Mdondoaji,
Nianze kujadili kidogo suala la gharama za serikali moja vis a vis tatu kama ulivyoomba. Nilikuwa nasubiri uniambie analytical framework uliyotumia kufikia hitimisho kwamba serikali moja ni nafuu. Haujaja nayo, hivyo ni dhahiri kwamba hauna.
Unachofananisha wewe nadhani ni sawa na mtu kuwa na gari moja au matatu, ipi ni nafuu zaidi, that's how linear your argument is. In linear terms, ofcourse gari moja ni nafuu kulihudumia mafuta, matengenezo, bima, road tax etc kuliko kuwa na magari matatu. Kwahiyo kama tunajadili a linear relationship, upo sawa.
Suala la serikali carries a multi dimensional aspect. Kuna siasa, masuala ya kijamii ambayo ndani yake kuna diversity, na muhimu zaidi, kuna suala la uchumi, ambalo ndio nguzo kuu, hasa public finance (mapato na matumizi).
Hapo juu umetupia tu bajeti ya serikali in a copy and paste fashion, kama vile unacheza darts - unarusha mshale wa darts, bila ya kujua precisely utatua wapi. Sidhani kama una uhakika umetua wapi na hizo data za bajeti. Ni muhimu uelewe kwamba hata hizo data zimeundwa, usione zinaelea tu kwenye tovuti husika ukazibeba hivyo hivyo tu. Ukipata muda, kaangalie "public expenditure reviews" za kila mwaka uone jinsi gani bajeti zimejaa mapungufu. Nikipata muda nitaya jadili, na baadhi ya mapungufu hayo, Lipumba, Zitto wameyajadili vyema sana ndani ya Bunge la Katiba katika kuonyesha jinsi gani serikali mbili mis-allocate resources. Tutaliangalia hili kwa undani zaidi baadae.
Kwa sasa niseme tu kwamba - unapoleta two autonomous entities in the context of fiscal matters, kwa maana ya tanganyika na znz, efficiency inakuja pale tu iwapo kila upande utapata autonomy fiscal wise. Katika muungano wa two sovereign states, lazima uwe na subnational governments working with the national government. Ndio maana mwalimu aliamua angalau iwepo ya znz, na hii ya Tanganyika, ita sacrifice kubeba muungano in the spirit of "pan-africanism". Ingawa tunapenda kujisifia kwamba sisi ni muungano pekee afrika, ukweli ni kwamba we are a case study of failure. Hii ni kwasababu muungano ulikuwa based on pure political grounds. Uchumi haukuwa considered kama siasa. Tazama katiba ya JMT (1977), haizungumzii hata the basic economic justice ya washirika wa muunngano. Hakuna. Uchumi ulitumikia siasa, basi.
Pia kuna hoja kwamba Tanzania ni jina tulilojipatia wenyewe, sio la mkoloni. Hii hoja ip very weak, hoja ya maana ni je, mipaka ya mkoloni tulifuta? Jibu ni hapana. Isitoshe, Mipaka ya Tanzania Bara ni ile ile ya Tanganyika hivi tunavyozungumza. Muhimu zaidi, Zanzibar wameshasema kwenye katiba yao, mipaka yao ni ile ya kabla ya 1964. Ni kwa maana hii, rasimu pia imeeleza hilo kwa Tanganyika.
Tukirudi kwenye suala la gharama:
Given hoja hapo juu ya haja ya subnational governments working with the central government, fiscal autonomy is what brings about efficiency in allocating resources (public finance matters). Unaweza ukaja na hoja kwamba kuna serikali za mitaa to deal with that - hii argument ni weak kwa sababu, local governments sio suala la muungano na haliwezi kuwa hivyo kwani serikali hizi za mitaa zinaendeshwa na katiba ya ndani ya subnational government (s). Hazina uhusiano na katiba inayoziunganisha pande mbili, tatu, nne za muungano. Lakini suala la kuleta two sovereign states linahitaji katiba ya pamoja. Nilikusoma awali ukijadili your preference ya sera ya majimbo na kwamba ndio solution ya matatizo ya muungano, kwa kuweka serikali moja. Hii ni wishful thought, nitaijadili baadae kidogo.
Iwapo tupo sawa hadi hapa juu ya umuhimu wa fiscal autonomy as a means of efficient allocation of public resources, the devil is in the details, so I will elaborate next:
Serikali kuu, na serikali shiriki - ndio uendesha muungano. Na katika muktadha huu, kila serikali ina competence yake ambayo ni unique, kwa mfano, sio kila aina ya taxes zipo more effective kuendeshwa na serikali kuu. Pia sio kila matumizi yana trickle down effect nzuri yakifanywa na serikali kuu. Yapo maeneo ambayo subnational government ina competence zaidi kuliko serikali kuu, and vice versa holds. Haya ndio mambo nimepanga kuyajadili in details kwenye uzi ujao.
Lakini hapa niseme tu kwamba - serikali moja unayotaka wewe,
Kobello,
Mzee Mwanakijiji,
Pasco, na wengine - wote mna ignore hii factor ya competence in different areas of taxation. Mna amini kwamba uniformity brings more efficiency wakati ukweli ni diversity that brings more efficiency. Mbali na suala la utofauti wa competence, pia lipo suala la upande mmoja kujifunza kutoka kwa fiscal system ya mwenzake badala ya kuweka all eggs in one basket. Faida ni nyingi, nitazijadili kwenye uzi maalum huku nikitumia contemporary data.
Nadhani hadi hapa umepata idea juu ya umuhimu wa uwep wa subnational governments zenye fiscal autonomy na zenye specialization in administering aina fulani fulani ya taxes kutokana na kuwa more competent, huku central government ikibakia na maeneo yake ya competence. Kukosekana kwa mgawanyiko huu ndi chanzo cha serikali mbili kuwa mzigo wa wananchi, na ndio maana nikasema hapo juu kwamba - uhusiano wa idadi ya serikali na gharama kwa wananchi haupo linear kama mnavyodhani.
Kuna haja ya kuwa na serikali tatu kwani kila upande again utatumia competence yake kutokana na geography, resources:
*Human Resources.
*Physical Resources.
*Natural Resources.
*Social Resources (social capital).
*Financial Resources.
*Political Capital.
Msingi wa competence unajengwa na haya, among other things. Ni kutokana na haya, ndio tax bases zitakuwa determined, innovation in mobilization of domestic resources - hasa new sources of revenue, etc.
Na kwa upande wa matumizi - efficiency in allocation pia itakuwa kubwa kwani baina ya serikali kuu na serikali shiriki (mfano Znz), anayejua priority za wananchi ni nini ni znz. Same applies to Tanganyika vis a vis Serikali kuu. Hali hii itapelekea mapato kuwa more transparent, matumizi kuwa monitored vizuri zaidi kwani yanakuwa linked moja kwa moja na local politics, sio hazina ya muungano.
Nadhani hadi hapa unaona jinsi gani serikali moja ni optimally inefficient kwani it means centralization of resources kwa serikali kuu bila ya kujali kama ina more competence katika maeneo ya kodi na matumizi mbalimbali vis a vis serikali shiriki.
Nimalizie na masuala mawili - serikali za majimbo, na serikali za mitaa.
Wewe ni muumini wa serikali za majimbo. With all due respect to Chadema on this one, hii sera haifai katika mazingira ya muungano. Kwanza, itazidisha grievances za zanzibar kwamba inamezwa, kwani it means znz ambayo ni moja ya nchi shiriki za muungano, sasa inageuzwa kuwa ni moja ya majimbo ndani ya muungano. Pili na muhimu zaidi, mabadiliko ya znz kikatiba (2010), wazanzibari hawatarudi nyuma, sio kwa shinikizo la CCM, sio kwa serikali ya muungano, na wala sio kwa nguvu za jeshi.
Na pili - serikali za mitaa. Hizi zimekuwepo kwa muda mrefu sana, zilifutwa baada ya uhuru na kurejeshwa tena 1984. Kuna mafanikio kadhaa yamejitokeza kama vile uboreshaji wa miundo mbinu, ujenzi wa shule, vituo vya afya, lakini ukweli unabakia kwamba mafanikio ya sera hii ni MORE QUANTITATIVE THAN QUALITATIVE. Barabara zimeboreshwa, lakini hazisaidii kupunguza umaskini kwani badala ya kupungua in the last 20 years kwa mfano, umeongezeka. Vituo vya afya vimejengwa vingi lakini hali za afya za wananchi walio wengi leo ni mbaya kuliko miaka ya azimio la arusha. Elimu - shule zimejengwa nyingi sana za kata, hence kuwa ni mafanikio quantitatively, lakini QUALITY wise, we all know nini kinaendelea. Why is it so?
Ni kwa sababu serikali kuu haitaki tekeleza decentalization in practice, it just preaches it. Kwa mfano, halmashauri zote hazina fiscal autonomy. Prioritization inafanywa na serikali kuu, sio na local government. Ushahidi wa hili upo wazi. Pia serikali kuu doesn't encourage local governments kuwa innovative na vyanzo vya mapato, ndio maana unakuta halmashauri ipo kwenye eneo lililojaa rasilimali kubwa lakini sehemu kubwa ya bajeti yake bado inategemea ruzuku ya serikali kuu kuliko vyanzo vya mapato locally. Pia kila mwaka wa fedha tunaona kwamba sehemu kubwa ya fedha zinazengwa hazifiki huko chini. Kwa mwaka huu wa fedha kwa mfano ambao tayari ni mpya, yapo maeneo ya nchi yetu ambayo hayajapata fedha zilizotengwa, maeneo mengi haifiki 60pct ya fedha zilizotengwa. But interestingly enough? Fedha zinazotengwa for nchi jirani ya Zanzibar zinafika kwa wakati, na mara nyingi huwa ni zaidi ya walizotengewa - over 100pct.
Tafadhali nipe muda nipange vizuri analysis yangu juu ya unafuu wa gharama za serikali tatu vis a vis mbili, na hata moja. Nikiwa tayari, nita share accordingly.
Cc
MwanaDiwani/@mwigulu nchemba,
Nape Nnauye,
Ritz,
HKigwangalla,
Anna Tibaijuka,
Ezekiel Maige,
Tumaini Makene,
Yericko Nyerere,
Gamba la Nyoka,
Mtanganyika,
FJM,
Mag3,
EMT,
JokaKuu,
Zakumi
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums