotoshaji wanajaribu lazimisha serikali na nchi viwe ni vitu synonymous.

Hapo juu nilisema pia kwamba baina ya takwimu na gharama kwa upande mmoja, na implications za katiba ya znz (2010), the later overshadows the former in significance. The former ni ya baadae, ya msingi ni ya katiba ya znz, je kwanini mnakimbia hilo tatizo na mnarukia gharama na takwimu? Mkiwa na majibu ya takwimu na gharama kwa wananchi, je yatajibu vurugu za kikatiba, kisheria, uporaji wa mamlaka ya muungano na mshirika mmoja wa muungano (znz)?

Wengi tunapenda serikali moja, then humo ndani we can decentralize via provinces etc, lakini serikali moja haiwezekani, znz hawawezi kubali hilo, kwanini mnapoteza muda na wishful thoughts wakati matatizo na hatari iliyopo mbele yetu ni contemporary? Majibu yako kwa hili ni muhimu yawe consistent na wewe kukiri hapo juu kwamba the trend among wananchi favours serikali tatu.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Unajua mkuu Mchambuzi,kuna watu wamemcheka mama Mongella alipozungumzia uwingi wa serikali.Hapa kinachogombewa ni REPUBLICS na siyo governments.
Hii rasimu ya Warioba imeifanya serikali ya muungano kuwa mbali kabisa ya wananchi. Serikali ya muungano chini ya rasimu hii haina carrot wala stick, unless unionyeshe.
Watanzania inabidi tuwe waangalifu mno kwa sababu serikali ya muungano ni symbolic tu unless jamaa waioverhaul rasimu. Kama unajua unachokipigania, sawa.
Serikali moja inawezekana sana tu. Ni kama wayahudi na wapalestina wanavyoweza kuwa ndugu na kuishi pamoja chini ya nchi moja.
It is possible, ila tumejiaminisha tu kuwa haiwezekani.

Kuhusu consistency yangu, I will never guarantee you that. Kadri siku zinavyoenda tutapeana elimu kuhusu umuhimu wa sisi kuwa na serikali moja/jamhuri moja kwa sababu mpaka sasa hivi, tamaa za wanasiasa ndiyo zinachochea serikali tatu na siyo nia ya kuimarisha muungano.
 
Mchambuzi data ambazo zilitakiwa ziwe indicative Kikwete na Kobello wamezifanya 'concusive' kama ulivyosema.
Data za Warioba zilikuwa kama straw poll ambayo ingetumika kufanyia kazi, in the end kura ya maoni inge prove validity ya data za Warioba 'conclusive'

Kikwete na Kobello wanafanya hypothesis kwa njia tofauti kidogo na inachanganya
1. Kikwete kasema 86% hawakuzungumzia muungano.
Hii haituelezi kuwa walikubali au walikataa, tunachojua hawakuzunguzia.

2. Kikwete na Kobello, wanasema data za Warioba si za kweli kuwa wananchi wanataka S3.
Fine, wapi matokeo ya ''null huypothesis'' yao kwamba wananchi hawataki S3?

Tume ya Warioba ina data zote zinazo wa back up ndio maana wanaweza kujenga hoja,
Kobello na Kikwete wanatumia asilimia 86 ambayo haijulikani kama ilitaka au haikutaka (kumbuka hawakuzunguzia kwa mujibu wa Kikwete). Hata kama kwa bahati mbaya wana data za ku fit kuwa wananchi wanataka S2 watawezaje kuzi back up wakati ambapo wanatumia asilimia 86% kama data zisizojulikana zinaelekea wapi au zinaelekeza nini (kumbuka, 86 hawakuzungumzia muungano kwa mujibu wa Kikwete)

Ukiangalia Kobello na Kikwete wame picku up namba 86 na kuifanya 'indicative na coclusive' hapo hapo.
Ndio maana hawataki suala lifike kwa wananchi, wanataka short cut wamalize mambo nyuma ya pazia Dodoma
Hata tukiwapa Kikweta na Kobello benefit of doubt, bado kuna maswali mengi yanajitokeza.

Hivi wanawezaje kusema asilimia 86(ambayo haikuzungumza kwa mujibu wa Kikwete) inataka serikali 2.
Je, idadi ya wabunge wa CCM 400 ndiyo back up ya data zao au ndiyo sample yenyewe?

Kama ina back up, ina back up nini(hawakuzungumzia kwa mujibu wa Kikwete) na kama 400 inasimama kama sample size, ipi ni kubwa ya Warioba au wabunge wa CCM?

Hata kama watasema wabunge wanawakilisha maelfu ya watu, bado conclusion itakuwa na matatizo.
Kwa maana kuwa haina reliability au replicability.
Wabunge 400 walioko gereza la uwazi Dodoma, ukiwaachia huru wapige kura bungeni au nje kwa siri hupati majibu sawa.
NAaqijibu yote kwa mpigo kwa sababu precedent ambayo hoja yako ipo chini yake ni very wrong.

1. Sikusema kuwa 86% wanataka serikali 2. Bali,
a) Hawatajali kama status quo itabadilishwa au la
b)wanataka mfumo bora kuliko uliopo ila options hawazijui na zilizopo haqzileti maana kwao.
One of these.

Kwa hiyo, Kikwete kwa kuona kuwa wana majority bungeni, na takwimu zinaonyesha kuwa wengi wameachia mpira kwenye kumi na nane, basi ataweka S2 (most likely kuizidishia autonomy ZNZ) na kubet on refferrendum.
UKAWA wanatafsiri kuwa hao 86% wasifikiriwe kama sample size na tuende na waliozungumzia muungano tu. That is wrong!

2)Sijasema kuwa data za Warioba si za kweli, data ni za kweli ila tafsiri ya data hizo ipo very fawed. Huwezi kupuuza asilimia 86 kwa sababu NOT TO DECIDE, IS TO DECIDE.
 
Mdondoaji,

Nianze kujadili kidogo suala la gharama za serikali moja vis a vis tatu kama ulivyoomba. Nilikuwa nasubiri uniambie analytical framework uliyotumia kufikia hitimisho kwamba serikali moja ni nafuu. Haujaja nayo, hivyo ni dhahiri kwamba hauna.

Unachofananisha wewe nadhani ni sawa na mtu kuwa na gari moja au matatu, ipi ni nafuu zaidi, that's how linear your argument is. In linear terms, ofcourse gari moja ni nafuu kulihudumia mafuta, matengenezo, bima, road tax etc kuliko kuwa na magari matatu. Kwahiyo kama tunajadili a linear relationship, upo sawa.

Suala la serikali carries a multi dimensional aspect. Kuna siasa, masuala ya kijamii ambayo ndani yake kuna diversity, na muhimu zaidi, kuna suala la uchumi, ambalo ndio nguzo kuu, hasa public finance (mapato na matumizi).

Hapo juu umetupia tu bajeti ya serikali in a copy and paste fashion, kama vile unacheza darts - unarusha mshale wa darts, bila ya kujua precisely utatua wapi. Sidhani kama una uhakika umetua wapi na hizo data za bajeti. Ni muhimu uelewe kwamba hata hizo data zimeundwa, usione zinaelea tu kwenye tovuti husika ukazibeba hivyo hivyo tu. Ukipata muda, kaangalie "public expenditure reviews" za kila mwaka uone jinsi gani bajeti zimejaa mapungufu. Nikipata muda nitaya jadili, na baadhi ya mapungufu hayo, Lipumba, Zitto wameyajadili vyema sana ndani ya Bunge la Katiba katika kuonyesha jinsi gani serikali mbili mis-allocate resources. Tutaliangalia hili kwa undani zaidi baadae.

Kwa sasa niseme tu kwamba - unapoleta two autonomous entities in the context of fiscal matters, kwa maana ya tanganyika na znz, efficiency inakuja pale tu iwapo kila upande utapata autonomy fiscal wise. Katika muungano wa two sovereign states, lazima uwe na subnational governments working with the national government. Ndio maana mwalimu aliamua angalau iwepo ya znz, na hii ya Tanganyika, ita sacrifice kubeba muungano in the spirit of "pan-africanism". Ingawa tunapenda kujisifia kwamba sisi ni muungano pekee afrika, ukweli ni kwamba we are a case study of failure. Hii ni kwasababu muungano ulikuwa based on pure political grounds. Uchumi haukuwa considered kama siasa. Tazama katiba ya JMT (1977), haizungumzii hata the basic economic justice ya washirika wa muunngano. Hakuna. Uchumi ulitumikia siasa, basi.

Pia kuna hoja kwamba Tanzania ni jina tulilojipatia wenyewe, sio la mkoloni. Hii hoja ip very weak, hoja ya maana ni je, mipaka ya mkoloni tulifuta? Jibu ni hapana. Isitoshe, Mipaka ya Tanzania Bara ni ile ile ya Tanganyika hivi tunavyozungumza. Muhimu zaidi, Zanzibar wameshasema kwenye katiba yao, mipaka yao ni ile ya kabla ya 1964. Ni kwa maana hii, rasimu pia imeeleza hilo kwa Tanganyika.

Tukirudi kwenye suala la gharama:

Given hoja hapo juu ya haja ya subnational governments working with the central government, fiscal autonomy is what brings about efficiency in allocating resources (public finance matters). Unaweza ukaja na hoja kwamba kuna serikali za mitaa to deal with that - hii argument ni weak kwa sababu, local governments sio suala la muungano na haliwezi kuwa hivyo kwani serikali hizi za mitaa zinaendeshwa na katiba ya ndani ya subnational government (s). Hazina uhusiano na katiba inayoziunganisha pande mbili, tatu, nne za muungano. Lakini suala la kuleta two sovereign states linahitaji katiba ya pamoja. Nilikusoma awali ukijadili your preference ya sera ya majimbo na kwamba ndio solution ya matatizo ya muungano, kwa kuweka serikali moja. Hii ni wishful thought, nitaijadili baadae kidogo.

Iwapo tupo sawa hadi hapa juu ya umuhimu wa fiscal autonomy as a means of efficient allocation of public resources, the devil is in the details, so I will elaborate next:

Serikali kuu, na serikali shiriki - ndio uendesha muungano. Na katika muktadha huu, kila serikali ina competence yake ambayo ni unique, kwa mfano, sio kila aina ya taxes zipo more effective kuendeshwa na serikali kuu. Pia sio kila matumizi yana trickle down effect nzuri yakifanywa na serikali kuu. Yapo maeneo ambayo subnational government ina competence zaidi kuliko serikali kuu, and vice versa holds. Haya ndio mambo nimepanga kuyajadili in details kwenye uzi ujao.

Lakini hapa niseme tu kwamba - serikali moja unayotaka wewe, Kobello, Mzee Mwanakijiji, Pasco, na wengine - wote mna ignore hii factor ya competence in different areas of taxation. Mna amini kwamba uniformity brings more efficiency wakati ukweli ni diversity that brings more efficiency. Mbali na suala la utofauti wa competence, pia lipo suala la upande mmoja kujifunza kutoka kwa fiscal system ya mwenzake badala ya kuweka all eggs in one basket. Faida ni nyingi, nitazijadili kwenye uzi maalum huku nikitumia contemporary data.

Nadhani hadi hapa umepata idea juu ya umuhimu wa uwep wa subnational governments zenye fiscal autonomy na zenye specialization in administering aina fulani fulani ya taxes kutokana na kuwa more competent, huku central government ikibakia na maeneo yake ya competence. Kukosekana kwa mgawanyiko huu ndi chanzo cha serikali mbili kuwa mzigo wa wananchi, na ndio maana nikasema hapo juu kwamba - uhusiano wa idadi ya serikali na gharama kwa wananchi haupo linear kama mnavyodhani.

Kuna haja ya kuwa na serikali tatu kwani kila upande again utatumia competence yake kutokana na geography, resources:
*Human Resources.
*Physical Resources.
*Natural Resources.
*Social Resources (social capital).
*Financial Resources.
*Political Capital.

Msingi wa competence unajengwa na haya, among other things. Ni kutokana na haya, ndio tax bases zitakuwa determined, innovation in mobilization of domestic resources - hasa new sources of revenue, etc.

Na kwa upande wa matumizi - efficiency in allocation pia itakuwa kubwa kwani baina ya serikali kuu na serikali shiriki (mfano Znz), anayejua priority za wananchi ni nini ni znz. Same applies to Tanganyika vis a vis Serikali kuu. Hali hii itapelekea mapato kuwa more transparent, matumizi kuwa monitored vizuri zaidi kwani yanakuwa linked moja kwa moja na local politics, sio hazina ya muungano.

Nadhani hadi hapa unaona jinsi gani serikali moja ni optimally inefficient kwani it means centralization of resources kwa serikali kuu bila ya kujali kama ina more competence katika maeneo ya kodi na matumizi mbalimbali vis a vis serikali shiriki.

Nimalizie na masuala mawili - serikali za majimbo, na serikali za mitaa.

Wewe ni muumini wa serikali za majimbo. With all due respect to Chadema on this one, hii sera haifai katika mazingira ya muungano. Kwanza, itazidisha grievances za zanzibar kwamba inamezwa, kwani it means znz ambayo ni moja ya nchi shiriki za muungano, sasa inageuzwa kuwa ni moja ya majimbo ndani ya muungano. Pili na muhimu zaidi, mabadiliko ya znz kikatiba (2010), wazanzibari hawatarudi nyuma, sio kwa shinikizo la CCM, sio kwa serikali ya muungano, na wala sio kwa nguvu za jeshi.

Na pili - serikali za mitaa. Hizi zimekuwepo kwa muda mrefu sana, zilifutwa baada ya uhuru na kurejeshwa tena 1984. Kuna mafanikio kadhaa yamejitokeza kama vile uboreshaji wa miundo mbinu, ujenzi wa shule, vituo vya afya, lakini ukweli unabakia kwamba mafanikio ya sera hii ni MORE QUANTITATIVE THAN QUALITATIVE. Barabara zimeboreshwa, lakini hazisaidii kupunguza umaskini kwani badala ya kupungua in the last 20 years kwa mfano, umeongezeka. Vituo vya afya vimejengwa vingi lakini hali za afya za wananchi walio wengi leo ni mbaya kuliko miaka ya azimio la arusha. Elimu - shule zimejengwa nyingi sana za kata, hence kuwa ni mafanikio quantitatively, lakini QUALITY wise, we all know nini kinaendelea. Why is it so?

Ni kwa sababu serikali kuu haitaki tekeleza decentalization in practice, it just preaches it. Kwa mfano, halmashauri zote hazina fiscal autonomy. Prioritization inafanywa na serikali kuu, sio na local government. Ushahidi wa hili upo wazi. Pia serikali kuu doesn't encourage local governments kuwa innovative na vyanzo vya mapato, ndio maana unakuta halmashauri ipo kwenye eneo lililojaa rasilimali kubwa lakini sehemu kubwa ya bajeti yake bado inategemea ruzuku ya serikali kuu kuliko vyanzo vya mapato locally. Pia kila mwaka wa fedha tunaona kwamba sehemu kubwa ya fedha zinazengwa hazifiki huko chini. Kwa mwaka huu wa fedha kwa mfano ambao tayari ni mpya, yapo maeneo ya nchi yetu ambayo hayajapata fedha zilizotengwa, maeneo mengi haifiki 60pct ya fedha zilizotengwa. But interestingly enough? Fedha zinazotengwa for nchi jirani ya Zanzibar zinafika kwa wakati, na mara nyingi huwa ni zaidi ya walizotengewa - over 100pct.

Tafadhali nipe muda nipange vizuri analysis yangu juu ya unafuu wa gharama za serikali tatu vis a vis mbili, na hata moja. Nikiwa tayari, nita share accordingly.

Cc MwanaDiwani/Mwigulu Nchemba, Nape Nnauye, Ritz, HKigwangalla, Anna Tibaijuka, Ezekiel Maige, Tumaini Makene, Yericko Nyerere, Gamba la Nyoka, Mtanganyika, FJM, Mag3, EMT, JokaKuu, Zakumi

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Hii rasimu ya Warioba imeifanya serikali ya muungano kuwa mbali kabisa ya wananchi. Serikali ya muungano chini ya rasimu hii haina carrot wala stick, unless unionyeshe.
Ni kitu gani umeongea hapa. Kati ya serikali moja, mbili au tatu, mfumo upi unapeleka serikali karibu zaidi na wananchi? As a matter of fact, serikali moja ndio ipo mbali kabisa na wananchi, ikifuatiwa na serikali mbili. Unless uelewa wetu juu ya serikali na wananchi haupo sawa. Iwapo utajadili suala la local governments (ikitokea hivyo), I have addressed this earlier na nimeku 'cc'.

Ilitakiwa useme hivi hapo juu:

Rasimu ya Katiba imewafungua wananchi, hasa wa Tanganyika (ukipenda ita Tanzania Bara) jinsi gani serikali yao ipo mbali nao.

Na katika hili ni kama umejichanganya kidogo unaposema:

Watanzania inabidi tuwe waangalifu mno kwa sababu serikali ya muungano ni symbolic tu unless jamaa waioverhaul rasimu. Kama unajua unachokipigania, sawa.

Hapa sijakuelewa kwani inaonekana kama vile unapinga mfumo wa sasa wa muungano (serikali mbili) kitu ambacho rasimu pia imefanya hivyo, yet hapo juu unampinga warioba. Unaposema "unless jamaa waiovehaul rasimu", jamaa ni kina nani? Na overhaul ya namna gani, maboresho ya serikali mbili? Tumeonyesha hayana maana. Je, mfumo wa serikali moja? Tumeonyesha hii ni wishful thinking. Overhaul gani iliyobakia?

Serikali moja inawezekana sana tu. Ni kama wayahudi na wapalestina wanavyoweza kuwa ndugu na kuishi pamoja chini ya nchi moja.
It is possible, ila tumejiaminisha tu kuwa haiwezekani.
Unatumia so much time, energy and resources kujadili kitu kisichotekelezeka, hivi ni kwanini mkuu. Warioba jana kasema kwamba baada ya kusikia malalamiko ya znz juu ya koti la muungano kuvaliwa na Tanganyika, pakawa na options mbili - serikali moja au tatu. Moja haiwezekani kwani sasa haitakuwa Tanganyika kuvaa koti bali sasa itakuwa ni "turubai". Kwanini hamuoni hili?

Kuhusu consistency yangu, I will never guarantee you that. Kadri siku zinavyoenda tutapeana elimu kuhusu umuhimu wa sisi kuwa na serikali moja/jamhuri moja kwa sababu mpaka sasa hivi, tamaa za wanasiasa ndiyo zinachochea serikali tatu na siyo nia ya kuimarisha muungano.
Serikali tatu sio tamaa ya wanasiasa. Unaishi USA I suppose, na hapo kuna serikali kuu, na serikali shiriki 50; je msukumo wake ni kiu ya madaraka? Hivi unadhania USA ingekuwa na mafanikio ya leo kama ingeamua kuwa na serikali moja 300 years ago? Msipotoshe uhalisia wa mambo.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mchambuzi
Naona unajaribu sana kuipaka matope CCM; hivi walichotoa CCM kama taasisi ni maamuzi au ni mapendekezo? Suala la katiba ni haki ya kila mtanzania na ndio sababu serikali aliweka utaratibu wa kila mtanzania kutoa maoni; sisi CCM kama taasisi mapendekezo yetu ni kuendelea na serikali 2; serikali 3 kwa mtazamo wetu hazitaondoa kero zilizopo; katiba haiwezi kumridhisha kila mwananchi; katika dunia yetu katiba ya India ndio inayosifika kuwa ni bora na ya kidemokrasia kushinda katiba zote suala la msingi la kujiuliza pamoja na ubora wa katiba ya India je inamnufaisha kila raia wa India? zipo katiba katika nchi tunazosema zimeendelea na ndio tunaiga kutoka kwao lakini katiba zao zina mapungufu mengi zipo zinazosema kama wewe sio mkristo wa madhehebu ya Anglikana huwezi kuwa waziri mkuu au kama sio mkatoliki huwezi kuwa waziri mkuu; ila walio wengi wamezikubali na ndio zinatumika hadi sasa; kwa hiyo hii katiba yetu haipo kumridhisha kila mtu ila walio wengi wataikubali hiyo ndio maana ya demokrasia; CCM tumetumia haki yetu kama taasisi kutoa mapendekezo na tunaamini wanachama wetu na watanzania wenye kuitakia mema nchi yetu watatuunga mkono. Mnapotumika kisiasa jiulizeni kwa makini huyo anayekutumia ana malengo gani sio kila anayepiga kelele Tanganyika irudi anaitakia mema nchi yetu; hoja nyingi ulizozileta ni dhaifu sio kama majibu yake hayapo ila kwasababu umeamua kujifurahisha endelea kujifurahisha; sisi CCM tupo imara na tunazifanyia kazi kero zilizopo kwa mustakabali wa taifa letu.
 
Kwanza Mwalimu aliwahi kutuasa ndani ya chama kuachana na ya kijinga na kufanya ya maana. Hili la maboresho ya serikali mbili ni la kijinga kwa hoja zangu huko juu. Inatakiwa na wewe uzijadili kwa hoja.

Pili, ikiwa wewe ni mwanachama wa kweli, sio wa kuunga unga, basi utakuwa unaelewa kwamba
Mwongozo wa CCM (1982) una kanuni ambayo pengine hauijui. Inasema hivi:

“KUKOSOA NA KUKOSOLEWA NDIO SILAHA YA MAPINDUZI”;

Kanuni hii inahimiza juu ya viongozi na wanachama wa CCM kukubali kukosolewa bila ya kuhamaki kwani hivyo ndivyo tutaweza kujenga na kuimarisha chama.

Wewe unachofanya hapa ni kuhamaki wakati kinachoendelea sio tu kwamba hakiimarishi chama, bali hata muungano.

Mapendekezo unayosema chama ina haki ya kuyatoa, ni kwa mantiki gani iwapo yanaenda mbali na kuwa ni rasimu mbadala ya ile ya wananchi iliyowasilishwa na tume?

Kama ulikuwa haujui ni nani haitakii mema nchi yetu basi ni wana CCM wanaoizuia Tanganyika isirudi kwani gharama ya kuizuia italipwa na CCM, na tumeshaanza kuona dalili hizi, ikiwepo makada wa ccm kuanza uchochezi wa kidini na uchochezi wa jeshi.

Na sipo peke yangu ndani ya ccm nisiyeridhishwa na mwenendo wa chama juu ya suala hili. Wapo wanachama wengi, wengine wazito kabisa ambao mkinywa kahawa, wanaongea lugha hii hii, wakienda dodoma, tunabaki shanngaa wanavyo "ufyata".

Unafiki, ufisadi na usaka tonge ndio vimebakia kama nguzo kuu za chama.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Tafadhali nipe muda nipange vizuri analysis yangu juu ya unafuu wa gharama za serikali tatu vis a vis mbili, na hata moja. Nikiwa tayari, nita share accordingly.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Mkuu Mchambuzi, asante kwa hii, nakusubiria!.

Wengi, ninaowasikia wakiuzungumzia Muungano, wanazungumzia zaidi structure badala ya dhima!.

Dhima ya Muungano ni kauli tuu,

Nyerere: "Tuungane!"
Karume: Sawa!, Wewe Rais, Mimi Makamo!".

Walidhamiria nchi moja na serikali moja "true Union!"

Zanzibar iliachiwa utawala wakre kwa muda as a transition steps kuelekea kwenye serikali moja!.

Hivyo kama ni kumuenzi Baba wa Taifa, safari sasa iwe ni kwenye serikali moja!.

Wote watakaopinga hoja ya serikali moja, waje na solid reasons other than, pride, selfishness na uchu wa madaraka!. Kama Watanganyika tulikubali ku sacrifice utaifa wetu kwa miaka 50 sasa kwa ajili ya Utanzania, now its about time, Zanzibar should do the same!. Hata kama wenyewe hawataki, we can make them taka!,

Kwani Muungano walioutaka tangu mwanzo?!. Si tumewafanya wautake!, then tunaweza kuwafanya wakatulia ndani ya serikali moja kwa utaratibu ule ule tunaoutumiaga kuwatuliza!.

Pasco.
 
Mchambuzi.
Kwa jinsi ambavyo wachangiaji wa CCM ktk Bunge la Katiba wameshindwa kushawishi kwa hoja za Kisheria na Kikatib, inatosha kumshawishi mtu yeyote makini kwamba CCM haina hata robo dose ya Kero za muungano.

Lakini tunajifunza aina ya wanasiasa walioko ktk chama tawala. Ni wabinafsi sana. Haijalishi amesoma ama aliishia msingi ama ametembea dunia hii na kufanya kazi na watu wasiopenda njia za mkato kiasi gani! Akiingia madarakani anafanya mambo y aibu.

Ni waraka wa watu walevi wa madaraka na wasio penda mijadala huru. Kama utaona hata wanachama wao hawataki wauone waraka wao na waujadili na kutoa mapendekezo.
 
Mdondoaji,

Umetaja kwamba Game Theory na Invisible inspired you in so many ways including economic reasoning. Waalike kwenye uzi wa Nguruvi3, nadhani wataona kitu kwani kama upo sahihi kuhusu umakini wao, hawatapitia ule uzi kwa juu juu na kusema umejaa siasa.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Mchambuzi,

JF imekuwa kichaka cha watoto ila waalikeni tutajadiliana kiustaarabu kuliko wakiingia hawa vurugu mechi. Besides mie sijui jinsi ya kutag tag wanangu wanaita sijui hashtag but waiteni watakuja kama mimi.
 
Kwanini usome juu juu iwapo unauliza swali kwa nia ya kuelewa?

Wapi kuna siasa? Kwanini tusijadili hili kule na hapa tupishe zaidi mjadala wa rasimu mbadala ya ccm? Nimesema kwamba naandaa mjadala, na uzi huo utakuwa mrefu kidogo, tukianza humu tutaondoa focus ya uzi huu, na nikikujibu juu juu hautaelewa vyema.

Kule I have made a lot of arguments on economic grounds, not just political, na narudia tena, zile arguments are only indicative towards uzi naoandaa, not conclusive.

Tatizo lenu mnarukia hoja ya gharama bila any framework of analysis and jump into conclusion. Very briefly nitakuambia why serikali moja sio tu ni mzigo kuliko tatu, bali hata mbili. Lakini kwanza niambie ur framework unayotumia kujengea hoja kwamba serikali moja ni nafuu. Nakuuliza kwa sababu aidha hauna au ipo flawed. In other words, how do u reach to a conclusion kwamba serikali moja ni nafuu? Nijibu so that I tell u very briefly why u are wrong, mengine yatafuatia kwenye uzi maalum as indicated.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Mchambuzi,

Kwanza nisamehe nimechelewa kujibu nilikuwa na mikutano mingi tangu asubuhi sikuwa nimetulia kutafakari ninayo kujibu. Hoja serikali moja inatokana na sababu za msingi zifuatazo:-
A. Mfumo wa uendeshaji wa serikali muungano :
Mfumo wa huu umegubikwa na political assumption and status quo. Kiasi kwamba baadhi ya mapendekezo yanakuwa magumu kutekelezeka mfano mmoja Joint Finance Account. Ukiangalia mtiririko wa hii uundwaji wa hii account unaona kwamba kuna ugumu mkubwa wa ni jinsi gani utaiendesha hiyo account. Hii ni kwasababu taasisi za muungano nyingi zimeibukia baada ya kuundwa kwa muungano wenyewe. Mfano elimu ya juu, baraza la mitihani, vyama vya siasa, Fedha n.k. Vile vile mfumo wa ugawaji matumizi ya mapato nao ni wachangamoto kwasababu kuna taasisi nyengine za muungano zinafanya kazi Zanzibar tu au Tanganyika. Sasa upelekaji wa fedha katika sekta hizo unatokea zaidi katika mfuko wa muungano kuliko kwa nchi wa washirika. Na likitokea hilo mgharamikiaji mkubwa ni serikali ya Tanganyika na sio Zanzibar ambayo haijawahi kuchangia mfuko wa pamoja tangia mwaka 1967.

B. Mgawanyo wa majukumu na mapato:
Kama unavyofahamu kwa kutumia fiscal policies serikali zetu zinatengeneza njia mbali za kuweza kusimamia na kupatia vyanzo vya mapato. Tanzania sasa hivi tuna parallel fiscal policies ambazo kwa namna moja au nyengine zinatoa changamoto kwa maisha ya mtanzania wa kawaida. Ukichukulia mfumo wa kodi wa Zanzibar unashirikisha taasisi ya ukusanyaji wa mapato ya ZRB, na TRA. Kuna kodi zinakusanywa na TRA na pia ZRB, hata hivyo kodi hizo hizo hazitambuliwi mainland kwasababu inamaanika kuwa wamekusanya wa kiwango cha chini kuliko Tanganyika. Sababu za kwanini zanzibar haikusanyi kodi kwa kiwango sawa na Tanzania Bara hazitajwi. Ibara gani ya kodi inayosema zanzibar wakusanye kodi kwa kiwango cha chini kuliko bara hakuna. Hili ni changamoto kwasababu kwanza linapunguza mapato ya serikali lakini linachangia kuua sekta za Tanzania Bara ambapo wafanyabiashara wanatumia zanzibar kama uchochoro wa kupitisha biashara za magendo. Lakini haya yanasababishwa na kuwepo kwa paralel fiscal policies ambazo zinachangia kwa namna moja au nyengine kutoa mianya ukwepaji kodi. Tungelikuwa serikali moja kodi ingelikuwa moja.

C. Taasisi za muungano:-
Katika taasisi za muungano pia kuna changamoto hasa kuchanganua ni nani anatakiwa kupewa huduma kama mtanzania na asiyekuwa mtanzania. Kwakuwa sheria haitenganishi kati ya mtanzania bara na visiwani na wote wanachukuliwa kama watanzania unakuta serikali ya Tanzania katika mambo yasiyokuwa ya muungano inaendelea kuhudumia wazanzibar hata katika mambo yasiyo ya muungano. Mfano mdogo ni mikopo ya elimu ya juu:-

7.Ministry of Higher Ed, Sc,T 0.44 0.83 0.60 1.50 1.92 1.46 2.07 3.98
8. Ministry of Education and TE 1.89 2.05 2.74 4.72 7.66 0.00 3.75 2.37

Taasisi hizi mbili zinahudumia wanafunzi wa bara na visiwani. Katika figure hizo hapo pesa yote inatokea Tanganyika na mfano elimu ya juu bodi ya mikopo inadhamini hadi wanafunzi kutoka Zanzibar. Mfano mwaka jana kuna wanafunzi zaidi ya 1000 walidhaminiwa na bodi ya mikopo kwenda kusoma vyuo vikuu kutokea zanzibar, mwaka huu wapo wanafunzi 1700 wamedhaminiwa na bodi ya mikopo kutokea Zanzibar. Pesa zinazotoka HESLB ni pesa zinatokea Tanganyika zanzibar haitoi senti tano. Je huu mfumo wa serikali mbili una uhalali wa kuendelea kuwepo? Kwanini tusiwe moja tukayarahisisha maisha na kuhudumia wanafunzi wote kama watanzania.

D. Gharama za Muungano:-
Kama nilivyokuwekea katika jedwali lililopita nimekwambia tunatumia kiasi cha zaidi ya Billioni 717 kwenye taasisi za muungano pekee. Taasisi hizi unadhani zitaendelea kubeba mzigo huu tukiwa ndani ya Serikali moja. Jibu lake ni hapana. Hii ni kwasababu kila taasisi itavunjwa na kuingizwa katika wizara husika. Hakutakuwa na haja ya kuwa na mawaziri wawili wa elimu ndani ya nchi moja. Vile vile mawaziri wa wizara nyengine nao watafutiliwa mbali. Kwa ufupi logic ya hata mtoto mdogo ITAKUAMBIA MOJA NI NDOGO KULIKO MBILI.
 
Mdondoaji,

Nianze kujadili kidogo suala la gharama za serikali moja vis a vis tatu kama ulivyoomba. Nilikuwa nasubiri uniambie analytical framework uliyotumia kufikia hitimisho kwamba serikali moja ni nafuu. Haujaja nayo, hivyo ni dhahiri kwamba hauna.

Unachofananisha wewe nadhani ni sawa na mtu kuwa na gari moja au matatu, ipi ni nafuu zaidi, that's how linear your argument is. In linear terms, ofcourse gari moja ni nafuu kulihudumia mafuta, matengenezo, bima, road tax etc kuliko kuwa na magari matatu. Kwahiyo kama tunajadili a linear relationship, upo sawa.

Suala la serikali carries a multi dimensional aspect. Kuna siasa, masuala ya kijamii ambayo ndani yake kuna diversity, na muhimu zaidi, kuna suala la uchumi, ambalo ndio nguzo kuu, hasa public finance (mapato na matumizi).

Hapo juu umetupia tu bajeti ya serikali in a copy and paste fashion, kama vile unacheza darts - unarusha mshale wa darts, bila ya kujua precisely utatua wapi. Sidhani kama una uhakika umetua wapi na hizo data za bajeti. Ni muhimu uelewe kwamba hata hizo data zimeundwa, usione zinaelea tu kwenye tovuti husika ukazibeba hivyo hivyo tu. Ukipata muda, kaangalie "public expenditure reviews" za kila mwaka uone jinsi gani bajeti zimejaa mapungufu. Nikipata muda nitaya jadili, na baadhi ya mapungufu hayo, Lipumba, Zitto wameyajadili vyema sana ndani ya Bunge la Katiba katika kuonyesha jinsi gani serikali mbili mis-allocate resources. Tutaliangalia hili kwa undani zaidi baadae.

Kwa sasa niseme tu kwamba - unapoleta two autonomous entities in the context of fiscal matters, kwa maana ya tanganyika na znz, efficiency inakuja pale tu iwapo kila upande utapata autonomy fiscal wise. Katika muungano wa two sovereign states, lazima uwe na subnational governments working with the national government. Ndio maana mwalimu aliamua angalau iwepo ya znz, na hii ya Tanganyika, ita sacrifice kubeba muungano in the spirit of "pan-africanism". Ingawa tunapenda kujisifia kwamba sisi ni muungano pekee afrika, ukweli ni kwamba we are a case study of failure. Hii ni kwasababu muungano ulikuwa based on pure political grounds. Uchumi haukuwa considered kama siasa. Tazama katiba ya JMT (1977), haizungumzii hata the basic economic justice ya washirika wa muunngano. Hakuna. Uchumi ulitumikia siasa, basi.

Pia kuna hoja kwamba Tanzania ni jina tulilojipatia wenyewe, sio la mkoloni. Hii hoja ip very weak, hoja ya maana ni je, mipaka ya mkoloni tulifuta? Jibu ni hapana. Isitoshe, Mipaka ya Tanzania Bara ni ile ile ya Tanganyika hivi tunavyozungumza. Muhimu zaidi, Zanzibar wameshasema kwenye katiba yao, mipaka yao ni ile ya kabla ya 1964. Ni kwa maana hii, rasimu pia imeeleza hilo kwa Tanganyika.

Tukirudi kwenye suala la gharama:

Given hoja hapo juu ya haja ya subnational governments working with the central government, fiscal autonomy is what brings about efficiency in allocating resources (public finance matters). Unaweza ukaja na hoja kwamba kuna serikali za mitaa to deal with that - hii argument ni weak kwa sababu, local governments sio suala la muungano na haliwezi kuwa hivyo kwani serikali hizi za mitaa zinaendeshwa na katiba ya ndani ya subnational government (s). Hazina uhusiano na katiba inayoziunganisha pande mbili, tatu, nne za muungano. Lakini suala la kuleta two sovereign states linahitaji katiba ya pamoja. Nilikusoma awali ukijadili your preference ya sera ya majimbo na kwamba ndio solution ya matatizo ya muungano, kwa kuweka serikali moja. Hii ni wishful thought, nitaijadili baadae kidogo.

Iwapo tupo sawa hadi hapa juu ya umuhimu wa fiscal autonomy as a means of efficient allocation of public resources, the devil is in the details, so I will elaborate next:

Serikali kuu, na serikali shiriki - ndio uendesha muungano. Na katika muktadha huu, kila serikali ina competence yake ambayo ni unique, kwa mfano, sio kila aina ya taxes zipo more effective kuendeshwa na serikali kuu. Pia sio kila matumizi yana trickle down effect nzuri yakifanywa na serikali kuu. Yapo maeneo ambayo subnational government ina competence zaidi kuliko serikali kuu, and vice versa holds. Haya ndio mambo nimepanga kuyajadili in details kwenye uzi ujao.

Lakini hapa niseme tu kwamba - serikali moja unayotaka wewe, Kobello, Mzee Mwanakijiji, Pasco, na wengine - wote mna ignore hii factor ya competence in different areas of taxation. Mna amini kwamba uniformity brings more efficiency wakati ukweli ni diversity that brings more efficiency. Mbali na suala la utofauti wa competence, pia lipo suala la upande mmoja kujifunza kutoka kwa fiscal system ya mwenzake badala ya kuweka all eggs in one basket. Faida ni nyingi, nitazijadili kwenye uzi maalum huku nikitumia contemporary data.

Nadhani hadi hapa umepata idea juu ya umuhimu wa uwep wa subnational governments zenye fiscal autonomy na zenye specialization in administering aina fulani fulani ya taxes kutokana na kuwa more competent, huku central government ikibakia na maeneo yake ya competence. Kukosekana kwa mgawanyiko huu ndi chanzo cha serikali mbili kuwa mzigo wa wananchi, na ndio maana nikasema hapo juu kwamba - uhusiano wa idadi ya serikali na gharama kwa wananchi haupo linear kama mnavyodhani.

Kuna haja ya kuwa na serikali tatu kwani kila upande again utatumia competence yake kutokana na geography, resources:
*Human Resources.
*Physical Resources.
*Natural Resources.
*Social Resources (social capital).
*Financial Resources.
*Political Capital.

Msingi wa competence unajengwa na haya, among other things. Ni kutokana na haya, ndio tax bases zitakuwa determined, innovation in mobilization of domestic resources - hasa new sources of revenue, etc.

Na kwa upande wa matumizi - efficiency in allocation pia itakuwa kubwa kwani baina ya serikali kuu na serikali shiriki (mfano Znz), anayejua priority za wananchi ni nini ni znz. Same applies to Tanganyika vis a vis Serikali kuu. Hali hii itapelekea mapato kuwa more transparent, matumizi kuwa monitored vizuri zaidi kwani yanakuwa linked moja kwa moja na local politics, sio hazina ya muungano.

Nadhani hadi hapa unaona jinsi gani serikali moja ni optimally inefficient kwani it means centralization of resources kwa serikali kuu bila ya kujali kama ina more competence katika maeneo ya kodi na matumizi mbalimbali vis a vis serikali shiriki.

Nimalizie na masuala mawili - serikali za majimbo, na serikali za mitaa.

Wewe ni muumini wa serikali za majimbo. With all due respect to Chadema on this one, hii sera haifai katika mazingira ya muungano. Kwanza, itazidisha grievances za zanzibar kwamba inamezwa, kwani it means znz ambayo ni moja ya nchi shiriki za muungano, sasa inageuzwa kuwa ni moja ya majimbo ndani ya muungano. Pili na muhimu zaidi, mabadiliko ya znz kikatiba (2010), wazanzibari hawatarudi nyuma, sio kwa shinikizo la CCM, sio kwa serikali ya muungano, na wala sio kwa nguvu za jeshi.

Na pili - serikali za mitaa. Hizi zimekuwepo kwa muda mrefu sana, zilifutwa baada ya uhuru na kurejeshwa tena 1984. Kuna mafanikio kadhaa yamejitokeza kama vile uboreshaji wa miundo mbinu, ujenzi wa shule, vituo vya afya, lakini ukweli unabakia kwamba mafanikio ya sera hii ni MORE QUANTITATIVE THAN QUALITATIVE. Barabara zimeboreshwa, lakini hazisaidii kupunguza umaskini kwani badala ya kupungua in the last 20 years kwa mfano, umeongezeka. Vituo vya afya vimejengwa vingi lakini hali za afya za wananchi walio wengi leo ni mbaya kuliko miaka ya azimio la arusha. Elimu - shule zimejengwa nyingi sana za kata, hence kuwa ni mafanikio quantitatively, lakini QUALITY wise, we all know nini kinaendelea. Why is it so?

Ni kwa sababu serikali kuu haitaki tekeleza decentalization in practice, it just preaches it. Kwa mfano, halmashauri zote hazina fiscal autonomy. Prioritization inafanywa na serikali kuu, sio na local government. Ushahidi wa hili upo wazi. Pia serikali kuu doesn't encourage local governments kuwa innovative na vyanzo vya mapato, ndio maana unakuta halmashauri ipo kwenye eneo lililojaa rasilimali kubwa lakini sehemu kubwa ya bajeti yake bado inategemea ruzuku ya serikali kuu kuliko vyanzo vya mapato locally. Pia kila mwaka wa fedha tunaona kwamba sehemu kubwa ya fedha zinazengwa hazifiki huko chini. Kwa mwaka huu wa fedha kwa mfano ambao tayari ni mpya, yapo maeneo ya nchi yetu ambayo hayajapata fedha zilizotengwa, maeneo mengi haifiki 60pct ya fedha zilizotengwa. But interestingly enough? Fedha zinazotengwa for nchi jirani ya Zanzibar zinafika kwa wakati, na mara nyingi huwa ni zaidi ya walizotengewa - over 100pct.

Tafadhali nipe muda nipange vizuri analysis yangu juu ya unafuu wa gharama za serikali tatu vis a vis mbili, na hata moja. Nikiwa tayari, nita share accordingly.

Cc MwanaDiwani/@mwigulu nchemba, Nape Nnauye, Ritz, HKigwangalla, Anna Tibaijuka, Ezekiel Maige, Tumaini Makene, Yericko Nyerere, Gamba la Nyoka, Mtanganyika, FJM, Mag3, EMT, JokaKuu, Zakumi

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Again these are bunch of jiber jabber political antics nikuulize maswali yafuatayo uyajumuishe katika
analysis yako :-
a. How many ministries will there be in the country (I mean the entire goverment of the federal government (Tanganyika, Zanzibar na Union).
b. What will be the distribution of revenue kati ya Tanganyika and Zanzibar ndani ya serikali 3.
c. The impact of revenue allocation katika mapato ya serikali ya Tanganyika na Zanzibar ni kwa kiwango gani?
d. Gharama za uendeshaji wa serikali zote tatu kwa ujumla na mgawanyiko wake kutoka hazina zote tatu.
e. Economic cost za jamii kwa mfumo unaopendekeza ukilinganisha na serikali 1, 2, na 3.

I am waiting......
 
Unajua mkuu Mchambuzi,kuna watu wamemcheka mama Mongella alipozungumzia uwingi wa serikali.
Hapa kinachogombewa ni REPUBLICS na siyo governments.

Hii rasimu ya Warioba imeifanya serikali ya muungano kuwa mbali kabisa ya wananchi. Serikali ya muungano chini ya rasimu hii haina carrot wala stick, unless unionyeshe.

Watanzania inabidi tuwe waangalifu mno kwa sababu serikali ya muungano ni symbolic tu unless jamaa waioverhaul rasimu. Kama unajua unachokipigania, sawa.
Serikali moja inawezekana sana tu. Ni kama wayahudi na wapalestina wanavyoweza kuwa ndugu na kuishi pamoja chini ya nchi moja.
It is possible, ila tumejiaminisha tu kuwa haiwezekani.

Kuhusu consistency yangu, I will never guarantee you that. Kadri siku zinavyoenda tutapeana elimu kuhusu umuhimu wa sisi kuwa na serikali moja/jamhuri moja kwa sababu mpaka sasa hivi, tamaa za wanasiasa ndiyo zinachochea serikali tatu na siyo nia ya kuimarisha muungano.
Rasimu ya Warioba ina carrot and stick. Imeonyesha jinsi muungano ulivyo laini na unapoelekea kuvunjika. Katiba ya znz kuwa juu ya katiba ya muungano ni ushahidi mzuri kuwa hakuna muungano. Kuna maafikiano tu , muungano haupo.

Maafikiano yanaweza kufanywa na majirani kuhusu bomba la maji, na wala siyo binding.
Znz imekiuka mkataba wa muungano,dalili nzuri ya kutowepo muungano.

Rasimu ya Warioba imeonyesha matatizo ya muda mrefu ambayo tume 10 hazikuweza kusikilizwa.Leo tunajua muungano ni wa Tanganyika pekee, na znz inatumia inapohitaji msaada.

Rasimu imeeleza uwepo wa fiscal autonomy kati ya washirika kuondoa mizozo isiyo na maana.
Imeonyesha ambavyo mgawanyo wa resource ulivyo na matatizo kwa Tanganyika ambayo inayotoa 100% kwa ajili ya muungano.

Ukitaka kuona carrot and biringanya za rasimu, ni pale inapozungumziwa bila mbadala.
Kwa mfano, watu wanamtuhumu Warioba, S3 kuwa ziyaongeza gharama.
Wakati huo huo hawatuonyeshi S2 zinapunguza vipi gharama.

Pili, tume ya Warioba imeainisha maeneo ya ushirikiano ili kuondoa mizizo,CCM na wewe hamuonyeshi ni vipi mnaondoa kero ikiwa miaka 50 mumeshindwa.

Tatu, tume imeonyesha vyanzo vya serikali ya shirikisho, tumeambiwa ni hafifu, ninyi wa serikali 2 na CCM hamtuonyeshi wapi mapato ya uhakika kwa sasa yanapotoka.

Nne, tume ya Warioba imeonyesha manung'uniko ya Watanganyika juu ya kubebea gharama nzito na mzigo wa kuendesha SMZ. CCM mnachokifanya ni kuongeza pipi na kashata kuwatuliza wznz.

Tume imeonyesha structure nzima ya shirikisho, CCM na Kobello hawaonyeshi structure gani itakayoleta maridhiano. Structure ya sasa ni Tanganyika kubeba muungano kwa mtindo wa changu chetu, chako chako.

Kuelekea serikali moja ni ndoto.Miaka 50 hatujaweza kujenga foundation imara ya kuelekea huko. Kinachoonekana ni hata msingi wa muungano kuvunjika.
Zanzibar haikubali ni sehemu ya Tanzania wala wznz hawakubali ni watanzania, isipokuwa pale wanapohitaji Tanzania. In other words Tanzania ni kama toilet paper, wakishatumia wana flash.

S1 ni ndoto kutokana na ubinafsi wa sehemu moja ya muungano. Utakuwaje na S1 ikiwa mznz hayupo tayari kuacha utaifa wake na sasa wamezidi kugawa hata nchi na Amir jeshi na majeshi?

S1 itawezeakanje ikiwa znz haithamini wala kutambua uwepo wa katiba ya JMT ya sasa.
Hivi huoni kama kuna kudumaa na wala si kwenda mbele

Mchambuzi hatuwezi kulazimisha muungano mimi naona ni kama tunahonga bila kujua sababu. Je kuna faida gani ya Muungano kwa Mtanzania wa kawaidi ambaye ni mkulima mikoani au hata mtu yeyote wa bara kuna faida gani ya muungano kwa sasa naomba mtu anieleze kwasababu sijasikia bado faida za muungano na huu si muungano ni kwasababu upande mmoja tu Zanzibar watu wake wana haki kote. Hivyo muungano ukivunjika sioni hasara kwa sisi wa bara hasa ukuzingatia Wanzanzibar wengi hawautaki muungano
Ni kweli Tanganyika inaonekana kama inaihonga Zanzibar ili kudumisha muungano. Ninachokiona ni kwamba muungano huu unasimama kwa nguvu ya viongozi. Siku alibuka kiongozi mtata basi muungano hautalala hata siku moja....
 
Mchambuzi.
Kwa jinsi ambavyo wachangiaji wa CCM ktk Bunge la Katiba wameshindwa kushawishi kwa hoja za Kisheria na Kikatib, inatosha kumshawishi mtu yeyote makini kwamba CCM haina hata robo dose ya Kero za muungano.

Lakini tunajifunza aina ya wanasiasa walioko ktk chama tawala. Ni wabinafsi sana. Haijalishi amesoma ama aliishia msingi ama ametembea dunia hii na kufanya kazi na watu wasiopenda njia za mkato kiasi gani! Akiingia madarakani anafanya mambo y aibu.

Ni waraka wa watu walevi wa madaraka na wasio penda mijadala huru. Kama utaona hata wanachama wao hawataki wauone waraka wao na waujadili na kutoa mapendekezo.
Kwa mtazamo wangu binafsi, huwezi kuwa mwanachama wa CCM mzuri kama unatumia akili zako vema.
Ili uweze kudumu ndani ya CCM lazima ukubali hukumu na kifungo cha kisiasa.
Lazima useme ndiyo hata kama unaamini ni hapana.

Huwezi kuamini maprofesa, madaktari wa falsafa, matibabu, wanasheria na wachumi wanapoitwa na Nape Nanuye na kuambiwa semeni ABCD kwa formula ya don't ask
Ni mtazamo binafsi tuendelee na mada.
 
Ni kweli Tanganyika inaonekana kama inaihonga Zanzibar ili kudumisha muungano. Ninachokiona ni kwamba muungano huu unasimama kwa nguvu ya viongozi. Siku alibuka kiongozi mtata basi muungano hautalala hata siku moja....
Na kibaya zaidi hongo hiyo ni kwa gharama za Mtanganyika.

Mfano kabla ya March mwaka huu, SMZ ilikuwa inalipa sh 800 milioni kwa gharama za umeme Pemba kwa mwezi.
Baada ya kuungwa na grid ya taifa, SMZ imetua mzigo huo.
Tanesco watabeba gharama hizo kwa kuzipitisha kwa JMT ambayo basically ni Tanganyika. Mambo mawili yatatokea

1. Tanesco itapandisha bei kufidia gharama za umeme wa Pemba ambao mkazi wa Mang'ula hatumii
2. Deni la ndani la taifa litaongezeka na gharama zake atazilipa Mtanganyika kupitia kodi.

Mwaka jana wanafunzi 1000 wa nchi jirani ya znz walikopeshwa na HESLB.
Mwaka huu hongo imeongezeka na sasa ni 1700. Hawa hawapatikani kwa merits, ila kwa sifa za uzanzibar.

Hili si suala la muungano, kwanini uumize wanafunzi 1700 wa Tanganyika ambao baba, mama na dada zao wanapinda migongo kulipa kodi ili hali watoto wao wananyimwa nafasi kwasababu tu si wznz.

Bajeti ya mwaka huu ya SMZ itaongezeka.
Chanzo cha mapato ya znz ni chini ya bilioni 350 kwa sasa, bajeti yao ni bilioni 700.

Hii maana yake kiasi cha bilioni 350 kimechotwa ili kwenda znz. Mwaka huu bajeti yao itaongezwa kama sehemu ya hongo, na kupunguzwa kwako Mtanganyika. Wewe kazi yako ni kulipa kodi na kulinda muundo wa S2.
 
Mkuu Mdondoaji, nitakurudia muda sio mrefu ila briefly kuhusu gharama za serikali moja vis a vis tatu. Lakini in the meantime, naomba unieleze umefikaje kwenye hoja kwamba serikali mbili ni nafuu kuliko tatu, what's your analytical framework? Is is just copying and pasting budget ya muungano na kuijengea hoja husika?
Hili ni swali ambalo CCM na akina Kobello hawalijibu. Tulitaka waonyeshe mbadala wa S3 ya warioba kwa kina, hawawezi.

Kwasababu S2 haina majibu ya nini kifanyike, Rais na CCM wameamua kumfanya Warioba public enemy number 1. Tena si tume ni Warioba kama mtu binafasi.

Kinachoeleweka kwa wananchi ni kitu kimoja, kwanini Warioba anashambuliwa?
Hili la kumtaja Warioba kila siku linampa sana credit mzee huyu. Tena CCM hawazungumzii hotuba ya mwenyekiti wao kwasababu ilikuwa ni hocus pocus

CCM hawawezi ku defend hotuba ya mwenyekiti wao, wanachoweza ni kumdhalilisha Warioba kwa kumwekea maneno. Mfano, rasimu nzima haikutaja kama kutakuwa na marais 3. CCM wanazusha ili Warioba aonekane amefanya fyongo.

Hata hivyo, kwani suala la marais 3 limeanza leo?
Jumbe anachukua cheki hazina
Mwintyo yupo anachukua pesa
Salimin anchukua cheki
Karume anchukua

Utashangaa nikukuambia zinatoka hazina Dar
 
Rasimu ya Warioba ina carrot and stick. Imeonyesha jinsi muungano ulivyo laini na unapoelekea kuvunjika. Katiba ya znz kuwa juu ya katiba ya muungano ni ushahidi mzuri kuwa hakuna muungano. Kuna maafikiano tu , muungano haupo.

Maafikiano yanaweza kufanywa na majirani kuhusu bomba la maji, na wala siyo binding.
Znz imekiuka mkataba wa muungano,dalili nzuri ya kutowepo muungano.

Rasimu ya Warioba imeonyesha matatizo ya muda mrefu ambayo tume 10 hazikuweza kusikilizwa.Leo tunajua muungano ni wa Tanganyika pekee, na znz inatumia inapohitaji msaada.

Rasimu imeeleza uwepo wa fiscal autonomy kati ya washirika kuondoa mizozo isiyo na maana.
Imeonyesha ambavyo mgawanyo wa resource ulivyo na matatizo kwa Tanganyika ambayo inayotoa 100% kwa ajili ya muungano.

Ukitaka kuona carrot and biringanya za rasimu, ni pale inapozungumziwa bila mbadala.
Kwa mfano, watu wanamtuhumu Warioba, S3 kuwa ziyaongeza gharama.
Wakati huo huo hawatuonyeshi S2 zinapunguza vipi gharama.

Pili, tume ya Warioba imeainisha maeneo ya ushirikiano ili kuondoa mizizo,CCM na wewe hamuonyeshi ni vipi mnaondoa kero ikiwa miaka 50 mumeshindwa.

Tatu, tume imeonyesha vyanzo vya serikali ya shirikisho, tumeambiwa ni hafifu, ninyi wa serikali 2 na CCM hamtuonyeshi wapi mapato ya uhakika kwa sasa yanapotoka.

Nne, tume ya Warioba imeonyesha manung'uniko ya Watanganyika juu ya kubebea gharama nzito na mzigo wa kuendesha SMZ. CCM mnachokifanya ni kuongeza pipi na kashata kuwatuliza wznz.

Tume imeonyesha structure nzima ya shirikisho, CCM na Kobello hawaonyeshi structure gani itakayoleta maridhiano. Structure ya sasa ni Tanganyika kubeba muungano kwa mtindo wa changu chetu, chako chako.

Kuelekea serikali moja ni ndoto.Miaka 50 hatujaweza kujenga foundation imara ya kuelekea huko. Kinachoonekana ni hata msingi wa muungano kuvunjika.
Zanzibar haikubali ni sehemu ya Tanzania wala wznz hawakubali ni watanzania, isipokuwa pale wanapohitaji Tanzania. In other words Tanzania ni kama toilet paper, wakishatumia wana flash.

S1 ni ndoto kutokana na ubinafsi wa sehemu moja ya muungano. Utakuwaje na S1 ikiwa mznz hayupo tayari kuacha utaifa wake na sasa wamezidi kugawa hata nchi na Amir jeshi na majeshi?

S1 itawezeakanje ikiwa znz haithamini wala kutambua uwepo wa katiba ya JMT ya sasa.
Hivi huoni kama kuna kudumaa na wala si kwenda mbele

Tatizo ni hotuba zilizojaa emotions.
Ukiuliza maswali najibu, halafu yanaishia hapo hapo. Mpaka sasa hivi hamjaonyesha legitimacy ya conclusions za Warioba, mapiga kelele na maandishi mengi ambayo hata watu wengi wanashindwa kuelewa.

Kama lengo ni kueleweshana, twende taratibu aya kwa aya, issue kwa issue bila kuchukizwa na msimamo wa mtu. Nikisema conclussions za Warioba ziko flawed, nimeonyesha ni kwanini.

Nikaambiwa mbona zake zinafanana na Afrobarometer? ... nikaleta link ya Afrobarometer inayoonyesha 14% ndiyo wanaotaka serikali 3 according to the same Afrobarometer.

Mimi nakubali kuwa, watanzania wanaotaka serikali 3 wanaongezeka kwa kasi kutokana na propaganda zinazoendelea zikichangiwa na ubovu wa mfumo wa serikali mbili.

Hata hivyo, bado takwimu za tume ya katiba hazitupi conclussion hiyo, msilazimishe.

Mwisho kabisa, na muhimu kwa sasa hivi, ni wewe kunielezea Carrot ni ipi na Stick ni ipi kwa serikali ya muungano kama ilivyopendekezwa. La sivyo, hiyo serikali itakuwa ni one of the biggest bureaucratic monster that has no meaning apart from symbolism.

Ichallenge you to show me the carrot and the stick.
 
Back
Top Bottom